Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Pata mafanikio, tangaza hapa

Tangaza nasi hapa.

Friday 28 June 2013


MWENYEJI wa mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa wa Manufaa kwa Wote, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kumbukumbu wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana, ambako majadiliano hayo yanafanyika.

Ujio wa Obama



ANGA la Tanzania litafungwa kwa nusu saa kabla ya kuwasili ndege ya Rais Barack Obama wa Marekani, Jumatatu mchana.
Rais Obama anatarajiwa kuwasili nchini akitoka Afrika Kusini, baada ya kuzuru Senegal, katika ziara yake ya pili barani Afrika, tangu aingie madarakani.
Ujio wa Rais Obama unasubiriwa kwa hamu, huku wengi wakiwa na matarajio ya kuboreshwa au kuongezwa ufadhili wa miradi ya maendeleo.
Kutokana na ujio wa Obama, ambaye ni kiongozi wa taifa kubwa duniani, ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, hususan Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na hoteli kadhaa za Jiji la Dar es Salaam, ambazo ujumbe wa kiongozi huyo utafikia.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Deusdedit Kato, akizungumza na gazeti hili jana,  alisema maandalizi yamekamilika na ulinzi umeimarishwa.
Alisema anga la Tanzania litafungwa kwa nusu saa kabla ya kuwasili ndege ya Rais Obama kwa sababu za kiusalama.
Kamanda Kato alisema vifaa vitakavyotumika katika ziara hiyo vimeshawasili, yakiwemo magari manne ya mizigo yaliyokuwa na vifaa vya mawasiliano.
Kato alisema magari hayo yaliletwa na ndege tatu zilizotua nchini Jumanne wiki hii na baadaye kuondoka.
Leo saa saba usiku inatarajiwa kuwasili ndege ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Marekani,” alisema.
Alisema wanatarajia pia zitawasili ndege zitakazobeba magari 50, ambayo yatatumika katika msafara wa rais huyo.
Kamanda Kato alisema Rais Obama atawasili na ndege mbili, moja ikiwa ni ya akiba.
Katika hatua nyingine, alisema teksi zinazoegeshwa uwanja wa ndege zitaondolewa Jumatatu na zitarejeshwa baada ya rais huyo kuondoka nchini.
Alisema magari ya wafanyakazi yataruhusiwa kuingia uwanjani baada ya ukaguzi kufanyika.
Kato alisema msafara huo utapishwa kama misafara mingine, na hakuna mawasiliano yatakayokatwa.
Kwa mujibu wa Kato, safari za anga zitakuwa kama kawaida baada ya kiongozi huyo kuwasili.
Aliwaomba wananchi kuwa wavumilivu kutokana na msongamano utakaosababishwa na msafara huo, kwani ziara hiyo ina manufaa kwa taifa.
Uwanjani hapo jana kulikuwa na ulinzi mkali, kukiwa na makundi ya askari wenye silaha waliokuwa wakifanya doria.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limesema Barabara ya Nyerere haitafungwa kwa saa tano, siku ya ujio wa Rais Obama, kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Polisi imesema haijatoa taarifa rasmi ya matumizi ya barabara siku hiyo na kwamba, litafanya hivyo siku moja kabla.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kumekuwa na habari nyingi za upotoshaji kuhusu ujio wa kiongozi huyo, kiasi cha kuwatia hofu wananchi.
Shughuli hazitasimama, mambo yataendelea kama kawaida. Barabara kubwa ya kwanza kutumika itakuwa Nyerere, lakini haitafungwa kwa saa tano kama inavyodaiwa, wananchi wasiwe na hofu,” alisema.
Licha ya ziara ya Rais Obama, Tanzania ina ugeni mwingine mkubwa wa viongozi wakuu wa nchi na marais wastaafu wanaohudhuria mkutano wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Alisema barabara zingine zitakazohusika ni zinazoingia katika hoteli kubwa, ambazo zitafungwa kwa muda asubuhi na jioni wakati wa wajumbe wakiingia na kutoka kwenye mkutano.
Katika hatua nyingine, wananchi wamepongeza usafi uliofanyika katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kutaka suala hilo liwe endelevu.
Pongezi hizo pia zimekuwa zikitolewa kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakisema ˜Dar es Salaam safi inawezekana
Licha ya usafi huo, baadhi ya wafanyabiashara walio kwenye maeneo yasiyo rasmi, wamekaidi kuondoka.
Baadhi ya wafanyabiashara hao waliendelea kupanga viatu, tai na bidhaa nyingine katika maeneo ya Posta, huku walioshika bidhaa mkononi wakiendelea na shughuli zao.

Mgumba ateuliwa Naibu Kamishna Zimamoto

NA MWANDISHI WETU
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Luteni Kanali Lidwino Mgumba, kuwa Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, uteuzi huo ulianza Juni 20, mwaka huu.
Taarifa hiyo, ilisema kuwa Luteni Kanali Mgumba ambaye ni Ofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ni mchambuzi na mtaalamu wa kijeshi katika masuala ya ulinzi, amani, diplomasia, usuluhishi wa migogoro na mawasiliano ya umma.
Ilisema kuwa taaluma hizo alizipata katika vyuo mbalimbali vikiwemo vya kijeshi na vya kiraia ndani na nje ya nchi.
Pia, ilisema Luteni Kanali Mgumba amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika JWTZ ikiwemo Msaidizi wa Kijeshi wa Mkuu wa Komandi ya Jeshi la Nchi Kavu na kuwa Msaidizi wa Kijeshi wa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Amtoa roho mwenzake katika ulevi

Na Samson Chacha, Tarime

MKAZI wa kijiji cha Ngoreme, Maheli Chacha, anasakwa na Polisi kwa tuhuma za kumshambulia mwenzake na kumsababishia kifo.
Chacha, anadaiwa kumpiga marehemu huyo walipokuwa wakinywa pombe za kienyeji.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime /Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa Chacha (43), anasakwa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Kapecho Robert (41), mkazi wa kijiji cha Bisarwi, kata ya Nyangoto.
Alisema tukio hilo lilitokea Juni 26, mwaka huu, mchana, katika kijiji cha Bisarwi kata ya Nyangoto, baada ya kuzuka ugomvi kati ya mtuhumiwa na Robert.
Kamugisha alisema katika ugomvi huo, Maheli alimshambulia Robert kwa ngumi na mateke tumboni na kumsababishia maumivu makali ambapo alizimia na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya Tarime.
Alisema Robert alikufa siku iliyofuata wakati akipatiwa matibabu na mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio.
Kamanda huyo, alisema polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa.
Pia, alisema mwili wa Robert umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo ukisubili kuchukuliwa na ndugu zake kwa mazishi.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa mara watakapomwona Maheli ili aweze kuchukulia hatua za kisheria.

Smart partnership kuinua sekta ya utalii

Na Mwandishi Wetu
 NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, amesema majadiliano ya pamoja kwa manufaa wa yote ‘smart partnership dialogue’ yatasaidia kuinua sekta ya utalii nchini.
Pia, alisema mkutano huo utasaidia kubadilisha mtazamo wa jamii katika sekta ya utalii na maliasili pamoja na kuanza utafutaji wa masoko ya utalii kiteknolojia.
Nyalandu aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kutembelea mabanda ya maonyesho ya mkutano huo. Mkutano huo utadumu kwa siku tatu na ulianza jana.
Alisema majadiliano haya ni muhimu kwani yanashirikisha watu wengi ambao watakuwa dira ya kubadilisha fikra na mtazamo wa sekta ya utalii na kuwezesha utafutaji wa masoko kiteknolojia.
â€Å“Kukua kwa teknolojia ni jambo la muhimu na kila nchi iliyoendelea na kupiga hatua ipo juu kiteknolojia, hivyo, naamini majadiliano haya ni chachu ya kupiga hatua zaidi,’’ alisema.
Nyalandu aliwataka Watanzania waliobahatika kushiriki katika majadiliano hayo, kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao kwa kuwa wamepata fursa muhimu.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema serikali imeanza kupiga hatua kubwa katika sekta ya utalii kwa kuutangaza kimataifa.
Awali tulikuwa tunaielezea sekta ya utalii kupitia makabrasha au vipeperushi, lakini sasa tumeingia katika mitandao, haya ni mafanikio, ninatumaini mkutano huu utatupa watalii zaidi,̢̢۪۪ alisema Nyalandu.

Vyama vya siasa mtegoni

Na Theodos Mgomba, Dodoma
SERIKALI imesema itachukua hatua kali kumaliza njama zinazofanywa na kundi la watu wachache, wanaopandikiza chuki za kisiasa na kidini nchini, hivyo kuvuruga amani na utulivu.
Imesema vyama vya siasa vitakavyobainika kuhusika na uvunjifu wa amani vitachukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa mujibu wa sheria.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema hayo bungeni jana, alipotoa hotuba ya kuahirisha Bunge.
Alisema hatua hizo zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo, bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuna dalili za kuwepo vikundi vya watu wachache wasioitakia mema Tanzania, kwa kupandikiza chuki za kisiasa na kidini miongoni mwa wananchi.
Alisema pia vimekuwa vikileta mauaji na mapigano miongoni mwa wananchi.Sina shaka kuwa fujo, vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani, ikiwemo mashambulio ya mabomu Arusha na vurugu za Mtwara ni sehemu ya mikakati hiyo mibovu,̢̢۪۪ alisema.
Waziri mkuu aliwasihi viongozi wa serikali, kisiasa, kidini na wananchi kwa jumla, kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa kisiwa cha amaTuendelee na mshikamano wa kukataa vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi yetu, kila mtu mwenye taarifa za kuwezesha kukamatwa kwa watu wanaohatarisha amani azitoe kwa vyombo vya dola na zitafanyiwa kazi kwa umakini kwa maslahi ya taifa,̢̢۪۪ alisema.

Pinda alisema katika kuhakikisha amani inadumishwa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewakutanisha viongozi wote wa vyama vya siasa na Jeshi la Polisi.

Alisema lengo la mkutano huo ni kueleza dhima ya polisi na vyama vya siasa katika kukua kwa demokrasia na amani nchini.

Kwa mujibu wa Pinda, katika mazungumzo hayo, viongozi wa vyama vya siasa walilaani tabia ya baadhi ya vyama kujihusisha katika kuvunja amani.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya vurugu yanayohusishwa na vyama vya siasa, huku sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake zinakataza vyama kujihusisha na vurugu, kuigawa nchi kwa udini, ukabila rangi au aina yoyote ya ubaguzi, ambayo itasababisha amani kutoweka.

Pinda alisema sheria hiyo pia ipo wazi kuwa, chama kitakachobainika kufanya hayo kitafutwa kwa mujibu wa sheria.

â€Å“Nawakumbusha viongozi wenzangu wa kisiasa kuwa, demokrasia si kufuta vyama au kuvuruga amani ya nchi, bali ni kuwa na sera nzuri zinazowaunganisha Watanzania na kudumisha amani.

â€Å“Nawaomba wanasiasa na viongozi wenzangu, tusijaribu kuweka nchi yetu rehani kwa kuhamasisha kwa njia moja au nyingine wananchi kuvuruga amani. Tuwafundishe kupendana, kuvumiliana na kusaidiana,’’ alisema.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu alisema serikali imeendelea kuwaondoa madarakani viongozi wasio waadilifu katika vyama vya ushirika, kutokana na kukithiri vitendo vya wizi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Alisema vitendo hivyo vimesababisha baadhi ya vyama kuiingia kwenye migogoro na madeni makubwa, kutokana na hasara za mara kwa mara zinazosababisha wanachama kukata tamaa kuhusu ushirika.

Pinda alisema viongozi hao pia wametozwa fidia ili kurejesha fedha zilizofujwa na kwamba, utaratibu wa kuchukua hatua zaidi za kijinai unaandaliwa.

Waziri mkuu alisema serikali itaunda timu imara ya ukaguzi, ikihusisha wakaguzi kutoka katika halmashauri.

Bunge limeahirishwa hadi Agosti 26, mwaka huu, litakapokutana katika mkutano wa 12.

Wednesday 26 June 2013

Ongezeko dawa za kulevya laogofya


Na Theodos Mgomba, Dodoma
KASI ya ongezeko la dawa za kulevya nchini imeanza kuitisha serikali, ambayo imesema ikiachwa inaweza kuendelea kuleta athari kubwa.
Imesema wafanyabiashara wa dawa za kulevya ni watu hatari na kwamba, wanaweza kuingilia misingi ya kiutawala, hivyo Watanzania hawana budi kuipiga vita kwa nguvu zote.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani.
Katika hotuba hiyo, Pinda amesema miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
Alisema iwapo biashara hiyo haitadhibitiwa kikamilifu na kuachwa ikaendelea moja ya athari zitakazojitokeza ni kuingiliwa kwa misingi ya utawala na ongezeko kubwa la rushwa.
Pinda alisema wafanyabiashara wa dawa za kulevya baadhi wamekuwa wakiwatumia watendaji wa serikali katika kufanikisha mambo hayo haramu.
Waziri mkuu alisema kushamiri kwa biashara hiyo kunaongeza mtandao wa fedha haramu na kusababisha mfumuko wa bei, hatua itakayoongeza umasikini kwa wananchi wa kawaida.
“Biashara hii ni hatari, inapaswa kupigwa vita. Ikiachwa itaendelea kuleta athari kubwa na wananchi watashindwa kumudu huduma za kijamii, kama vile elimu na afya. Uwezo wa serikali katika kutoa huduma muhimu unaweza kupungua kutokana na biashara hii haramu,” alisema.
Alisema Watanzania wengi wamekuwa wakijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, hali inayoharibu taswira ya nchi kimataifa.
Waziri mkuu alitoa mfano kuwa, katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012, watuhumiwa 10,799 walitiwa mbaroni kwa kujihusisha na biashara hiyo nchini.
Katika kipindi hicho, alisema  Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na baadhi wamefungwa.
“Hali hii inaharibu taswira ya nchi kimataifa, Watanzania wasio na hatia wanapata usumbufu na kuwekewa masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali kutokana na sifa mbaya.
“Wachache wanafanya wengi wanapata usumbufu na kushindwa kutumia fursa za kibiashara zilizoko katika nchi za nje,” alisema.
Kuhusu ukamataji wa dawa hizo, alisema kumekuwa na juhudi kubwa zinazofanywa na vyombo vya dola na kwamba, kiwango kinachokamatwa ni kikubwa.
Hatua hiyo alisema inatokana na ulinzi mkali katika mipaka na maeneo mengine ya kuingia nchini, ambapo kuanzia mwaka 2010 hali imekuwa mbaya kuliko miaka ya nyuma.
Ukamataji mkubwa umekuwa ukifanyika eneo la kimataifa katika Bahari ya Hindi, ambako dawa hizo zimekuwa zikiingizwa kwa meli kubwa, ikiwa ni moja ya mbinu zinazotumiwa na wafanyabiashara.
Alisema kilo 914 za dawa za kulevya aina ya heroin zilikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia uharamia, hali iliyodhihirisha kuwa kasi ya uingizaji wa dawa hizo ni kubwa.
Kwa upande wake, Kamishna wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, alisema tume imekuwa na changamoto kubwa katika kudhibiti wafanyabiashara wa dawa hizo.
Alisema licha ya kudhibiti watu hao, pia imegundulika kuwa bangi imekuwa ikilimwa katika kila mkoa nchini.
Shekiondo alisema kitendo hicho kinahamasisha vijana wengi wa umri mdogo kuanza kuitumia kutokana na kulimwa katika mashamba na nyingine jirani na makazi ya watu.

Jalada la Sugu latinga kwa DPP


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
POLISI mkoani Dodoma imekamilisha upelelezi wa tuhuma zinazomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (CHADEMA), anayetuhumiwa kumtukana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kupitia mtandao wa kijamii.
Imeelezwa jalada limepelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, alisema jana kuwa, polisi imeshakamilisha upelelezi wa tuhuma hizo na jalada kupelekwa kwa DPP.
“Polisi tumeshakamilisha upelelezi na jalada liko kwa DPP kwa hatua zaidi kwa jinsi atakavyoona inafaa,” alisema.
Hata hivyo, alisema Sugu jana aliripoti Kituo Kikuu cha Polisi kama alivyotakiwa kufanya na kwamba, ameongezewa dhamana hadi leo, ambapo anatakiwa kuripoti kituoni.
“Jana alitimiza masharti ya dhamana kwa kuja kuripoti, anaendelea na dhamana hadi kesho, tukisubiri uamuzi wa DPP,” alisema.
Sugu alikamatwa juzi, saa nane mchana, akitoka bungeni, akituhumiwa kumtukana Pinda kwa kutumia mtandao wa kijamii.
Kwa mujibu wa Misime, baada ya kukamatwa, Sugu alifikishwa Kituo Kikuu cha Polisi alikohojiwa kwa takriban saa mbili na nusu.
Mbunge huyo anatuhumiwa kumtukana Waziri Mkuu Pinda kuhusu utendaji wake wa kazi na kumdhalilisha.
Anatuhumiwa kumtusi waziri mkuu kutokana na kauli aliyoitoa hivi karibuni bungeni alipojibu maswali ya papo kwa hapo.
Waziri Mkuu Pinda alivitaka vyombo vya dola, likiwemo Jeshi la Polisi kutowavumilia watu wanaotishia amani na utulivu nchini.
Sugu amedhaminiwa na mbunge mwenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu na mtu mwingine, mkazi wa Dodoma.

Ulinzi mkali ujio wa Rais Obama


NA RABIA BAKARI
JESHI la Polisi limeimarisha ulinzi mara dufu, kutokana na ujio wa wakuu wa nchi zaidi ya 14, walioanza kuingia nchini jana.
Miongoni mwa wakuu hao wa nchi ni Rais wa Marekani, Barack Obama, atakayewasili Jumatatu.
Jeshi hilo pia limepiga marufuku maandamano ya CUF na mengine yaliyoandaliwa kwa siri, yakilenga kusambaza vipeperushi na mabango wakati Rais Obama atakapowasili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema wana taarifa za uhakika kuwa, kuna chama cha siasa na taasisi ambazo zimejiandaa kujitokeza na mabango, kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa usalama.
“Uchunguzi wa hali ya juu unafanyika kuwabaini wahusika. Hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayeleta vurugu wakati wa ugeni huo. Tunawasihi kuwa watiifu wa sheria bila shuruti,” alionya.
Kuhusu maandamano ya CUF, alisema yalilenga kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete. Alisema wamekwisha kujibiwa na Ikulu kwamba, rais hataweza kuonana au kupokea maandamano hayo, kwa kuwa atakuwa na ugeni.
“Maandamano hayo pia yataingilia misafara ya viongozi na wajumbe wao. Barabara wanayotarajia kutumia ipo katika orodha ya zitakazotumika wakati wa ugeni huo mkubwa,” alisema.
Akizungumzia ulinzi, alisema polisi wengi watakuwa barabarani na mitaani na kwamba, jambo hilo ni la kawaida katika kuimarisha usalama kwa kipindi hicho, hivyo wananchi wasiwe na hofu.
“Licha ya ujio wa Obama, tuna wageni mbalimbali watakaoshiriki mkutano wa Smart Partnership utakaoanza keshokutwa.
“Mkutano huu ni wenye manufaa kwa nchi. Tukiachana na upolisi au uandishi wa habari, wote tuungane na kuwa wazalendo kwa matokeo mazuri ya mkutano huo,” alisema.
Alisema baadhi ya nchi zimetuma vikosi vya usalama ambavyo vinashirikiana na jeshi hilo. Alisema ikilazimika watatumia helikopta kuhakikisha amani haivurugiki.
Kova amewaomba wamiliki wa hoteli na magari binafsi au ya umma kuwa waaminifu na wazalendo ili kutangaza sifa nzuri ya taifa. Wametakiwa kulinda mali za wateja wanaotumia huduma zao.
Alisema wanaangalia uwezekano wa kuondoa usumbufu, hususan katika matumizi ya barabara, lakini wananchi wanatakiwa wawe wavumilivu, kwani mahitaji yatakuwa makubwa.
Kamanda Kova alisema elimu ya matumizi ya barabara itatolewa na kila linalowezekana litafanyika ili kuhakikisha matumizi ya barabara hayaleti adha kwa watumiaji.
Alisema wasiokuwa na mambo muhimu ya kufanya mjini, ni vyema wawe watulivu majumbani.

