Monday, 22 December 2014

LIVERPOOL, ARSENAL ILIKUWA SHUGHULI PEVU

KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers, akiteta jambo na nahodha wake Steven Gerrard, katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal uliochezwa juzi usiku Uwanja wa Anfield. Timu hizo zilitoka sere ya mabao 2-2.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck, akiruka juu kumpongeza, Olivier Giroud, aliyefunga bao na Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) katika mchezo dhidi ya Liverpool.

BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel, akipata huduma ya kwanza baada ya kugongana na Olivier Giroud wa Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England.

MCHEZAJI wa Liverpool, Philippe Coutinho, 'akikontroo' mpira mbele ya kiungo wa Arsenal, Oxlade-Chamberlain katika mchezo wa Ligi Kuu England.

PHILIPPE Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake wa Liverpool, baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Arsenal.

BEKI wa Arsenal, Mathieu Debuchy (kushoto), akifurahia bao alilofunga dhidi ya Liverpool.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru