Wednesday 18 March 2015

Ufinyu wa bajeti kikwazo



UFINYU wa bajeti ya serikali umeelezwa kuwa kikwazo kwa wanafunzi wanaosoma kwa lugha za kigeni kupata mafunzo kwa vitendo.
Hata hivyo, serikali imesema jitihada mbalimbali zinaendelea kufanywa ili kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma kwa vitendo.
Kusoma kwa vitendo ni njia mojawapo ya njia za kumwezesha mwanafunzi kuwa na uelewa mpana.


Hayo yalielezwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango-Malecela.

Alisema Sera ya Elimu aliyoiwasilisha mezani imeweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi kuanzia ngazi ya awali wanajifunza kwa lugha za kigeni.
Anne alikuwa akijibu swali la Suzan Lyimo (Viti Maalum- CHADEMA), aliyehoji mikakati ya serikali kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaofundishwa kwa lugha za kigeni kama Kichina, Kiarabu na Kifaransa.
Anne alisema Chuo Kikuu cha Dodoma kilikuwa tayari kutoa mafunzo ya lugha hizo, lakini kikwazo kikubwa kilikuwa kuwapata wanafunzi.
Alisema UDOM ilijipanga kuanza kutoa mafunzo ya lugha ya kiarabu katika mwaka wa masomo wa 2008/ 2009 na mwaka 2009/2010.
“Kundi la kwanza la wanafunzi wa shahada ya sanaa katika lugha ya Kiarabu lilipatikana mwaka wa masomo 2010/11, ambapo wanafunzi sita tu ndio walidahiliwa,” alisema 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru