Na Shomi Mtaki, Tunduma
SERIKALI mkoani Mbeya imewaagiza viongozi kuwakamata na kuwachukulia hatua wavamizi wanaochimba kokoto katika barabara ya Sumbawanga-Tunduma.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, mjini Tunduma baada ya kuwanasa baadhi ya watu wakichimbua kokoto katika eneo la Mwaka akiwa safarini kwenda Kapele kukagua miradi ya maendeleo.Alisema watu hao hawatakiwi kufumbiwa macho kwa kuwa wameanza kufanya uharibifu mkubwa, ambao umesababisha athari kubwa wakati wa kuitumia.
Awali, Mhandisi wa Kampuni ya CCC, Eliazary Rweikiza, alisema wavamizi hao wamekuwa wakichimba na kozoa mchanga usiku na mchana.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamedai kuwa wavamizi hao wamekuwa wakikusanya malighafi hiyo na kwenda kuziuza kwa bei ya sh 5000 kwa kiroba cha kilo tano.
Sunday, 16 February 2014
RC Kandoro acharuka
21:48
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru