Pata mafanikio, tangaza hapa
Tangaza nasi hapa.
Pata mafanikio, tangaza hapa
Tangaza nasi hapa.
Pata mafanikio, tangaza hapa
Tangaza nasi hapa.
Pata mafanikio, tangaza hapa
Tangaza nasi hapa.
Tuesday, 23 December 2014
MAONI YA MHARIRI
02:44
No comments
Taasisi zilizoagizwa kuwachunguza watuhumiwa wa Escrow zitende haki.....!
"HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ameweka hadharani mambo yote kuhusiana na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kuchukua hatua kwa baadhi ya watendaji.
Akihutubia mkutano wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Rais
Kikwete, alimvua uwaziri Profesa Anna Tibaijuka kutokana na kuhusishwa katika
kashfa hiyo na watendaji wengine wakiendelea kuchunguzwa.
Pia, aliagiza hatua kadhaa kuchukuliwa ili kuhakikisha
serikali inapata halali yake kwenye mambo ambayo yalizusha utata baada ya
sakata hilo kuibuka na kutikisa nchi.
Kabla ya hatua hiyo, sakata la akaunti ya Tegeta Escrow
lilifikishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambaye
baada ya uchunguzi aliwasilisha ripoti iliyopelekwa bungeni na ambako maazimio
kadhaa yalifikiwa.
Ni ukweli usiopingika kuwa katika sakata hilo kuna baadhi ya
watu na wanasiasa ambao walitaka kulikuza na kuliongeza chumvi, lengo likiwa
kuwakomoa baadhi ya watendaji kwa kutaka wawajibishwe.
Walio katika kundi hilo, walihakikisha wanatumia mbinu na kila
aina ikiwemo kuvumisha na kusingizia wengine uongo huku wakijua wanafanya hivyo
kwa makosa, lakini walitaka kushinikiza malengo yao kutimia.
Wapo waliotetea na kutaka kuona haki inatendeka na ambao
baadhi yao walijitoa kimasomaso kuhakikisha waliotenda makosa wanaadhibiwa
badala ya kuwahusisha waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mkumbo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Frederick Werema, kwa
kutambua kuwa ushauri wake haukueleweka kiasi cha kusababisha mtafaruku kwa
busara aliamua kujiuzulu.
Hata hivyo, kutokana na sababu ambazo baadhi ya wahusika
wanazijua, walishinikiza kutaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, nao wajiuzulu kwa sababu walisema fedha
zile hazikuwa za umma.
Kauli ya Rais Kikwete kuwa fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya
Tegeta Escrow hazikuwa za umma bali za Kampuni ya Independent Power Tanzania
(IPTL) inamaliza utata ulioibuka kuhusiana na fedha hizo.
Kwa hiyo, suala hilo limewekwa hadharani na kila kitu
kimeelezwa, hivyo kilichobaki ni kuacha kuumiza vichwa kwa jambo ambalo
limeshapatiwa ufumbuzi kwani mwenye fedha ameshachukua na kinachotakiwa sasa ni
kuendelea kuumiza vichwa ili kuona ni kwa namna gani wananchi wengi watanufaika
na nishati ya umeme tena kwa bei nafuu.
Pia, utaratibu unaotaka kuota mizizi hivi sasa na hasa kwa
wafanyabiashara na wanasiasa kuviziana na ‘kuumizana’ kwa sababu za maslahi
binafsi unapaswa kuepukwa ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Escrow imefungwa na watu wanapaswa kuacha nongwa na badala
yake kujikita katika jitihada za kujikwamua kiuchumi badala ya kuendelea
kulumbana kwa mambo ambayo hayana faida.
Kwa mamlaka zilizopewa majukumu ya uchunguzi, zinapaswa kukamilisha majukumu yake na kujendelea na taratibu nyingine ili kuona haki ikitendeka."
Hizi ni salamu kwa watendaji wazembe
02:42
No comments
NA KHADIJA MUSSA
RAIS Jakaya Kikwete, amesema watendaji watakaozembea
katika kutelekeza majukumu yao watashughulikiwa kikamilifu.
Amesema watendaji wanapaswa kufahamu kuwa serikali
ipo na hukasirishwa pindi mambo yanapokwenda kinyume na matarajio.
Pia amesema ameridhishwa na hatua zilizochukuliwa na
Waziri wa Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, wa kutengua nafasi za
wakurugenzi sita, kusimamia wengine na kutoa onyo kali.
Akizungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, jana,
Rais Kikwete alisema, uamuzi wa kuwatimua kazi wakurugenzi hao ulistahili na
umefanyika kwa wakati mwafaka.
Alisema hatua hiyo itakuwa fundisho kwa watandaji
wengine waliopewa dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali ikiwemo uchaguzi.
“Uamuzi huu ni sahihi kabisa na nimeubariki…haiwezekani watu wanaharibu kazi na serikali ikae kimya. Hawa tumewapa jukumu la kusimamia uchaguzi na mwakani ndio watasimamia uchaguzi mkuu, sasa tukiacha mambo yaende hivi tutaharibikiwa,” alisema.
Alisema watendaji hao wanapaswa kutambua kuwa
serikali ipo na wenyewe wapo na kwamba, wanajua kukasirika na kuwajibisha
wazembe.
Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa na
watapangiwa kazi zingine kulingana na taaluma zao wakati uchunguzi zaidi
ukiendelea ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mkuranga, Benjamin
Majoya.
Wengine ni Abdalla Ngodu (Kaliua), Masalu Mayaya
(Kasulu), Goody Pamba (Serengeti), Julius Madiga (Sengerema) na Simon Mayeye
(Bunda).
Waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni
wakurugenzi watendaji watano ambao ni Felix Mabula (Hanang’), Fortunatus Fwema
(Mbulu), Isabella Chilumba (Ulanga), Pendo Malabeja (Kwimba) na Wiliam Shimwela
(Sumbawanga Manispaa).
Alisema Wakurugenzi wengine watatu wanapewa onyo kali
na watakuwa chini ya uangalizi ili kubaini kama wana udhaifu mwingine ili
wachukuliwe hatua zaidi ni Mohamed Maje (Rombo), Hamis Yuna (Busega) na Jovin
Jungu (Muheza.
Hawa alisema wakurugenzi wengine watatu walipewa onyo
na kutakiwa kuongeza umakini wanapotekeleza majuku yao ni pamoja na Isaya
Mngulumu (Ilala), Melchizedeck Humbe (Hai) na Wallace Karia (Mvomero).
Hata hivyo, alisema licha ya kuwepo kwa dosari ndogo
ndogo uchaguzi wa serikali za mitaa umekwenda vizuri.
Halmashauri 21 kati ya 165 ndio uchaguzi wake
ulikumbwa na dosari kwenye baadhi ya maeneo yake ikiwemo kuzuka kwa vurugu.
Tayari Rais Kikwete alisema ameliagiza jeshi la
polisi kuhakikisha inakamata na kuwachukulia hatua wote waliohusika na vurugu
hizo.
Alisema bila polisi kuchukua hatua kali, tabia na
vitendo hivyo vinaweza kugeuka na kuwa mambo ya kawaida kwenye uchaguzi.
Dar
yampa Krismas JK
Mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik,
amesema kukamilika kwa ujenzi wa maabara kwenye sekondari zake, ni zawadi ya
mwaka mpya kwa Rais Jakaya Kikwete.
“Ujenzi wa maabara umekamilika kwa shule zote 281 za serikali hapa Dar es Salaam, ambazo zilitakiwa kujengwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo lako (JK),” alisema.
Alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Rais
Kikwete kwa kutoa agizo hilo kwani, walikuwa wamelala lakini waliamka na
kufanya kazi usiku na mchana.
Alisema zawadi nyingine kwa Rais Kikwete ni ushindi
wa CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kwa mkoa wa Dar es Salaam, CCM kimepata ushindi wa
asilimia 75 na wapinzani kugawana zilizosalia.
Monday, 22 December 2014
LIVERPOOL, ARSENAL ILIKUWA SHUGHULI PEVU
04:57
No comments
![]() |
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck, akiruka juu kumpongeza, Olivier Giroud, aliyefunga bao na Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) katika mchezo dhidi ya Liverpool. |
![]() |
BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel, akipata huduma ya kwanza baada ya kugongana na Olivier Giroud wa Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England. |
![]() |
MCHEZAJI wa Liverpool, Philippe Coutinho, 'akikontroo' mpira mbele ya kiungo wa Arsenal, Oxlade-Chamberlain katika mchezo wa Ligi Kuu England. |
![]() |
PHILIPPE Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake wa Liverpool, baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Arsenal. |
![]() |
BEKI wa Arsenal, Mathieu Debuchy (kushoto), akifurahia bao alilofunga dhidi ya Liverpool. |
Kinana: Serikali imejizatiti kuongeza ajira
04:48
No comments
NA SHAABAN MDOE, LONGIDO
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amesema
serikali ya Rais Jakaya Kikwete imejipanga kuhakikisha inaongeza ajira na
kudhibiti watumishi.
Amesema kurejeshwa kwa mamlaka za ajira ndogo ndogo
katika ngazi za halmashauri kutasaidia kuongeza ajira kwa jamii.
![]() |
Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu CCM |
Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye semina
ya siku mbili kuhusu ardhi kwa viongozi wa mila wa Kimasai katika Mji wa
Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.
Kinana yuko mkoani hapa akiendelea kuzungumza na
wananchi na viongozi wa kimila kuhusiana na migogoro ya ardhi.
Akijibu swali la kiongozi wa kimila Tina Timani,
alihoji kuwa pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro kuwa katika makazi ya watu wa
kabila la Wamasai, bado nafasi za ajira kwa watu hao zimekuwa chache.
Alimuomba Kinana kuhakikisha kuwa mbali na ajira, pia
asilimia 50 ya mapato yote ya hifadhi hiyo yanarejeshwa kwa jamii kama faida
kwa kuwa ndio walinzi hifadhi hiyo na wanyama waliomo ndani.
Kufuatia kilio hicho ndipo, Kinana alipotolea
ufafanuzi suala hilo la ajira ambalo hapo awali hata watumishi wa kada ya chini
ya serikali wakiwemo maafisa watendaji wa kata, vijiji na udereva zilikua
zikitolewa na tume ya ajira taifa jambo ambalo lilikua likiwanyima fursa wakazi
wa eneo husika wenye vigezo.
Pia, alitolea mfano wa nafasi za udereva katika
halmashauri mbalimbali nchini ambapo mtumishi huyo utakuta anaajiriwa kutoka
mikoa na wilaya za mbali huku wale wenye sifa zinazohitajika kutoka halmashauri
husika wakiachwa.
Alisema kwasasa ajira hizo zitakua zikitolewa kwa
watu wa eneo husika wenye vigezo na italazimika kwenda kwa watu wa mbali
watakaopelekwa katika maeneo hayo iwapo tu hakutakua na mtu mwenye sifa
zinazohitajika.
“Napongeza uamuzi huo ile ya zamani hapana hata mtendaji wa kata au dereva anatolewa wilaya za mbali Tunduru au Newala huko analetwa hapa Longido wakati wapo wenye vigezo vinavyohitajika hii nasema hapana tuombe utekelezaji wa maagizo hayo uanze mara moja,” alisema Kinana.
Alisema kigezo anachokifahamu kilichokua kikitumika
kuwapata watumishi hao kutoka maeneo
mbalimbali ilikua ni kulinda utaifa zaidi lakini
alishauri kigezo hicho kibaki kwa watumishi wa ngazi za juu kuanzia makatibu
tawala wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na wengine lakini
siyo kwa wale wa kada za chini za uongozi.
Alieleza kuwa kuajiriwa kwa watumishi hao kutoka
maeneo wanayoishi kutasaidia mambo mengi ikiwemo gharama za malazi,likizo na
hata kuwezesha halmashauri husika kumuwajibisha pindi atakapokua hatimizi
majukumu yake ipasavyo.
“Sasa utakuta mtendaji anatoka huko Newala au Tunduma halafu unao kama kumi na mbili hivi je serikali itakua na uwezo wa kuwasafirisha kwenda likizo kila mwaka wao na familia zao hapana ila hii itasaidia,” alisema Kinana.
Kuhusu masuala ya ajira katika hifadhi ya Ngorongoro
na hifadhi nyingine aliahidi kulifikisha jambo hilo kwa viongozi wakuu wa
serikali ili liweze kufanyiwa kazi na kamwe hapendi kuona jambo moja
likizungumzwa zaidi ya mara tatu huku likikosa majibu yake.