Alisema
wajumbe wote wanaotoka katika UKAWA
ambao wamehudhuria vikao vya bunge hilo, wanaelewa kuhusu maslahi ya
nchi kwanza, ni wazalendo na hawapaswi
kukashifiwa.
Mrema: Nina akili
timamu
Mbunge
wa Vunjo, Agustino Mrema amewaeleza wananchi wake kuwa ana akili timamu na
hawezi kususia vikao kama wajumbe wa UKAWA.
Mrema,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP, alisema jana kuwa kitendo cha UKAWA kususa
bunge hilo ni kuwanyima haki za msingi za uwakilishi kwa wananchi
waliowachagua.
Alisema
yeye amechaguliwa na wananchi wa Vunjo kwa ajili ya kuwatetea na kuwasemea
matatizo yao, kama anavyofanya katika vikao mbalimbali vya bunge na sio kugomea
vikao na kutoka nje.
“Wapo
watu wamekuwa wakinisema kuwa sifai kuwaongoza wananchi wangu, kwa sababu
natumiwa na CCM kuwakandamiza ndio maana sijaungana na UKAWA, lakini najua hao
wamekosa ya kusema,” alisema Mrema.
JUKATA laonya katiba si mradi
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)
limesema mchakato wa kuandika katiba mpya sio mradi wa mtu binafsi au chama
chochote bali ni mradi endelevu wa watanzania wote.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deus
Kibamba, aliyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini
hapa kuhusiana na mchakato wa katiba.
Kibamba alisema katiba mpya ya
kidemokrasia na yenye viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Rais Jakaya kikwete
wakati wa kuanzisha kwa mchakato huo ni muhimu kuzingatiwa.
Alisema hakuna sababu ya kuharakisha
kupatikana kwa katiba hiyo ili itumike katika uchaguzi mkuu ujao kwani muda
uliobaki ni mfupi kukamilisha katiba.
Aidha Kibamba alisema bado
kunahitajika mazungumzo ya kina ili kufikia maridhiano kati ya UKAWA na bunge katika
kuhakikisha katiba inapatikana.
Alisema hivi sasa pamoja na
kuendelea kwa juhudi mbalimbali bado UKAWA wameonyesha kutorejea na hivyo
kuvitaka vyama hivyo kujali maslahi ya watanzania.
Kwa mujibu wa Kibamba hivi sasa kuna
mpasuko ndani ya UKAWA kwani, baadhi ya wabunge wanaoamini kuwa Bunge maalumu
la katiba halipaswi kuendelea kwa sasa lakini pia wapo ambao wameona ni vyema
kuhudhuria.
"Haikuwa kwa mashangao
kushuhudia wajumbe watatu kutoka kundi la UKAWA wakitinga bungeni na kujiandikisha
ili kuendelea na vikao," alisema.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru