NA SELINA WILSON
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika kata 27, ambapo CCM imeshinda kata 23.
Katibu wa kamati kuu NEC (CCM) itikadi na uenezi, Nape Nnauye akiteta jambo. |
Kimesema siri ya kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema hayo na kuongeza kuwa matokeo hayo ni ushahidi kwamba CCM inakubalika zaidi na Watanzania walio wengi.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.
Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo na Santillya (Mbeya).
Zingine ni Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro), Mrijo (Dodoma).
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru