Thursday 3 July 2014

Bei ya umeme kuanza kushuka


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Pan African Power Solutions (PAP) imesema bei ya umeme inaweza kuanza kushuka kutokana na ongezeko la umeme katika gridi ya taifa.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam, jana, na Mwanasheria Mkuu wa PAP, Joseph Makandege alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa kampuni hiyo.
PAP ilianza kuzalisha umeme baada ya kununua mitambo ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Hali hiyo inafuatia PAP kuzalisha megawati 100 ambazo ni kiwango cha juu cha uwezo wa mitambo yake.
Uzalishaji wa kiwango cha juu ulifikiwa Juni 15, mwaka huu ambapo uogozi wa PAP umesema  unaendelea kutekeleza mpango mkakati wake  kwa awamu.
“Juni 15, mwaka huu, mitambo ya IPTL iliyopo eneo la Tegeta, ilianza kuzalisha megawati 100 za umeme, ambazo ndiyo uwezo wa mitambo hiyo. Hii ni moja ya ahadi zilizotolewa na uongozi wa PAP wakati wa ununuzi wa mitambo ya IPTL,” alisema Makandege.
Alisema IPTL ambayo inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Pan African Power Solutions Tanzania Limited, inaendelea na jitihada zake za kutimiza ahadi yake ya kuwapunguzia wateja adha ya gharama ya umeme.
“Tumepanga kuzalisha megawati 200 kwa kutumia mitambo inayoendeshwa kwa kutumia gesi ifikapo Desemba 2015, ambapo tutauza umeme  kwa chini ya dola nane za kimarekani, ikiwa ni awamu ya kwanza ya upanuzi wa huduma.
Katika awamu ya pili, kampuni hiyo imejiwekea malengo kuzalisha megawati 300.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru