Wednesday 18 March 2015

Bil. 1.8 zajenga miundombinu ya maji


SERIKALI imetumia sh. bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Kibirizi wilayani Bukoba.
Fedha hizo zimetumika kuchimba mitaro saba yenye urefu wa kilometa 84 na magati 110, tanki za kuhifadhia huku kazi iliyobaki kwa sasa ni kulaza mabomba na kujenga magati 15.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Agrey Mwanri, alisema bungeni jana kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha wakazi wa kijiji hicho wanapata maji safi na salama.
Alikuwa akijibu swali la Jasson Rweikiza (Bukoba Vijijini-CCM), aliyetaka kujua mpango wa dharura wa saerikali kuwapatia maji wakazi wa vijiji vya Omubweya, Kibirizi na Rugaze.
Mwanri alisema miradi hiyo iko kwenye hatua mbalimbali ili kuhakikisha vijiji hivyo vinapata majisafi na salama na kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru