Tuesday 15 July 2014

Mtawa, dereva kizimbani kwa ukatili wa kijinsia


NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
MTAWA wa Kanisa Katoliki la Shirika la Watawa la Wamisionari wa Augustino, Flora Karimi (38), amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia. 
Flora (38), ambaye ni Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Monica ya Moshono, jijini Arusha, na dereva wa shule hiyo, Yasin Mswaiki (36), walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha.
Wakili wa Serikali, Sabina Silayo, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Jasmin Abdul kuwa Mswaki, ambayec ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, anakabiliwa na makosa mawili aliyoyatenda kwa siku tofauti wakati wa saa za kazi. 
Sabina aliyataja makosa hayo kuwa ni kuwaingizia vidole watoto wa kike katika sehemu zao za siri.
Katika kosa la kwanza, wakili hiyo alidai kuwa dereva huyo alimwingizia vidole mtoto mwenye umri wa miaka minne  na nusu (jina linahifadhiwa) katika basi la shule kwa siku na saa isiyojulikana, wakati ama wa kwenda shuleni au kurudi nyumbani.
Aidha alidai katika kosa la pili, dereva huyo alimwingizia vidole mtoto mwingine (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka mine katika basi la shule wakati akiwarejesha nyumbani au kuwapeleka shuleni. 
Kwa upande wa Mtawa Flora, Sabina alidai kuwa ameunganishwa katika kesi kutokana na uzembe wa kushindwa kuzuia kosa hilo kutendeka. Alidai kuwa kwa nafasi yake akiwa mwalimu mkuu wa shule, alipaswa kuhakikisha usalama wa wanafunzi wake.
Washitakiwa hao walikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana hadi Agosti 27, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.
Walitakiwa kuwa na wadhamini wawili wawili na kutia saini bondi ya sh. 500,000 kila moja, masharti ambayo waliyatimiza. 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru