Sunday, 17 May 2015

Wakimbizi wa Burundi wahifadhiwa Lake TanganyikaKUFUATIWA kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi kutoka Burundi, uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika, umetumika kwa muda kuhifadhia wakimbizi wakati wakipatiwa msaada wa chanjo na matibabu.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR, idadi ya watu 100,000 wamekimbia nchini Burundi kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea.
Idadi kubwa ya wakimbizi hao wamepokelewa nchini Tanzania huku wengine wakikimbilia nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda. Msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Karin de Gruijl alisema idadi imeongezeka zaidi siku chache zilizopita huku wengine wakiishi kwenye fukwe za Ziwa Tanganyika.
Alisema kufuati hali hiyo, wengine wamehifadhiwa kwa muda kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa ajili ya chanjo, ukaguzi na baadae watapelekwa kwenye kambi za wakimbizi.
Alisema malori 17, yaliyobeba vifaa muhimu kama vile vyandarua dawa na mahema yanapelekwa Kigoma.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru