Wednesday 4 September 2013

JK kuanza ziara ya kutembelea miradi


NA PETER KATULANDA, MWANZA
RAIS Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kuanza ziara ya kiserikali ya siku saba mkoani hapa, ambapo atakagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, iliyotekelezwa kufuatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Rais ambaye alitarajiwa kuwasili jijini hapa jana, asubuhi baadaye kwenda nchini Uganda kukutana na Rais Yoweri Mseveni, kabla ya kurejea hapa leo, ambapo anatarajia kuanza ziara hiyo kesho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa, Mhandisi Evarist Ndikilo, Rais Kikwete atatembelea wilaya zote ili kujionea shughuli za maendeleo, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Wilaya hizo ni Sengerema, Ukerewe, Nyamagana, Ilemela, Misungwi, Magu na Kwimba.
Ndikilo alizitaja shughuli hizo kuwa miradi ya nishati ya umeme ya MCC, inayofadhiliwa na serikali ya Marekani inayotekelezwa katika wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Sengerema ambapo utazinduliwa katika Kijiji cha Bukokwa.
ìMradi mwingine wa umeme utakaozinduliwa na Mheshimiwa Rais ni wa megawati 60 uliojengwa Nyakato wilayani Ilemala, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kitega uchumi hapa na kufungua hoteli ya Golden Crest iliyopo kwenye jengo la PPF Plaza,î alisema Ndikilo.
Aliongeza kuwa, katika sekta ya afya, atafungua jengo la zahanati ya Lugeye wilayani Magu, maabara ya hospitali ya wilaya ya Ukerewe na kuzindua X-ray mbili, ikiwemo ya kisasa iliyotolewa na Denmark kwa ufadhili wa  Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga.
X-ray nyingine ndogo ilinunuliwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya hospitali ya Mitindo wilayani humo, na kufungua shule ya msingi ya Ntulya iliyojengwa na shirika la African School House ya Marekani kupitia mbunge huyo.
Aidha, Raqis Kikwete atafungua kituo kipya cha Polisi Nyakato, mradi wa maji wa Kaatunguru wilayani Sengerema, uwanja wa ndani wa michezo Malya wilayani Kwimba na kuweka jiwe la msingi katika Kanisa la Kisabato Pasiansi wilayani Ilemela.
ìKatika maeneo hayo, Rais atazungumza na wananchi, hivyo natoa wito kwao kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza, hii ni fursa pekee kwa wana-Mwanza kujionea shughuli za maendeleo yao zilivyotekelezwa na serikali yetu kama utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,î alieleza Ndikilo.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru