Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Thursday 29 May 2014

Wakazi Kigamboni kulipwa mamilioni



  •  Thamani ya ekari moja ni milioni 141/-
  •  Ni fidia ya kupisha ujenzi wa mji mpya

NA TUMAINI MSOWOYA, DODOMA
WAKAZI wa Kigamboni, Dar es Salaam, ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mji mpya, watalipwa fidia ya shilingi milioni 141.6 kwa ekari moja.
Malipo hayo ni sawa na  sh. 35,000 kwa mita moja ya mraba.
Malipo hayo yalitangazwa juzi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alipokuwa akiwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

"Hiki ni kiwango cha fidia kwa mujibu wa sheria kulingana na thamani ya ardhi iliyopo katika mji huo wa Kigamboni,îalisema Profesa Tibaijuka.
Aliwataka wakazi wa Kigamboni, wasikubali kuuza maeneo yao kwa bei poa kutokana na kuibuka kwa kundi la wajanja linalowarubuni kufanya hivyo.
Waziri Tibaijuka alisema wajanja hao wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kununua maeneo yao ili baadaye walipwe fidia na Wakala wa Kuendelea Mji wa Kigamboni (KDA).
Alisema serikali imeandaa mpango kabambe wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni kwa kasi katika mwaka huu wa fedha,ikiwemo kufanya tathmini ya mali na kulipa fidia wananchi ili kupisha ujenzi wa mradi huo.
Aliwaonya wale wanaowarubuni wananchi na kununua ardhi yao, kuacha mara moja kufanya hivyo na kuwataka wanaodhani kazi hiyo imeshindikana, kubadili mtizamo wao.
Alisema katika mwaka wa fedha uliopita, wizara yake haikuweza kutekeleza mpango wake wa kuendeleza mji wa Kigamboni, kutokana na ukosefu wa fedha.
"Ninawahimiza wananchi wa Kigamboni kuendelea kuwa wavumilivu na kutokubali kurubuniwa kuuza maeneo yenu kwa wajanja, ambao baada ya viwango vya fidia kutajwa, wamejitokeza wakitaka kununua ardhi zenu kwa bei poa,îalisema
Aliwataka wananchi wa mji huo, kuitambua KDA na kutokubali kudanganywa na wale wanaotaka kupima maeneo ya mji wao bila fidia stahiki kulipwa.
Alisema wananchi wa Kigamboni wataendelea kubaki Kigamboni katika makazi mapya yatakayojengwa katika eneo la Uvumba, kata ya Kibada.
Profesa Tibaijuka alisema wananchi hao watawezeshwa kutumia sehemu isiyopungua asilimia kumi, kununua hisa za KDA kwa lengo la kuendelea kufaidi matunda ya mji mpya wa Kigamboni.
Alisema Machi, mwaka huu, mtaalamu aliteuliwa na ameshaanza kazi yake, jambo ambalo litaongeza kasi ya kuchochea ujenzi wa mji huo mpya. Alisema 
watapima maeneo ya miundombinu, umma na kusimamia utekelezaji wa mpango kabambe kupitia KDA.
Aliwataka wananchi wa Kigamboni kuendelea kuwa na imani na mpango huo kwa kwa kuwa hatua iliyofikiwa mpaka sasa ni nzuri.
Aliwaondoa wasi wasi wale wanaodhani kuwa kazi hiyo imeshindikana kwa madai kuwa mradi huo unatekelezwa kutokana na maagizo ya Ilani ya CCM ya mwaka 2010.
Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, 
imeishauri wizara hiyo kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo.
Akisoma taarifa ya kamati hiyo, Ester Bulaya alisema utekelezaji wa mradi huo umechukua muda mrefu tangu mwaka 2008, kiasi cha kuwakatisha tamaa wananchi.
Aliishauri wizara hiyo kuanza mara moja utekelezaji wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni kwa kujenga miundombinu huku maeneo mengine yakiachwa kwa ajili ya wawekezaji.

Hakimu, karani kortini kwa rushwa ya 50,000/-


NA SYLVIA SEBASTIAN
HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo Buguruni, Dar es Salaam, Grace Kivelege na karani wake, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Ilala, kujibu mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa ya sh. 50,000.
Hakimu Grace na Karani Rose Kuhima, walifikishwa mahakamani hapo jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Wakili wa TAKUKURU, Devota Mihayo, aliwasomea washitakiwa hao mashitaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassani.
Devota alidai washitakiwa hao walitenda makosa hayo Mei 7, mwaka huu, katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni,  wilayani Ilala.
Katika shitaka la kwanza linalomkabili Hakimu Grace, anadaiwa Mei 5, mwaka huu, mahakamani hapo, akiwa mwajiriwa, alimshawishi Clementina Guruma, kumpatia sh. 50,000, kama kichocheo cha kutoa rushwa ili aweze kumsaidia kesi iliyokuwa mbele yake.
Shitaka la pili, Hakimu Grace na karani wake, wanadaiwa Mei 7, mwaka huu, katika mahakama hiyo, walipokea rushwa hiyo kutoka kwa Clementina.
Washitakiwa walikana mashitaka hayo, ambapo Devota alidai upelelezi umekamilika na kuomba tarehe ya usikilizwaji wa awali. Pia Devota alidai hana pingamizi juu ya dhamana kwa washitakiwa.
Washitakiwa hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili waaminifu, watakaotia saini bondi ya sh. milioni mbili. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 11, mwaka huu, kwa usikilizwaji wa awali.
Wakati huo huo, Ally Yahya (24), alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, kujibu shitaka la wizi wa vifaa vya gari vyenye thamani ya sh. 100,000.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi, Matrona Luanda, Karani Blanka Shao, alidai Juni 23, mwaka huu, saa mbili asubuhi, maeneo ya Faya, mshitakiwa aliiba futo mbili za gari zenye namba ya usajiri T. 701CVF Toyota Rauni zenye thamani ya sh. 100,000, mali ya Vicent Mnyanyika.
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na alirudishwa rumande hadi Juni 10,mwaka huu kutokana na kutotimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Matrona aliyataja masharti hayo kuwa ni wadhamini wawili watakaotia saini bondi ya sh. 200,000.     

Mengi akana tuhuma alizozushiwa


NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP Limited, Dk. Reginald Mengi, amesema kuwa tuhuma mbalimbali zilizosambazwa kupitia ujumbe mfupi wa simu na mitandao ya kijamii juu yake ni za uongo, chuki na uzushi.
Dk. Mengi aliyasema hayo jana kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma, kwa maelezo kwamba hivi karibuni ameshuhudia kusambazwa kwa taarifa kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms) na mitandao ya kijamii zikimhusisha na tuhuma mbalimbali.
"Napenda kuufahamisha umma kwamba taarifa zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za uongo, chuki na uzushi. 
ìKilichonisikitisha sana ni kuona kuwa uzushi huo unachochea kuifarakanisha jamii yetu kwa misingi ya ukabila, ambalo ni hatari kwa umoja na mshikamano, ambao Tanzania tumejitahidi sana kuujenga na mtu yeyote anayediriki kuleta uchochezi wa kikabila, hastahili kuwa kiongozi wa ngazi yoyote katika taifa letu,î alisema.
Dk. Mengi aliongeza kuwa, amekuwa ni miongoni mwa Watanzania walio mstari wa mbele wanaomuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kusisitiza kuwa rasilimali za asili zilizopo nchini ni mali ya Watanzania, na ni lazima wawe wamiliki wakuu wa rasilimali hizo na gesi asilia.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni, dhana ya Watanzania kuwezeshwa na kumiliki uchumi wa nchi yao, imetambuliwa na serikali na Chama tawala.
Mwenyekiti Mtendaji huyo wa IPP,  alisema amekuwa akiishawishi serikali kutekeleza sera na sheria ya uwekezaji ili kuwashirikisha Watanzania kikamilifu katika uchumi wa taifa na kwa sasa katika uchumi wa gesi asilia ili kudumisha amani na utulivu nchini.

'Mbwa mwitu' 10 watiwa mbaroni


NA MUSSA YUSUPH
JESHI la Polisi  Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeendelea kupambana na kundi la wahalifu, maarufu kwa jina la 'mbwa mwitu',  ambapo idadi ya waliokamatwa imefikia 165 baada ya wengine kumi kukamatwa jana.
Pia limesema litaweka hadharani majina ya watuhumiwa wote waliokamatwa baada ya kukamilisha operesheni hiyo ya kuwasaka mbwa mwitu.
Watu hao walikamatwa juzi jioni katika maeneo ya Kigogo, ikiwa ni mwendelezo wa harakati za jeshi hilo katika kulisambaratisha kundi hilo.
Akizungumza na Uhuru jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleimani Kova alisema vijana hao ni miongoni mwa watuhumiwa wanaojihusisha na vitendo vya uporaji na ukabaji chini ya kundi hilo.
Kamishna  Kova alisema baada ya mahojiano kukamilika, majina yao yatawekwa hadharani pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu makosa yao.
Wakati huo huo, wakazi wa maeneo ya Kigogo wamelipongeza jeshi hilo kwa kulidhibiti kundi hilo kwenye makazi yao.
Walisema sasa wanaweza kufanya shughuli zao bila  bugudha kutoka kwa kundi hilo na kutaka kuongezwa kwa msako dhidi yao.
"Kukamatwa kwa Athumani Saidi, ambaye ni kiongozi wa kundi hilo kwenye maeneo yetu ni jambo zuri kwani alikuwa akitusumbua kila kukicha" alisema Shahibu Mkumbo mkazi wa eneo hilo.
Pia aliliomba jeshi hilo kufanya doria za mara kwa mara katika uwanja ujulikanao kama 'Chaukucha', ulioko maeneo hayo, hasa nyakati za usiku kutokana na baadhi ya vijana wa kundi hilo kuendesha vitendo vya ukabaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Wednesday 28 May 2014

Wabunge nusura wazichape kavukavu



  •  Ni Keissy wa CCM na Sanya wa CUF
  •  Hoja walizozitoa bungeni zazusha balaa

NA ABDALLAH MWERI, DODOMA
MBUNGE wa Nkasi (CCM), Ally Keissy na mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Mohammed  Sanya, jana  nusura wazichape kavukavu katika viwanja vya Bunge mjini hapa.
Ally Keissy (MB), Nkasi

Chanzo cha wabunge hao kutaka kuzitwanga ni mzozo ulitokea baada ya Keisy  kuwashukia wabunge wa CUF, akidai kwamba wamekuwa wakitoa malalamiko ya kuonewa bila sababu za msingi.
Keissy alisema hayo wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo alisema wamekuwa wakilalamika kwamba wanaonewa huku wakiendelea kunufaika na huduma za maji na umeme bila kuchangia chochote kwenye Muungano.
Kauli yake hiyo ilisababisha kuzuka kwa mzozo mkali nje ya ukumbi wa bunge, ambapo Keissy  aliendelea kurushiana maneno makali na Sanya, ambaye alikuwa akijibizana naye kwa hasira kiasi cha kutaka kupigana.
Mzozo huo ulivuta idadi kubwa ya wabunge kutoka vyama mbalimbali, wakiwemo wa CCM, ambao waliingilia kati na kuokoa jahazi kwa kuwatenganisha wabunge hao. Keissy aliondoka katika eneo hilo huku akirusha makombora kwa kambi ya upinzani.
Licha ya kuondolewa katika eneo la tukio, Keissy aliendelea kupiga vijembe akidai kila kukicha wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamika suala la kuonewa bungeni.
“Mmezidi bwana, kuchangia hamchangii, kazi yenu kulalamika tu,” alisema Keissy huku akiondoka katika eneo hilo kwa hasira baada ya kuamuliwa na baadhi ya wabunge.
Akijibu makombora ya mpinzani wake, Sanya, alimtaka Keissy kufunga mdomo, akidai siku zote amekuwa mpinzani katika ustawi wa maendeleo ya Zanzibar.
“Kwenda zako, huna maana wewe, kila siku umekuwa mpinzani wa Zanzibar, tutaonana jioni (ndani bunge),” alisema Sanya na kuungwa mkono na wabunge wenzake wa CUF.
Tukio hilo lilitokea saa 7:03 mchana, nje ya ukumbi wa bunge, mbele ya idadi kubwa ya wabunge, baada ya Naibu Spika, Job Ndugai, kuahirisha shughuli za bunge hadi saa 10: 00 jioni. Tafrani hiyo ilidumu kwa takribani dakika 10.
Kituko hicho kilikuwa kama filamu kwa kuwa kilivuta idadi kubwa ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa bunge, ambao walikuwa wamepigwa na butwaa kuhusu tukio hilo.
Tukio hilo liliwagawa wabunge waliolishuhudia kwa kuwa baadhi walisema Keissy alikuwa na hoja ya msingi kwa madai kuwa  wapinzani, hususani wabunge wa CUF, wamekuwa wakipinga Muungano na wengine walimtetea Sanya.
Awali, Kombo Khamisi Kombo (Mgogoni-CUF),  alisema Zanzibar imekuwa ikibaguliwa katika suala la balozi na wafanyakazi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Kombo alidai kati ya mabalozi 35 wa Tanzania, Zanzibar imetoa mabalozi wanne, hatua aliyodai ni upendeleo. Pia alisema wafanyakazi wengi wanaofanya kazi katika balozi za nje ya nchi, wanatoka Tanzania Bara.
Kwa upande wake, Keissy baada ya kupata fursa ya kuchangia, alisema Zanzibar ina wananchi wachache, ikilinganishwa na Tanzania Bara na kwamba imekuwa haichangii katika wizara hiyo kwa zaidi ya miaka 20.

Libya hakukaliki-Membe


NA TUMAINI MSOWOYA, DODOMA
SERIKALI imewashauri Watanzania kusitisha safari zao za kwenda nchini Libya, mpaka hapo watakapotangaziwa vinginevyo, kutokana na kuwepo kwa hali tete ya kiusalama nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema hayo bungeni mjini Dodoma jana, alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha.
Bernard C. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa K'taifa

Membe alisema Watanzania hawapaswi kwenda Libya kwa sasa, kutokana na hali ya kiusalama ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kushika kasi kwa mauaji ya raia.
Alisema tangu kuuawa kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi,  miaka mitatu iliyopita, pamoja na Balozi wa Marekani nchini Libya,  mauaji ya wenyeji na raia yamekuwa yakiongezeka kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Membe alisema hali ya nchi hiyo imekuwa mbaya zaidi kiasi cha kusababisha waziri mkuu wa nchi hiyo kutekwa nyara na baadaee kuachiliwa na bunge kuvamiwa na kuchomwa moto.
Alisema hali hiyo imezifanya ofisi nyingi za balozi kufungwa kutokana na mauaji hayo na kuifanya Libya isitawalike.
ìTunawashauri Watanzania wasiende Libya kwa sasa kutokana na hali iliyopo mpaka pale serikali itakaposhauri vinginevyo,îalisema Membe.
Kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi, Membe alisema msimamo wa Tanzania ni kwamba mpaka kati yake na nchi hiyo upo katikati ya Ziwa Nyasa.
Alisema mazungumzo ya usuluhishi wa mgogoro huo yanaendelea na kwamba, serikali inaandaa hoja nzito na zenye ushawishi kuhusu mpaka huo.
Waziri Membe alisema kinachosubiriwa kwa sasa ni kikao, ambacho kitaitishwa na jopo la usuluhishi ili kuendelea na usuluhishi kutokana na mchakato wa uchaguzi na kuundwa kwa serikali mpya ya Malawi.
Kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi, Membe aliwataka Watanzania kuendelea kulinda amani na utulivu kwa kutokubali kusuluhisha baadhi ya mambo kwa njia za kigaidi.
Alisema vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kikundi cha Boko Haram nchini Nigeria na Al-shaababu nchini Kenya, havivumiliki na kwamba serikali imeshatuma salamu za pole na utayari wake katika kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.
Kuhusu  Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alisema Tanzania imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kulinda amani, usalama na demokrasia kwenye nchi za kusini mwa afrika, ikiwemo DRC.
Alisema kutokana na msimamo huo, Tanzania imechangia kikosi kimoja cha askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),  kwenye FBI, iliyoko chini ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (UN) cha kulinda amani.
Waziri alisema kikosi hicho kimesaidia kukisambaratisha kikundi cha waasi wa M23, ambao wamekuwa wakivuruga amani kwa muda mrefu Mashariki ya DRC.

CHADEMA ‘inatumika’ na Rwanda - Membe


NA ABDALLAH MWERI
SERIKALI imesema itachukua hatua kali kwa baadhi ya Watanzania, ambao watabainika kutoa siri za nchi kwa ajili ya manufaa binafsi.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alipokuwa akijibu hotuba ya Kambi ya Upinzini iliyosomwa na Mbunge Ezekiel Wenje (Nyamagana-CHADEMA).
Katika hotuba yake, Wenje ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alidai kuwa Membe, anachochea vita kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Membe alisema ni aibu kwa mbunge kusimama ndani ya bunge kutetea maslahi ya Rwanda na kuonya kuwa hatua hiyo ni hatari kwa mustakabali wa nchi.
Alisema ameshangazwa na kauli ya Wenje kwamba Serikali ya Tanzania inaibeba DRC katika vita kati ya nchi hiyo na Rwanda.
Akionekana kukerwa na kauli ya Wenje, Membe alisema mbunge huyo hana nia njema na mustakabali wa wananchi wa Tanzania na lengo lake ni kutaka kuchochea mgogoro kati ya Tanzania na Rwanda.
“Ni aibu kwa Mbunge Wenje kusimama bungeni macho yamemtoka, akiitetea Rwanda. Mtu wa aina hii ni msaliti mkubwa na hafai kuwa kiongozi
“Kwa nini Wenje anatetea nchi jirani? Mtu makini ni lazima apiganie nchi yake hata kama serikali yake inafanya mabaya au mazuri. Mtu wa aina hii ni rahisi kutumika au kutoa siri za nchi,” alisema Membe.
Membe alisema haamini kama kauli ya Wenje ni azimio la chama chake cha CHADEMA na alishangaa kwa nini Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameruhusu hotuba hiyo kusomwa bungeni.
“Mheshimiwa Mbowe ulikuwa wapi mchana wakati kauli za namna hii zilizojaa uchochezi zinasemwa na mbunge wako. Hii ni aibu na nimesikitika sana, naomba Watanzania wafahamu kwamba askari wa M23 ni Wanyarwanda,” alihoji Membe.
Katika kauli yake, Wenje alitetea akidai kuwa askari wa kundi la M23 walioko DRC si raia wa Rwanda, kauli ambayo ilimshitua Waziri Membe.
Waziri huyo alisema yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri, ikiwa itathibitika kuwa askari wa 23 si raia kutoka Rwanda.
Pia alimtaka Wenje athibitishe kauli yake kwamba askari hao si raia wa Rwanda na akishindwa, achukuwe hatua ya kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.
Mbowe alikiri baadaye kuwa, hotuba iliyotolewa na Wenje ni ya kambi rasmi ya upinzani.

Wanafunzi bora wapewa fedha badala ya vocha


NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetoa ufafanuzi kuhusu zawadi zilizotolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na sekondari, mwaka jana.
Imesema wanafunzi 10 wa kidato cha nne walipewa vocha za thamani ya sh. 500,000 kwa ajili ya kununua vitabu vya kiada na ziada.
Shukuru Kawambwa - Waziri (MoEVT)

Taarifa hiyo ilisema wizara imeamua kuwakabidhi wanafunzi 10 wa kidato cha nne fedha taslimu sh. 500,000 badala ya vocha, ili wanunue vitabu wao wenyewe.
“Hii ni kwa sababu wanafunzi hawa wanaweza kujiunga na kidato cha tano katika tahasusi mbalimbali na ni vyema wakanunua vitabu kulingana na tahasusi zao,”alisema.
Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome, ilisema katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu, kilichofanyika Mei 10, mwaka huu, mkoani Dodoma, tuzo mbalimbali zilitolewa, zikiwemo za fedha kwa makundi tofauti.
Ilisema tuzo ya fedha taslimu ilitolewa kwa wanafunzi 30, waliofanya vizuri katika mtihani wa mwaka jana, ambapo wanafunzi watano bora, waliofanya vizuri katika mtihani wa elimu ya msingi, walipata sh. 120,000.
Profesa Mchome alisema wanafunzi watano bora wasichana na wanafunzi bora wavulana waliofanya vizuri mtihani wa kumaliza kidato cha nne, walipata sh.250,000.
Sifuni Mchome - Katibu Mkuu (MoEVT)

Alisema pia kuwa, wanafunzi watano bora wasichana na watano bora wavulana waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya sekondari kitado cha sita, walipata sh. 500,000.
Kwa mujibu wa Profesa Mchome, fedha zngine zilizotolewa, zilikuwa ni hundi ya sh. milioni tatu  kwa walimu wa shule 60 zilizoongoza ufaulu katika mtihani wa mwaka jana.

Saba mbaroni kwa mauaji ya askari


Na Moses Mabula, Tabora
POLISI mkoani Tabora, imewatia mbaroni watu saba wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya askari polisi wawili kwa kuwapiga risasi.
Tukio hilo la uhalifu, lilitokea hivi karibuni katika kijiji cha Usoke wilayani Urambo mkoani Tabora.
Watuhumiwa hao walikiri kuhusika na mauaji hayo, pamoja na matukio mengine ya uhalifu na unyang`anyi wa kutumia silaha, likiwemo tukio la Aprili 28, mwaka huu, ambapo askari hao walipoteza maisha.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Silvester Mussa, maarufu kwa jina la Kindwendu(31), mkazi wa Mkuyuni Tambukareli, Mwanza, Sadiki Hamisi, maarufu kwa jina la White, mkazi wa mtaa wa Mihogoni mjini Tabora na Abeli Benedict, mkazi wa Muungano, Urambo.
Wengine ni Fransic  Masanja (38), mkazi wa Nansio, Ukerewe mkoani Mwanza, Haji Athumani (50), mkazi wa Usoke, Urambo, Mussa Khatibu (49) na Ramadhani Kassimu  maarufu kwa jina la Rama Manywele, wakazi wa Tabora.
Susan alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na bastola na risasi tano. Alisema walipohojiwa, walikiri kuitumia bastola hiyo katika matukio ya uhalifu.
Kamanda huyo alisema baada ya kuwahoji, watuhumiwa hao walikiri kuhusika na  matukio ya uhalifu wa kutumia silaha, likiwemo tukio hilo la kuuawa kwa askari namba  F.5179 PC, Jumanne na namba G. 3388, PC Shabani.
Askari hao wa kituo cha polisi cha Usoke, waliuawa katika majibizino ya risasi katika tukio la uporaji  katika nyumba ya mmoja wa wafanyabiashara wa kijiji hicho mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mbali na watuhumiwa hao , alisema wamemtia nguvuni mtuhumiwa mmoja, akimiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia katika vitendo mbalimbali vya uhalifu.
Wakati huo huo, watu 17 wamekamatwa na polisi katika wilaya za Kaliua, Igunga, Nzega na Manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kupatikana na gunia sita na kete 402 za bhangi na lita 110 za pombe haramu aina ya Gongo.
Kamanda Suzan alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi wa polisi kukamilika.

Profesa Tibaijuka akabidhi hatimiliki za kimila Mvomero


NA REHEMA ISANGO
SERIKALI imeanza kwa vitendo kutatua migogoro ya kudumu ya ardhi na upimaji wa kila kipande, baada ya kutoa hatimiliki za kimila katika kijiji cha Lekenge, wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Utatuzi huo ulianza juzi baada ya  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kukabidhi hati hizo kwa wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hati hizo, Profesa Tibaijuka alisema hatimiliki za kimila zina faida kubwa, ambapo mbali ya kutatua migogoro, zinasaidia katika kupata mikopo kwenye taasisi za fedha.
Akizungumzia ufugaji, alisema kufuga ni haki na kazi  na ni ruksa kwa kila mtu kufanya hivyo, lakini kinachotakiwa ni kufuga kwa kufuata utaratibu, ikiwemo kufuata ufugaji wa kisasa.
Alisema  migogoro inayoibuka mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima, kwa kiasi kikubwa inatokana na aina ya ufugaji, ambapo wafugaji wengi wanaendelea kutumia mbinu za kizamani za ufugaji wa kuhamahama.
Profesa Tibaijuka alisema katika siku zijazo, wafugaji watatengewa maeneo kwa kila mfugaji, hivyo wanapaswa kujiandaa kujiunga kwenye vikundi vya ushirika ili waweze kwenda na wakati.
Alisema kwa sasa serikali inafanya jitihada za kuwatafutia wafugaji maeneo kwenye ranchi za taifa na mapori ya akiba, ambayo yatawekewa uzio ili  mifugo isitoke na kwenda kwenye mashamba ya wakulima.
Kuhusu hatimiliki za kimila, Profesa Tibaijuka aliwaasa waliopimiwa mashamba kuwa,   wanapaswa kujenga barabara ili maeneo yao yaweze kufikika na wahusika waweke mipaka kwa kupanda miti ya kijadi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Selassie Mayunga, aliwaahidi wananchi hao kutekeleza ahadi yake ya kuwachimbia kisima kimoja.
Alisema kutokana na kukamilika kwa upimaji huo wa ardhi,  migogoro ya wakulima na wafugaji itamalizika kwa kila jamii kugawiwa ardhi na kila kipande cha ardhi kuwa na matumizi yaliyoainishwa kwenye ramani ya kijiji.
Katika  risala yao, wananchi wa Lukenge walisema wamepokea mpango huo kwa furaha kubwa kwa kuwa utasaidia kumaliza migogoro ya ardhi, iliyokuwa ikijitokeza mara kwa mara.
Katika mgogoro wa wakulima na wafugaji mwaka jana, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, walikimbia nyumba zao na kwenda kupata hifadhi kwenye Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa.

Mjamzito ajiua kwa sumu ya panya


Na  Latifa Ganzel, Morogoro
MAMA mjamzito aliyekuwa na mimba ya miezi tisa, Anjela Domiano (42), mkazi wa Nanenane katika Manispaa ya Morogoro, amefariki baada ya kunywa sumu ya panya.
Tukio hilo lilitokea juzi, saa 2.30 asubuhi, katika eneo la Kichangani katika Manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, alisema jana kuwa, marehemu
Angela alifia katika hospitali ya mkoa, ambako alipelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Alisema siku ya tukio, Angela alikutwa akiwa ameanguka huku akitapatapa katika eneo la Kichangani.
Alisema polisi walipata taarifa na kufika katika eneo la tukio na kumchukua mama huyo na kumfikisha katika hospitali hiyo, ambapo alifariki wakati akipatiwa matibabu.
“Wasamaria wema walipomwona mama huyo kaanguka chini, walitoa taarifa polisi na walipofika eneo la tukio, walimkuta akiwa anatapatapa na kuamua kumkimbiza hospitali ili kuokoa maisha yake,” alisema.
Alisema Angela alikutwa na sumu ya panya katika pochi yake na uchunguzi  wa awali umeonyesha kuwa, alifariki kutokana na kunywa sumu hiyo.
Kamanda huyo alisema hawakuweza kumhoji Anjela kutokana na hali yake kuwa mbaya  na wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Dovutwa alazwa Aga Khan


NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba na Mwenyekiti Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kifua.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UPDP, Felix Makuwa jana ilisema kuwa,
Dovutwa alilazwa juzi hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kifua kwa siku kadhaa.
“Alianza kusumbuliwa na kifua tangu wiki iliyopita. Tatizo hilo limekuwa likimsababishia pumzi kuziba,îalisema.
Makuwa alisema awali, Dovutwa alikwenda katika Hospitali ya Sanitas Mikocheni, lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya, alihamishiwa Aga Khan.
Alisema bado hali ya kiongozi huyo si nzuri na kwamba, amehamishiwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU), ambako madaktari wanaendelea kumtibu.

Mtoto Nasra ahamishiwa Muhimbili


Na  Latifa Ganzel, Morogoro
MTOTO  Nasra Mvungi (4), aliyekuwa akiishi ndani ya boksi kwa miaka minne, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dk. Rita Lyamuya, alisema jana kuwa, Nasra amehamishiwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi na kupatiwa matibabu.
Dk. Rita alisema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri, lakini amehamishiwa Muhimbili ili kupata huduma za mifupa, ambazo hazipo katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
“Ilikuwa apelekwe Muhimbili Mei 27, lakini tuliamua kumpeleka mapema baada ya kuona hali yake inaendelea vizuri na pia baada ya kupata usafiri,” alisema.
Alisema wameshawasiliana na mama anayemlea mtoto huyo, ambaye aliwajulisha kwamba walifika Dar es Salaam salama na kwanza ameshaanza kupatiwa matibabu.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa mkoa wa Morogoro, Oswing Ngungamtitu, alisema licha ya mtoto huyo kuhamishiwa Muhimbili, bado ataendelea kuwa chini ya usimamizi wa ofisi yake.
Alisema kwa sasa, mtoto huyo amepatiwa mama mlezi, Josephin Joel, ambaye atakuwa akiishi naye kwa muda, akiwa hospitali kwa ajili ya kumpatia huduma zote muhimu.

Sunday 25 May 2014

Kinana: Utekelezaji Ilani umefanikiwa

NA Mohammed Mussa, Iramba.
  • Nape asema ‘Katiba ya Watanzania bila UKAWA inawezekana’

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wanachama na wananchi kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010-2015, chini ya Rais Jakaya Kikwete, unakwenda vizuri.

Amesema katika ziara zake za

kukagua utekelezaji wa ilani kwenye mikoa mbalimbali nchini, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba kazi iliyobakia ni ndogo.

Kinana alisema wanachama na wananchi wana kila sababu ya kujivunia kutokana na Chama, kutekeleza kwa vitendo ahadi ilizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake watahakikisha CCM, inazidi kujiimarisha ili iweze kuwatumikia Watanzania.

Kinana alisema hayo Wilaya ya Iramba Mashariki mkoani Singida, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya wilaya hiyo.

Alisema lengo la ziara zake ni kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, uhai wa Chama na maandalizi ya uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa.

Kinana alisema Chama chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kimefanya mambo mengi katika jamii na kwamba asilimia kubwa ya ahadi zake imezitekeleza.
 

Hakuna anayekamilisha kila kitu, lakini mambo mengi tuliyoahidi tumeyatekeleza na wananchi ni mashahidi,î alisema na kuwa ni lazima Chama, kizidi kujiimarisha na kujengwa upya ili kiweze kutatua matatizo ya wananchi," alisema.

Kinana alisema katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Chama kitaibuka na ushindi mkubwa.

Alisema CCM, ndio yenye jukumu la kuzunguka nchini na kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana baada ya uchaguzi hadi sasa kwa kuwa wapinzani wanataka viongozi wa Chama, wasizunguke ili wapate la kusema.

Alisema miradi mbalimbali imetekelezwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, umeme, shule, maabara, afya na mawasiliano.

Kuhusu mchakato wa katiba mpya, Kinana alisema baadhi ya viongozi wameugeuza mchakato huo kuwa mazingaombwe.

Alisema katiba wanayoitaka wapinzani ni ya kuwaweka madarakani na wala si ya kuleta maendeleo katika jamii.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, ametoboa siri ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kutoka ndani ya Bunge, kuwa wanafanya majaribio kwani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,wengi hawatarudi bungeni.

Amesema baadhi ya wajumbe hao ambao pia ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watakosa ubunge, hivyo wanafanya mazoezi ya kurejea uraiani.

Mwigulu alisema wabunge wengi ambao wamejiunga na UKAWA baada ya uchaguzi mkuu hawatakanyaga tena ndani ya Bunge na wataishia mapokezi au sehemu za kufikia wageni.

Kauli hiyo, aliitoa wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba Mashariki mkoani Singida.

Mwigulu ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, alisema UKAWA hawana sababu ya msingi ya kutoka bungeni.

Alisema baada ya UKAWA kushindwa kwa hoja, walifanya kila hila kutafuta sababu za kususia Bunge Maalumu la Katiba na kwamba sababu zao hazina msingi wowote.

Mwigulu alisema Bunge Maalumu la Katiba litakapoendelea tena Agosti, mwaka huu, watashauri posho zilipwe kila baada ya wiki moja.

Kwa upande wake, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema wasiotaka katiba mpya, ipo ya zamani ambayo itatumika.

Alisema vyama vya siasa vinaigiza ili vipate kula na kwamba katika kuigiza kwao, vinataka watu wote wawaamini.

Nape alisema CCM, ndio Chama pekee ambacho kikipanga mambo yake, kinamaanisha na kutekeleza.

Alisema CCM inazidi kuimarika na kukubalika katika jamii kwa sababu ndiyo kinacholeta maendeleo nchini na kuwa: Katiba ya Watanzania bila ya UKAWA inawezekani.”

Alisema kama UKAWA hawautaki mchakato wa katiba, waachwe waende barabarani.

Ajira mpya laki saba kuzalishwa

NA THEODOS MGOMBA,DODOMA
WIZARA  ya Kazi na Ajira inatarajia kuzalisha ajira 700,000 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Gaudentia Kabaka alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake.

Gaudentia alisema ajira hizo zitatokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayotekelezwa na taasisi za umma, programu ya kukuza ajira kwa vijana na hatua mbalimbali za uwekezaji.

Waziri alisema hadi kufikia Aprili mwaka huu, ajira 630,616 zilizalishwa katika mwaka wa fedha unaoishia mwezi ujao.

Alisema ajira hizo zilizalishwa katika sekta za kilimo (130,974), elimu ajira (36,073), ujenzi na miundombinu ajira (32,132) nishati na madini ajira 453,  afya ajira 11,221, TASAF ajira 8,686 na sekta nyingine serikalini ajira 2,321.

Sekta nyingine ni sekta binafsi ajira 211,970, viwanda vidogo na vya kati (SMEs) ajira 7,192, miradi ya uwekezaji kupitia maeneo huru ya uwekezaji -EPZ ajira 26,381, mawasiliano ajira 13,619 na miradi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania  (TIC) ajira 149,594.

Gaudentia alisema wizara kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaendelea na juhudi za kuwajengea vijana uwezo wa kuwawezesha kujiajiri wenyewe katika maeneo yao.

Alisema mafunzo ya ujasiriamali  yametolewa kwa vijana 11,500 kupitia Mradi wa Kazi Nje Nje katika mikoa 17 ya Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Waziri Gaudentia mafunzo hayo yalilenga katika kubadili fikra za vijana  kuwa ajira ni pamoja na kujiajiri, kuwajengea uwezo vijana katika kutambua fursa zilizopo, namna bora ya kuandaa miradi, kutafuta masoko na kutunza hesabu za biashara.

Alisema ili kukuza ajira na kazi za staha nchini, wizara itaratibu uingizaji wa masuala ya ukuzaji ajira katika mipango na programu za maendeleo za kisekta kwa kutoa mafunzo katika mikoa mitatu.

Pia, katika mwaka ujao wa fedha  pamoja na programu hizo,  wizara itafuatilia utekelezaji wa mwongozo wa namna ya kuhuisha ukuzaji ajira nchini.

Alisema wizara itaendelea kufanya utafiti wa hali ya nguvu kazi ambao utatoa picha ya hali ya ajira nchini.

Waziri Gaudentia alisema utafiti huo utatoa taarifa kuhusu ajira katika sekta rasmi na isiyo rasmi, hali ya utumikishwaji wa watoto na idadi ya ajira mpya zilizozalishwa katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2014.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha  serikali inatarajia kuzuia watoto 4,000 kuingia kwenye ajira mbaya na kuwaondoa watoto 10,000 wanaotumikishwa kwenye ajira mbaya.

Akichangia hutuba hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda alisema ni vyema serikali ikakamilisha mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Pensheni ya Wazee.

Alisema kuanzishwa kwa mfuko huo kutasaidia wazee waweze kuboreshewa hali zao za kimaisha.

Mtanda alisema kumekuwa na mitazamo mingi tofauti ikiwa ni pamoja na mtazamo kuwa wazee ambao hawakuchangia kuweka akiba katika mfumo rasmi hawawezi kulipwa pensheni.

Vinara wa ‘mbwa mwitu’ wanaswa

NA William Shechambo
BAADA ya kikundi cha vijana wahalifu cha mbwa mwitu au panya road kufanya vurugu kwenye maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Jeshi la Polisi Kanda Maalum limewakamata vijana sita ambao ni viongozi wa kundi hilo.

Vinara hao, Said Athuman (20), Joseph Mponela, Clement Peter (25) Roman Vitus (18), Mwinshehe Adam (37) na Daniel Peter (25) walikamatwa kutokana na msako mkali uliofanywa na jeshi hilo.

Katika mkutano wa dharura na waandishi wa habari uliofanyika jana ofisini kwake, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema msako uliofanywa umezingatia maeneo yaliyokuwa yakisumbuliwa na kikundi hicho ambayo ni Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala.

Kova alisema ili kuhakikisha kikundi hicho na vingine vyenye tabia ya kufanya uhalifu na kusababisha uvunjifu wa amani jijni Dar es Salaam, vinadhibitiwa, askari wa kutosha wamejipanga kwenye maeneo hayo kwa ajili ya doria.

“Nimepanga askari wa kutosha kwenye maeneo hayo kwa ajili ya doria ili kudhibiti mlipuko wowote wa vitendo vya kihuni vyenye ishara ya uhalifu vinavyoleta hofu kwa wananchi,” alisema Kova.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi limegundua mchezo unaofanywa na baadhi ya watu wa kutoa taarifa za uongo kwa umma kwa njia ya ujumbe wa simu za mkononi kuhusiana na kuvunjika kwa amani kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema tabia hiyo ni mbaya na polisi linatoa onyo kali kwa sababu inasababisha hofu kwa wananchi huku kukiwa hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani kwenye maeneo husika.

“Kwa tekinolojia tuliyonayo, tuna uwezo wa kumtambua mtu au kundi la watu wanaosambaza ujumbe wa uongo ili kuwapa watu presha. Wenye tabia hizo waache mara moja kabla hatujawatia nguvuni,” alionya Kova.

Alisema upelelezi wao umebaini kuwa habari za uvunjivu wa amani uliofanywa na mbwa mwitu ambazo zilizotolewa wiki iliyopita, zilivumishwa kutokana na watu kufikiri kuwa kikundi hicho kitajitokeza hadharani kulipiza kisasi baada ya wenzao wawili kuuawa na wananchi Mei, 18 na 20, mwaka huu.

Rais Zuma aapishwa

Na Joseph Damas, Pretoria
RAIS Jacob Zuma wa Afrika Kusini, amekula kiapo kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa pili wa miaka mitano huku akiahidi kuboresha utendaji wa serikali.

Pia, ameahidi kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa miongoni mwa baadhi ya watumishi wa umma.

Hafla ya kuapishwa kwa Rais Zuma ilifanyika jana kwenye Jengo la Union mjini hapa, imeandika historia nyingine kwa wananchi wa Afrika Kusini, ambapo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 20 ya Demokrasia na Uhuru tangu kuondolewa kwa utawala wa kibaguzi.

Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wageni 400 wakiwemo marais na wakuu wa serikali kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.

“Tutaendelea kuimarisha utendaji wa serikali na kupambana na rushwa katika utumishi wa umma ili kuendelea kuwahudumia wananchi wetu kwa kuwapa huduma zote muhimu. Tumefanya mambo mengi ya maendeleo katika kipindi kifupi, lakini bado tunapaswa kuendelea kuboresha zaidi,” alisema Zuma.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Union, Rais Zuma aliwapongeza wananchi kwa kumchagua kuongoza tena taifa hilo huku akiwahakikishia kuwa amelipokea jukumu hilo.

Amesema ushindi wake ni ishara kuwa wananchi wa Afrika Kusini wameendelea kukiamini Chama cha African National Congress (ANC).

Hata hivyo, alisema jukumu la kuongoza taifa hilo ni la wananchi wote bila kujali rangi na kwamba, umoja na mshikamano unahitajika ili kuendelea kulivusha taifa hilo.

Alisema jukumu kubwa lililombele yake kwa sasa ni kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kutengeneza nafasi za kutosha za ajira hususan kwa vijana.

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Rais Robert Mugabe (Zimbabwe), Salva Kiir (Sudan Kusini), Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicent, Goodluck Jonathan (Nigeria), Ian Khama (Botswana).

MAMBO YALIVYOKUWA


Wananchi wa Afrika Kusini walianza kuwasili viwanja vya Union saa 10 alfajiri, ambapo ulinzi katika eneo hilo uliimarishwa maradufu.

Walioruhusiwa kufika kwenye jengo la Union ni viongozi wa serikali, wakuu wa nchi na wageni wengine waliokaribia 4000.

Idadi kubwa ya wananchi ilikuwa imefurika kwenye viwanja hivyo mbali kidogo na jengo hilo na kila kilichokuwa kikiendelea waliona kupitia luninga kubwa zilizowekwa uwanja hapo.

Wasanii na wanamuziki maarufu karibu wote wa Afrika Kusini walikuwa wakitoa burudani kwa wananchi, ambapo baada ya wageni wote kufika na kuketi katika nafasi zao, Rais Zuma aliwasili tayari kwa kuapishwa.

Rais Zuma aliwasili eneo la tukio saa 11:00 akiwa ameongozana na mkewe Mantuli, ambapo umati ulilipuka kwa furaha huku nyimbo za kumsifu za kila aina zikisikika kutoka kila upande.

Jaji Mkuu wa Afrika Kusini, Mogoeng Mogoeng alimwapisha rasmi Zuma kuwa kiongozi wa taifa hilo na baadaye mizinga pamoja na ndege za kivita zilipamba anga ikiwa ni kutoa salamu za utii kwa kiongozi huyo.

Mara baada ya kuapa na kuhutubia taifa huku akitumia muda mfupi katika hotuba yake, Zuma alishuka chini na kwenda kupanda jukwaani mahali ambako wananchi walikuwa wamekusanyika.

Kwa mara nyingine tena, Zuma aliwaeleza wananchi dhamira yake ya kuhakikisha maendeleo zaidi yanapatikana ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji.

Rais Zuma anatarajiwa kutangaza Baraza la Mawaziri leo, ambapo ameahidi ni wachapakazi  na waadilifu ndio watapewa nafasi ya kuungana naye.

Viwanda vya kukamulia alizeti kujengwa Singida

NA MWANDISHI WETU, SINGIDA
SERIKALI mkoani Singida, imesema inatarajia kujenga viwanda vitano vya kukamulia mafuta ya alizeti.

Mkuu wa mkoa huo, Dk. Paraseko Kone alisema hayo juzi katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana inayoendelea mkoani Singida.

Alisema kati ya viwanda hivyo, vinne vitakuwa vya kati na kimoja kitakuwa kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ambacho kitajengwa mjini hapa.

Dk. Kone alisema lengo la ujenzi wa viwanda hivyo ni kuongeza thamani ya zao la alizeti na kupata soko la uhakika la zao hilo.

Alisema katika mwaka 2006/2007, tani 28 za alizeti zilizalishwa katika mkoa huo na kwamba msimu uliopita walizalisha tani 200,000.

Kwa upande wake, mmoja wa wamiliki wa kiwanda cha kukamulia mafuta ya alizeti, Yussuf Amiri, alisema wananchi wa mkoa huo wana mwamko mkubwa wa kulima zao la alizeti.

Kwa upande wake, Kinana alisema Mkoa wa Singida unaongoza kwa kujenga viwanda vidogo vya kukamulia mafuta ya alizeti.

Migogoro ya ardhi wakulima, wafugaji yawa moto bungeni

NA ABDALLAH MWERI
SAKATA la kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji nchini, jana ulizua mjadala mzito bungeni
wakati wabunge wakichangia majadiliano kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. Titus Kamani, juzi usiku aliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Sehemu kubwa ya majadiliano ya wizara hiyo yalihusisha zaidi mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji katika
maeneo mbalimbali nchini.

Wabunge hao walisema serikali ina wajibu wa kuchukua hatua haraka kwa lengo la kuepusha mapigano ya wakulima na wafugaji ambayo yamesababisha vifo.

Mbunge Benedict Ole Nangoro (Kiteto-CCM) alisema fedha zilizotengwa ya bajeti iliyotengwa katika wizara hiyo haina mashiko kwa kuwa waziri atashindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ni nyeti, hivyo ilitakiwa kupewa fedha za kutosha ambazo miongoni mwa kazi zake ni kuhakikisha zinatatua migogoro ya wakulima na wafugaji nchini.

Ole Nangoro alisema mbali na fedha ndogo kutengwa katika wizara hiyo, pia serikali inatakiwa kuunda chombo maalumu ambacho kitakuwa wakala wa kushughulikia matatizo ya wakulima na wafugaji.

“Serikali iunde chombo maalumu au wakala kama TANROADS ambacho kitakuwa na mamlaka ya kushughulikia matatizo yote ya wakulima na wafugaji,” alisema Ole Nangoro.

Naye Mahmoud Jumaa (Kibaha Vijiji-CCM), alisema migogoro ya ardhi itaepukwa endapo serikali itatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafugaji.

Pia, alisema ujenzi wa machinjio ya kisasa akitolea mfano katika jimbo lake la Kibaha Vijijini, utapunguza kwa kiasi kikubwa mapigano ya wakulima na wafugaji.

Alisema serikali inatakiwa kujenga machinjio ya kutosha katika maeneo mbalimbali nchihi hatua ambayo itachochea ufugaji wa kisasa ambapo wafugaji watapata fursa nzuri ya kufunga kitaalamu.

Kwa upande wake, Selemani Nchambi (Kishapu-CCM), alisema ili kuepusha mauaji, serikali ina wajibu wa kujibu kwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji kwa lengo la kuepusha mapigano.

“Bajeti ya mifugo ni ndogo ni jukumu la serikali kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji ili kuepusha mapigano dhidi ya wananchi katika maeneo mbalimbali kama Kiteto na Kishapu,” alisema Nchambi.

John Cheyo (Bariadi Magharibi-UDP), alisema serikali imechelewa kuchukua hatua kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, hivyo ameitaka kuchukua hatua haraka ili kukomesha mauaji.

Alisema wafugaji wamekuwa wakihama kutoka eneo moja hadi jingine kwa kuwa serikali imeshindwa kuwajengea uwezo wa kufuga katika mazingira bora.

Ridhiwani Kikwete (Chalinze-CCM), alisema elimu ya kutosha ndiyo njia pekee inayoweza kunusuru mapigano baina ya jamii hiyo.

Mbunge huyo aliitaka serikali kutenga maeneo tofauti ya wakulima na wafugaji sanjari na kujenga kwa wingi majosho na machinjio.

Muhammad Sanya (Mji Mkongwe -CUF) alisema Tanzania ina hazina kubwa ya mifugo na ikitumika vyema itakuwa na uwezo wa kupata fedha nyingi za kigeni.

Sanya alisema endapo wafugaji wataelimishwa kufuga kisasa, Tanzania itapata fedha kutoka Saudi Arabia, Omani, Comoro na nchi zingine zenye uhitaji mkubwa na nyama.

Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM) alisema Tanzania ina hazina kubwa na mifugo, lakini wafugaji wameshindwa kupata faida kutokana na kazi yao kwa kuwa serikali haijatoa elimu ya kutosha.

Kwa upande wake, Lekule Laizer (Longido CCM), alisema migogoro baina ya jamii hiyo imetokana na serikali kushindwa kuchukua hatua stahiki mapema akitolea mfano wa Hifadhi ya Murtangos iliyoko Kiteto, Manyara.

Ziadi ya watu 10 wameuawa katika mapigano makali kati ya wafugaji kutoka Wilaya ya Kiteto na wakulima wa Kongwa, Dodoma ambao wanagombea eneo lililotengwa kwa ajili ya hifadhi tengufu.

Nkamia aimwagisa sifa Steps Solar

CHARLES MGANGA
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Juma Nkamia ameimwagia sifa kampuni ya Steps Solar kwa mkakati wake wa kuwapa huduma ya nishati nuru wananchi wa kipato kidogo nchini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma, Nkamia alisema, tayari kampuni hiyo kwa kushirikiana na jamii, imefunga bidhaa zake za nishati ya mwanga katika maeneo mbalimbali wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.

Nkamia alitaja maeneo ambayo kampuni hiyo imetoa vifaa hivyo kwa ajili ya nishati ya mwanga kuwa ni pamoja na shule ya sekondari za Ovada na Kingale  na vituo vya afya vya Tandala na Itolwa.
 

Kimsingi naishukuru kampuni ya Steps Solar kwa kunikabidhi vifaa hivi kwa ajili ya nishati hii ya mwanga. Nina uhakika wanafunzi katika shule hizo watapata fursa ya kujisomea kwa wakati wanaotaka. Pia wagonjwa nao watahudumiwa vyema katika vituo hivyo vya afya ambavyo kampuni hiyo imepeleka nishati hiyo,î alisema Nkamia.

Nkamia ambaye ni mbunge wa Kondoa Kusini alisema, aliwasilisha maombi ya kupatiwa huduma hiyo kabla hajateuliwa kuwa Naibu Waziri.
 

Jamani, msaada huu kwa ajili ya hizi shule na vituo vya afya, niliomba kabla hata ya kuteuliwa kuwa naibu waziri," alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Dilesh Solanki alisema, lengo la kuanzisha kampuni hiyo ni kuona idadi kubwa ya watu wanaoishi hasa maeneo ya vijijini wakitumia nishati nuru.

Alisema, kwa sababu watu wengi hawajanufaika na huduma hiyo, kampuni yake imeanzisha nishati nuru kwa kushirikiana na serikali katika jitihada za kuhakikisha nishati nuru iliyo na gharama nafuu inasambaa nchini kote.

Alitaja baadhi ya maeneo ambayo mpaka sasa yamenufaika na nishati hiyo ni vituo vya polisi Mjimwema na Feri, vituo vya afya Mjimwema, Ungindani vyote vya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Alhaji Kimbisa awafunda wanachama wapya 200

 NA SAKINA MASOUD, DODOMA
MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaj Adam Kimbisa, amewataka wanachama wapya 200 waliojiunga na CCM katika Kata ya Chifutuka wilayani Bahi kuwa  waaminifu na waadilifu bila ya kuhangaika na vyama vinavyoundwa kiukoo.

Alhaj Kimbisa alitoa rai hiyo juzi wakati akikabidhi kadi katika muendelezo wa ziara yake ya kuangalia utekelezaji wa Ilani, kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwenyekiti na kuangalia uhai wa Chama katika Mkoa wa Dodoma.

Alisema CCM ndio chama pekee ambacho kipo kwa ajili ya kila mtu, tofauti na vyama vingine ambavyo ukiangalia hata majina yao ni yale yale ya kutoka kule kule.
 

Wanachama wenzangu mliokula kiapo leo (juzi) msibabaike na vyama vingine, CCM imewazaa, imewalea na mnazeeka mkiwa nayo, msiwe kama baadhi ya watu ambao sio waaminifu wanaoonekana  asubuhi wakiwa  CCM, mchana CHADEMA na usiku anakuwa CUF,”alisema.

Pia, aliwataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaokuja na kusisitiza kuchagua mtu aliye tayari kuwatumikia wakati wote wa uongozi wake na asiye tayari kutoa au kupokea rushwa.


Ndugu zangu uchaguzi unakuja na mna nafasi ya kugombea nafasi yoyote mnayoona inafaa kwako, lakini wajibu wenu mkubwa ni kuangalia aina ya kiongozi mnaemchagua nyinyi wenyewe ili kesho  na keshokutwa msilalamike maana mtakuwa mmemchagua wenyewe,”alisema  Kimbisa.

Kimbisa aliwaahidi kuwa kama mkoa hawatakata jina la mgombea yoyote aliyependekezwa na wananchi na kuwasisitiza kuhakikisha kura zote wanapeleka CCM.

Katika ziara yake kwenye kata hiyo aliahidi kupeleka ‘solar’ katika Shule ya Sekondari ya Magaga ili wanafunzi waweze kusoma vizuri.

Nyambacha: Tunatoa elimu kwa ngazi zote

NA EVA-SWEET MUSIBA
JESHI la Zimamoto na Uokoaji limesema litatoa elimu kwa makatibu wakuu na viongozi wakiwemo wengine wakiwemo wabunge, vyama vya siasa katika ngazi zote ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na majanga ikiwemo moto.
Akizungumza katika kikao cha makamanda wa mikoa kote nchini, kilichofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam,  Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha, alisema ni muhimu elimu itolewe kwa viongozi hao  ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na majanga na wafahamu majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Pia , amewakumbusha makamanda hao kujilinda kunapotokea majanga ya moto wawapo kazini.

Alisema jeshi hilo limeanza utaratibu wa kutoa elimu kwa viongozi wake na  viongozi wa kisiasa kote nchini ili kuwahamasisha wananchi wao kujilinda na kujikinga na majanga ya moto yanapotokea.

Tumekuwa tukitoa elimu kupitia vyombo vya habari, lakini sasa tumepanua wigo mpaka kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuzuia majanga yasitokee na kuwamahasisha wananchi kutii sheria husika, alisema Nyambacha.

Kuhusu changamoto zinazolikabili jeshi hilo, Nyambacha alisema ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kazi kama magari, upungufu wa vifaa vya kuzimia moto, ubovu wa barabara kwa baadhi ya mikoa na msongamano wa magari katika majiji hasa Dar es Salaam na Arusha ambao unachangia kuchelewa kufika eneo la tukio.

Alisema kuwa kanuni ya ukaguzi na vyeti imefanyiwa marekebisho, hivyo  tozo zimepungua kulinganisha na hapo awali na kuna ambazo zimepanda kutoka na ukubwa kwa eneo.

Mhe. Sophia Simba awakabidhi kadi za CCM wapya 400 Baraza UWT Kinondoni.








Thursday 22 May 2014

Pata nakala yako



SAKATA LA MTOTO ALIYEISHI NDANI YA BOKSI


Mazito  yaibuka

  •  Abainika kuathirika mifupa, Nduguye hajulikani alipo

NA LATIFA GANZEL, MOROGORO
SAKATA la mtoto Nasra Mvungi (4), aliyefichwa ndani ya boksi kwa miaka mine, limechukua sura mpya baada ya mtoto huyo kufanyiwa uchunguzi na kubainika kwamba ana hitilafu kwenye mifupa.
Mtoto huyo alikuwa akiishi kwenye boksi kwa miaka minne baada ya kufichwa na wazazi wake walezi, Mariam Said na mumewe, Mtonga Omari ambao tayari wanashikiliwa na polisi.

Kutokana na hali hiyo, mtoto huyo anatarajiwa kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili yakupatiwa matibabu makubwa zaidi.
Mbali na matokea ya uchunguzi kuonyesha hali hiyo, pia imebainika kuwa kaka wa Nasra, anayeitwa Nasoro, hajulikani alipo na hivyo kuzidi kuzua hofu dhidi ya mama yao mkubwa, Mariam Said.
Akizungumza na Uhuru jana, Daktari Mshauri wa Masuala ya Watoto wa Hospitali ya mkoa wa Mrorogoro, Dk. Isaack Msaky alisema vipimo vimeonyesha kwamba mtoto huyo ana matatizo ya mifupa ya mikono na miguu.
“Tulifanya vipimo vya x-ray na kugundua kwamba mtoto huyu, ana matatizo ya mifupa, hivyo inatulazimu tumuhamishie Hospitali ya Taifa Muhimbili,”alisema Dk. Msaky.
Hata hivyo, alisema watamuhamishia Muhimbili baada ya kumpatia matibabu ya ugonjwa wa homa ya vichomi (Nimonia) unaomsumbua mtoto huyo.
Dk. Msaky alisema mbali na ugonjwa huo, pia mtoto huyo aligundulika kuwa na tatizo la utapiamlo mkali, ambao umesababisha afya yake kudhoofika.
Wakati huo huo,  mtoto mwingine, ambaye ni kaka wa Nasra, aliyefahamika kwa jina la Nasoro, hajulikani alipo hali ambayo imeendelea kuzua hofu kwa majirani.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Mariam aliachiwa watoto wawili baada ya mdogo wake kufariki, lakini mtoto mmoja alionekana kwa miezi kadhaa na baadaye kutoweka.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Azimio anakoishi Mariam, Tatu Mgalagala, alisema kwamba Mariam aliachiwa watoto wawili, lakini mmoja haonekani.
Tatu alisema  majirani wa Mariam walisema walimuona mtoto huyo, anayekadiriwa kuwa na miaka minane, wakati wa msiba wa mama yao, lakini baada ya miezi kadhaa, mtoto hajaonekana hadi sasa.
Wakizungumza na Uhuru, majirani wa Mariam walilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na mazingira anayoishi mama huyo.
Walisema wakati mdogo wake anafariki, Mariam alikabidhiwa watoto wawili, Nasra na Nasoro, lakini kwa muda mrefu hawajamuona mtoto huyo wa kiume.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paul, alisema polisi bado wanafanya uchunguzi na kwamba watatoa taarifa watakapokamilisha.
Juzi polisi mkoani hapa waliwakamata Mariam na mumewe, Omari kwa tuhuma za kufanya unyama huo nyumbani kwao katika mtaa wa Azimio, kata ya Kiwanja cha Ndege.
Kamanda  Paul alisema tukio hilo lilibainika baada ya majirani kushuhudia  unyama huo, ikiwa ni pamoja na Nasra kutoonekana nje.
Alisema kutokana na kuumizwa na unyama huo, jana majirani waliamua kuizingira nyumba wanayoishi wanandoa hao, lakini polisi walipata taarifa kwa raia wema na kufika eneo la tukio.
Kamanda Paul alisema baada ya polisi kufika eneo hilo, walielezwa kinachoendelea na kuamua kufuata taratibu za kuingia ndani ya nyumba na hatimaye kumkuta Nasra akiwa kwenye boksi.
Kutokana na tukio hilo, polisi walilifikisha suala hilo katika ofisi za Ustawi wa Jamii mkoa kwa hatua za awali.
Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswing Ngungamtitu, alisema mtoto huyo alipokewa akiwa na hali mbaya kiafya na sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufani mkoani hapa.
Alisema hali ya Nasra si nzuri na kwamba, afya yake imedhoofu kiasi cha kuonekana kama mtoto mchanga.
Ofisa huyo alisema kwa sasa Nasra yuko chini ya uangalizi wa ofisi yake huku wakisubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Akizungumza na waandishi wa habari, baba mzazi wa mtoto huyo, Nassoro Rashid alisema alimkabidhi Nasra kwa Mariam na amekuwa akitoa gharama zote za matunzo ya binti yake.
Alisema kwa sasa anaye mke mwingine wa ndoa na watoto na kwamba, hakuwahi kumweleza mkewe huyo kuhusu kuwa na mtoto mwingine nje ya ndoa.
“Nimeumizwa mno na hali niliyomkuta nayo mwanangu. Nilimkabidhi kwa mama yake mkubwa na naleta matunzo kwa ajili yake kila wakati. Mara kadhaa ninapofika na kutaka kumwona, ananieleza kuwa amelala, hivyo sipati fursa ya kumuona,” alisema Rashid.

Raia wa Romania kortini kwa kuihujumu TCRA


Na Furaha Omary
MABOSI wawili wa Kampuni ya X Plora Ltd,  raia wa Romania, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashitaka ya kufanya mawasiliano ya simu za kimataifa bila leseni na kuisababishia serikali hasara ya sh.bilioni mbili.
Meneja Mtendaji wa kampuni hiyo, Razvan Pantilie (47) na Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Robert Kraus (27), wanaoishi Hoteli ya Serena, walipandishwa kizimbani jana mahakamani hapo.
Washitakiwa hao, ambao wanatetewa na Wakili Alex Mgongolwa, walisomewa mashitaka saba na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Isaya Arufani.
Kweka alidai washitakiwa walitenda makosa hayo, kati ya Aprili na Mei, mwaka huu, katika ofisi za Raha Data Center, zilizoko maeneo ya Banda la Ngozi, Dar es Salaam.

Alidai katika tarehe tofauti, washitakiwa hao walifanya mawasiliano ya simu za kimataifa kinyume cha sheria kwa kutokuwa na leseni ya TCRA, kwa lengo la kukwepa kodi.
Pia, alidai katika kipindi hicho, washitakiwa hao waliingiza nchini vifaa vya mawasiliano bila kuwa na leseni ya TCRA.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuingiza nchini Voice over Internet Protocol (VOIP) nne na kuvifunga bila kuwa na kibali cha kuwaruhusu kufanya hivyo.
Pia, washitakiwa hao wanadaiwa kutumia vifaa hivyo vya mawasiliano, ambavyo havijathibitishwa na TCRA.
Katika shitaka la sita, ambalo linamkabili ofisa mtendaji mkuu huyo, anadaiwa alibadilisha usajili wa umiliki wa kadi za simu bila ya kutoa taarifa kwa kampuni husika.
Mshitakiwa huyo anadaiwa alibabadili umiliki wa kadi za simu namba 0776990681 na 07769990758 zilizotolewa na Zantel(T) Ltd na kushindwa kutoa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa Zantel alipoihamishia kwa Global Com.
Shitaka la saba la kuisababishia hasara mamlaka husika linawakabili washitakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika kipindi hicho wakiwa hawana leseni, walitumia njia ya mawasiliano bila kibali na kuisababishia serikali na TCRA hasara ya sh. 2,109,888,000.
Hakimu alisema washitakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi hivyo hawatakiwi kujibu lolote.
Wakili wa Serikali alidai upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 27, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa walirudishwa rumande.
Machi, mwaka huu, TCRA ilimpandishwa kizimbani mahakamani hapo, raia wa Kenya, Nelson Rading Onyango, kwa tuhuma za kutoa huduma za simu za kimataifa bila ya leseni na hivyo kuisababishia serikali na TCRA hasara ya sh. bilioni  6.8 .

Bil. 220/- kutumika kujenga minara ya mawasiliano


ABDALLAH MWERI, DODOMA
SERIKALI inatarajia kutumia sh. bilioni 220 kwa ajili ya ujenzi wa mawasiliano katika mikoa yote ya Tanzania Bara kabla ya mwaka 2015.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
January, alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge Selemani Zedi (Bukene-CCM), aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga minara ya kutosha katika maeneo ya vijijini nchini.
Alisema wizara yake inatarajia kupata sh. bilioni 154 ilizoomba kutoka serikali ya India, ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa minara ya mawasiliano nchini.
Alisema  dhamira ya serikali ni kujenga minara mingi ili kuwapa fursa wananchi kupata mawasiliano kwa uhakika.
January alisema pia kuwa, wizara yake ina mpango mkakati wa kujenga minara ya kutosha ya mawasiliano katika maeneo ya mipakani, ikiwemo mikoa ya Ruvuma na Kagera.
“Wizara imedhamiria kujenga minara mingi maeneo yote ya Tanzania yaliyokosa mawasiliano. Binafsi nilikwenda India kuomba fedha na tunatarajia kupata sh. bilioni 154, ambazo zitatumika kwa ujenzi wa minara,” alisema January.

Mifugo imepunguzwa Ulanga-Mwanry


SERIKALI imetumia sh. milioni 481.731 katika mchakato wa kupunguza mifugo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa(TAMISEMI), Aggrey Mwanry alisema hayo jana bungeni mjini hapa alipokuwa akijibu swali la  Hadji Mponda (Ulanga-CCM).
Mponda alitaka kujua mchakato wa kuhamisha mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kwa msimu wa kiangazi wa mwaka 2012 na gharama zilizotumika katika mpango huo.
Mwanry alisema kiasi kilichopangwa katika utekelezaji wa mpango huo kilikuwa sh. 85,000,000, ambapo Wizara ya Maliasili na Utalii ilitoa sh. 75,000,000 na Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ilitoa sh. 10,000,000.
Alisema jumla ya sh. 396,731,510 ziliongezeka kwa kuwa muda wa siku nne uliopangwa kwa ajili ya operesheni hiyo haukutosha, badala yake ilitumika miezi mitatu.
Naibu Waziri alisema katika kipindi hicho, ng’ombe waliokuwepo walikuwa 350,000, ambapo kati yao, ng’ombe 285,000 walipunguzwa na kubaki 65,700.
Akijibu swali la Lekule Laizer (Longido-CCM) kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji, Mwanry alisema serikali inafuatilia kwa makini kuhakikisha kila upande unapata haki stahiki kulingana na eneo husika.
Alisema migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa tatizo kubwa, hivyo wizara yake inaendelea na mpango mkakati wa kuhakikisha kila upande unamiliki ardhi yake kwa uhalali.
Naibu Waziri alisema miongoni mwa mikakati ya serikali ni kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji ili kuleta amani na utulivu miongoni mwao.

Kebwe: Maambukizi ya malaria yamepungua


WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema maambukizi ya ugonjwa wa malaria yamepungua kwa asilimia 47 kati ya mwaka 2008 na 2013.
Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe alisema mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini yamechangia kupungua kwa vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.
Alisema vifo hivyo vimepungua kutoka 148 kwa kila vizazi hai 1,000 waliozaliwa mwaka 1995-1999 hadi kufikia vifo 54 mwaka 2013.
Dk. Kebwe alikuwa akijibu swali la  Moza Saidi (Viti Maalumu-CUF), aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kupambana na ugonjwa huo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa za tafiti za viashiria vya ugonjwa wa malaria ngazi ya jamii, kiwango cha uwepo wa malaria mwaka 2008 kilikuwa asilimia 18 na mwaka 2012 kilishuka hadi asilimia 10.
“Wizara inahimiza juu ya matumizi sahihi ya dawa za kutibu malaria ili kuzuia kujitokeza kwa malaria sugu, matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu, kutumia nyenzo za kinga kama usafi wa mazingira, kudhibiti mazalia ya mbu na upulizaji wa dawa majumbani,” alisema.
Alisema serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa malaria nchini na miongoni mwa juhudi hizo ni kuwepo kwa dawa za kutibu malaria ya kawaida na kali katika vituo vya afya.
Alizitaja hatua zingine kuwa ni kugawa vyandarua vyenye uatilifu, kutoa dawa za kukinga malaria kwa mama wajawazito na kuelimisha jamii.
Aidha, alisema wizara kwa kushirikiana na serikali ya Cuba, imejenga kiwanda cha mradi wa dawa za kuua viluwiluwi kilichoko Kibaha, Pwani.
Wakati huo huo, serikali imesema dawa ya mseto imethibitika kuwa na uwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida wakati kwinini inatibu malaria sugu baada ya kupimwa na wataalamu katika maabara.

Wajasiriamali wa chumvi watakiwa kujisajili


SERIKALI imevitaka vikundi vya wajasiriamali wa chumvi, kujisajili ili kupata mikopo ya masharti nafuu na kujiunga na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA).
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanry, alitoa mwito huo jana alipokuwa akijibu swali la
Christina Lissu (Viti Maalumu-CHADEMA).
Mbunge huyo alitaka kujua mkakati wa wizara kuhusu wanakijiji wa kata ya Kikio na Misughaa wilayani Ikungi, wanaojishughulisha na uzalishaji chumvi katika ukanda wa Bonde la Ufa.
Mwanry alisema Halmashauri ya  Ikungi inavyo vikundi viwili vya uzalishaji chumvi, ambavyo ni NGAA Group na ISANJA Group, vilivyoanzishwa mwaka 2007, ambavyo vina jumla ya wanachama 165.
Alisema serikali kwa kutambua umuhimu wa vikundi hivyo, ilivipatia mabomba 30 kupitia uhisani wa UNICEF kwa ajili ya kuchanganya madini joto na chumvi.
Naibu Waziri alisema pia kuwa vikundi hivyo vilipewa madini joto na vifaa vya kupimia madini joto kutoka Tanzania Food $ Nutrition Centre (TFNC) na mafunzo ya jinsi ya kuchanganya chumvi, madini joto na kuhifadhi chumvi isipoteze ubora.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Halmashauri ya wilaya ya Singida kabla ya kugawanywa kuwa mbili, ilipata mkopo kwa vikundi 14 vya kinamama wajasiriamali vilikopeshwa sh. 7,000,000 mwaka 2012.
Alisema mwaka 2013/2014, vikundi 19 vya kinamama wajasiriamali vilikopeshwa sh.milioni tisa na mwaka huu, Halmashauri ya Ikungi imetenga sh. 62,800,000 kwa ajili ya mikopo ya masharti nafuu kwa vikundi vya kinamama na vijana.

Kivuko Dar-Bagamoyo mwezi ujao


NA ABDALLAH MWERI
UJENZI wa kivuko kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo, kitakamilika mwezi ujao tayari kwa kuanza kazi.

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema hayo bungeni juzi wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo na Makadirio ya Mapato na Matumizi katika mwaka wa fedha 2014-2015.
Dk. Magufuli alisema ujenzi wa kivuko hicho unaendelea nchini Bangladesh na ukamilishwaji wake utakuwa na ustawi mzuri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo.
Pia alisema ujenzi wa kivuko cha Kahunda/Maisome unaendelea mkoani Mwanza, sanjari na kivuko cha Msangamkuu na boti ya uokozi, itakayotoa huduma mkoani Mwanza.
Alisema ujenzi wa maegesho ya vivuko vya Msangamkuu, Muharamba, Kikumbaitale na Senga umekamilika tangu Aprili, mwaka huu.
Aliongeza kuwa utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya kuwapata makandarasi wa ujenzi wa maegesho ya Kilambo, Ukara, Ilagara, Bugolora na Kivuko kwa usafiri wa majini kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo unaendelea.
Alisema ukarabati wa kivuko cha MV Chato umekamilika na kinaendelea kutoa huduma na ukarabati wa vivuko vya MV Kome 1 na MV Geita unaendelea mkoani Mwanza.
Dk. Magufuli alisema ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni na MV Kilombero 1 uko katika hatua ya kumpata mkandarasi. Alisema katika mwaka wa fedha 2014-2015, mradi wa ukarabati wa vivuko vya MV Magogoni, MV Mwanza, MV Kiu na MV Pangani 11 umetengewa sh. bilioni 2.1.
Akifafanua, alisema kivuko cha MV Magogoni kimetengewa sh. milioni 660, MV Mwanza (sh. milioni 500), MV Morogoro (sh. milioni 400) na MV Pangani 11 (sh. milioni 472). 
Katika hatua nyingine, Magufuli amesema ujenzi na ukarabati wa nyumba  na majengo ya serikali kwa ajili ya makazi ya viongozi na watumishi, umetengewa sh. milioni 2,689.46.
Waziri Magufuli alisema kipaumbele katika ujenzi wa nyumba hizo, kimelenga kwa majaji na viongozi wengine wa serikali wenye stahiki.
Alisema katika mwaka wa fedha 2014-2015, sh. milioni 200 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa nyumba ya makazi ya mkuu wa wilaya ya Urambo. 

Alisema zimetengwa sh. milioni 540 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa nyumba za majaji katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Mtwara, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Dk. Magufuli alisema sh. milioni 100 zimetengwa kuendelea na ujenzi wa uzio na kuweka mfumo wa ulinzi katika nyumba za viongozi wa serikali zilizoko Mikocheni,  Kijitonyama na Msasani Peninsular. 
Alisema Wizara ya Ujenzi imetenga sh. milioni 480 kwa ajili ya kufanya matengenezo na ukarabati wa nyumba za viongozi wa serikali na sh. milioni 500 kwa ununuzi wa samani.

Mbowe, Slaa wapewa siku 14 kujitoa UKAWA

Na Hamis Shimye
WANACHAMA wa CHADEMA wameupa siku 14 uongozi wao wa juu kujitoa katika muungano wa Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA).


Pia wametaka Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, liitishwe na lisimamiwe na baraza la wazee na si uongozi uliopo kwa kuwa umeonyesha ni watu wenye uchu wa madaraka.
Tamko hilo lilitolewa jana mjini Geita na Katibu wa BAVICHA mkoani Geita, Fikiri Migiyo, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Migiyo alitoa tamko hilo, kwa niaba ya wajumbe wenzake wa baraza kuu na mkutano mkuu katika mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu na Kagera.
Alisema wanaungana na kuwapongeza wajumbe wenzao wa mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Tanga kuukemea upuuzi huu wa UKAWA.
“Suala hili halipaswi kuvumiliwa na ninawaomba wanachama wenzangu katika mikoa mingine, wasimame na wakemee kwa pamoja kuondoa upuuzi huu,’’ alisema.
Migiyo alisema CHADEMA ni chama makini kinachoamini katika nguvu ya umma na sio nguvu ya viongozi, ambao wameendelea kuwaburuza  wanachama.
Alisema viongozi wa ngazi za chini ndani ya CHADEMA wanaburuzwa bila kushirikishwa katika maamuzi ya chama.
“Tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha viongozi wetu wa juu kufanya maamuzi ya kihuni na ya kifedhuli kususia Bunge Maalumu la Katiba na kujiunga katika umoja wao,’’ alisema.
Kiongozi huyo alisema kuanza kutoa masharti ni mambo ya kitoto na wanapaswa kurudi bungeni ili kuendelea na mchakato huo.
“Tunasikitishwa na unafiki huu uliopitiliza, viongozi wetu wamekubali kuwa sehemu ya matapeli wa kisiasa, wamekwenda kwenye Bunge la Katiba kula posho zinazotokana na kodi zetu walala hoi, halafu wameacha kufanya walichotumwa,’’ alisema.
Alisema kuanzishwa kwa UKAWA na kususia Bunge la Katiba ni muendelezo wa siasa za kinafiki kwa kuwa huu ni muendelezo wa mipango ya kuwahadaa watanzania kupitia misimamo yao.
Hivyo alisema wanautaka uongozi chini ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa kuitisha kikao cha baraza kuu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Tamko la wajumbe hao, kupinga chama chao kujiunga na UKAWA, limekuja muda mfupi baada ya wajumbe wenzao kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Tanga kupinga uamuzi huo.

Wabunge waitaka serikali ipunguze msongamano Dar



  •  Washauri kuwepo na tozo ya barabara kwa wanaokwenda mjini
  •  Filikunjombe amfagilia Magufuli, asema ni mtendaji kazi makini

NA THEODOS MGOMBA,DODOMA
SERIKALI imeshauriwa kuweka mkakati wa kitaifa kwa kukopa fedha kutoka vyombo vya fedha vya ndani na nje  kwa ajili ya kutatua tatizo la msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.
Pia imeshauriwa kuweka tozo ya barabara ili kupunguza watu wanaokwenda mjini bila kuwa na kazi maalumu na badala yake kwenda kupiga mizinga.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu alipokuwa akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi.
Zungu alisema ni vyema serikali ikakopa kutoka vyombo vya fedha vya ndani au nje ili kuboresha miundombinu, hususani barabara ili kupunguza msongamano uliopo hivi sasa.
Alisema serikali haina haja ya kuogopa kukopa kwani mara baada ya miundombinu kukamilika, mkopo huo unaweza kujilipa kutokana na kodi mbalimbali, ikiwemo ya barabara na majengo.
“Kama ilivyofanya kwa mji wa Dodoma, serikali ikope hata sh. bilioni 400 tu kwa ajili ya kazi hiyo na mkopo utajirejesha wenyewe kwani kama mtu akiona maboresho yamefanyika, hawezi kukataa kulipa,” alisema.
Zungu alisema pia kuwa ni vyema kukawa na utaratibu wa kulipia gharama za barabara ili kupunguza idadi ya watu wanaokwenda katikati ya mji bila ya kuwa na sababu.
ìEndapo kutakuwa na kodi, kila anayetaka kuingia mjini ni lazima alipe, basi wale ambao hawana kazi mjini hawawezi kwenda na hivyo kupunguza msongamano,”alisema.
ìWapo wengine wanakwenda mjini hawana cha kufanya, wanakwenda kupiga mizinga tu, sasa watu kama hawa hawataweza kwenda kwani hawatakuwa na fedha za kulipia na hivyo kupunguza idadi ya magari na hivyo kupunguza msongamano,” aliongeza.
Mbunge huyo pia aliitaka Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inaitendea haki barabara ya Uhuru kwani inatia aibu.
Alisema inashangaza barabara hiyo, ambayo ipo katika Jimbo la Ikulu, imekuwa na mashimo na haifai kiasi kwamba magari yanakwama.
Kwa upande wake, mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe alisema Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Dk. John Magufuli hayumo katika mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo kwani anachokifanya kinaonekana.
Alisema endapo Tanzania ingekuwa na mawaziri watano kama Dk. Magufuli, ingefika mbali kwani amekuwa akifanya kazi zake kwa umakini mkubwa.
Filikunjombe alisema ni vyema waziri huyo akaendelea na utaratibu wake wa kujenga barabara katika sehemu zote kidogo kidogo na si kujenga sehemu moja.
ìWanosema sijui barabara zangu za Kawe, sijui za wapi hazijengwi, hapana wewe ni waziri wa Watanzania wote, hivyo jenga hivyo hivyo kidogo kidogo kila sehemu waguswe,” alisema.
Mbunge huyo alimshukuru Waziri Magufuli kwa kuanza ujenzi wa barabara katika jimbo lake na kusema kuwa, endapo kasi hiyo ingeanza miaka ya nyuma, hivi sasa barabara zingepitika zote katika jimbo hilo.