Sunday, 17 May 2015

Wanaume “vicheko” KenyaWANAUME nchini hapa wamepokea kwa furaha kusainiwa kwa sheria itakayokabiliana na vitendo vya unyanyasaji hususan majumbani.
Sheria hiyo iliyosainiwa na wiki iliyopita na rais Uhuru Kenyata, inatarajiwa kuwapa ahuweni wanaume waliokuwa wakipigwa na wake zao na kushindwa kuripoti matukio hayo polisi.
Matukio ya wanaume nchini Kenya kupigwa na wake zao yamezidi kuongezeka na kuhatarisha amani katika familia.
Baadhi ya wanaume walisema wamekuwa wakipigwa na wake zao mara kwa mara na kuwafanya kutokua na amani kwenye ndoa zao.
Walisema kinga hiyo ya kisheria itakuwa ni fundisho kwa wanawake wenye kuendekeza tabia za kuwapiga kwa kudai kuwa wameshindwa kutimiza mahitaji ya ndoa na familia madai ambayo wameyakataa.
Kukithiri kwa matukio hayo kunasababisha kuanzishwa chama cha kutetea haki za wanaume na kutaka kuitishwa kwa mgomo wa wanaume kwenye ndoa mpaka sheria hiyo itakapopitishwa.
Mmoja wa waathirika wa vipigo hivyo ni Simon Kiguta, ambaye alipigwa na kujeruhiwa vibaya na mkewe ambapo tukio hilo liliamsha hasira za wanaume wengi nchini hapa.

1 comments: