Hispania
yaridhishwa
na
kazi ya TASAF
SERIKALI ya Hispania imeridhishwa na
utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya mbalimbali nchini
ambao unatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).
Akizungumza baada ya kutembelea baadhi ya
vijiji vya Wilaya ya Bagamoyo kwa
wanufaika wa mpango huo, Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis, alisema mpango huo unaonyesha unatekelezwa
kikamilifu na kwa mafanikio makubwa.
Alisema lengo la serikali ya Hispania na
nchi nyingine wafadhili ni kuona umasikini unapungua kwa kasi nchini Tanzania
na ikiwezekana kuutokomeza, ifikapo mwaka 2025.
“Tumeridhishwa na utekelezaji wa mpango,
kwani tumepata fursa ya kuzungumza na
walengwa kutoka kaya masikini na kutudhihirishia manufaa yake,” alisema.
Naye Mkurugenzi wa TASAF,Ladislaus
Mwamanga, alisema mpango wa kunusuru kaya masikini na uhawilishaji fedha ni
moja ya mipango ya serikali katika
kuhakikisha inapunguza wimbi la umasikini
Mwamanga alisema utekelezaji wa mpango
huo umekuwa ukitekelezwa katika njia kuu mbili, ikiwemo mpango wa kunusuru kaya
masikin na mpango wa utoaji wa ajira za muda.
Naye Mratibu Mkazi wa Shirika Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Maendeleo(UNDP),Alvaro Rodriguez,
aliipongeza jamii katika
maeneo waliyoyatembelea na kueleza kwamba
kila penye mafanikio panahitaji mipango ya uhakika .
Alisema jambo kubwa ni kuweka
dhamira ya kweli katika ushiriki na utekelezaji wa mpango huo,
hivyo wanapaswa kuupiga vita umasikini kwa vitendo.