NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, amewashukia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa madai ya kusambaza taarifa za uongo dhidi yake.
Mengi alisema hayo katika taarifa yake aliyotoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari, zilizoeleza kwamba amezushiwa kuwa alimpatia Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, mabilioni ya shilingi kwa lengo la kuwahonga wabunge ili wapinge vikali wizi uliofanyika kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Katika taarifa hiyo aliwataja Masele na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, kwamba wanahusika kutoa taarifa kwamba alitoa fedha hizo ambazo hakutaja kiwango kamili kwa wabunge.
“Ole Sendeka ni rafiki yangu, kwa hiyo nilimwuliza kuhusu taarifa hiyo. Alinijibu kwamba siku moja akiwa amekaa meza moja na Masele kule Dodoma alipigiwa simu na kijana wake ikabidi aombe radhi na kusogea pembeni ili aweze kusikiliza simu hiyo.
“Masele ni mtu wa ajabu kwani alimtuma mhudumu eti aje kusikiliza mazungumzo yake ya simu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Mengi.
Hivi karibuni katika vikao vya Bunge, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwana mbunge wa Kigoma Kaskazini, iliwasilisha ripoti juu ya akaunti ya Tegeta Escrow na kuibua mjadala mkali.
Thursday, 18 December 2014
Mengi sasa awageukia Masele, Maswi, Wassira
06:41
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru