KABUL, Afghanistan
WATU watatu
wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko katika uwanja
wa ndege wa kimataifa uliopo mjini Kabul.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema
mtu mmoja alijitoa mhanga kwa kujilipua ambapo aliwalenga wanajeshi wa
kimataifa nje ya lango kuu la uwanja huo.
Lango hilo hutumiwa na vikosi vya
kijeshi vya kigeni, ambapo bado haijabainika endapo walinusurika na shambulio
hilo.
Msemaji wa polisi alisema, shambulio
hilo lilifanyika karibu na ofisi za safari za ndege nchini humo zilizoko nje ya
uwanja.
Shambulizi hilo linafanyika ikiwa
ni siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja kuwaua watu 14 wakiwemo raia tisa wa
kigeni mjini humo.
No comments:
Post a Comment