TRA yaboresha mtandao wa kodi


Na Hamis Shimye
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya imeboresha ulipaji kodi kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi.
Uboreshaji huo ni pamoja na kuzindua mtandao utakaosaidia kupatikana kwa taarifa za kodi kwa wananchi na kuunganisha kwa mawasiliano baina ya TRA na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji huo, Mkurugenzi wa Fedha wa TRA, Salehe Mshoro, alisema utasaidia pia mifumo ya kompyuta ya BoT na TRA kuungana.
Mshoro alisema hatua hiyo ni sehemu ya mageuzi mengine katika ulipaji wa kodi, ambapo mfumo huo utaanza kutumika Julai Mosi, mwaka huu kwa wafanyabiashara wakubwa na baadae kwa wafanyabiashara wengine nchini.
Naye, Meneja Mradi huo unaojulikana kana  ‘Revenue Gateway’, Ramadhan Singati, alisema umebuniwa na TRA kwa kushirikiana na BoT.
Alisema nia ni kuongeza uwezo katika ukusanyaji wa taarifa na ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara.
“Hautakuwa na matatizo hata kidogo, kwani ni mfumo bora na una uwezo mkubwa kutokana na aina ya teknolojia iliyopo na ni salama kwa fedha na taarifa,” alisema Singati.
Kwa upande wake, Kamishina wa Upelelezi wa Kodi wa TRA, Lusekelo Mwaseba, alisema wamejipanga kikamilifu na wana vifaa na rasilimali watu ya kutosha kuendesha mitambo hiyo na hakuna hujuma itakayojitokeza.
Alisema mfumo huo ni mzuri na utakuwa na faida kubwa kwa wateja na pia, utasaidia kuwaondolea usumbufu katika ulipaji kodi.

Utekelezaji wa miradi wamleta Obama nchini


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema moja ya sababu ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini ni kutokana na kuvutiwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utawala wa kidemokrasia.
Pia, imesema amelenga kujionea matumizi mazuri ya fedha za misaada zinazotolewa na nchi yake kwa ajili ya kuboresha maendeleo katika sekta mbalimbali nchini, zikiwemo za miundombinu, afya na elimu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Kituo cha Radio Clauds cha jijini Dar es Salaam.
Membe, alisema Rais Obama anakuja nchini kutokana na kuvutiwa na serikali inavyotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia utawala bora na demokrasia, jambo ambalo ni tofauti na mataifa mengine.
Alisema nchi nyingi duniani zinaiangalia Tanzania kama taifa lililopiga hatua katika vigezo vya amani duniani, ukilinganisha na mataifa mengine.
Alisema Tanzania inatumia muda mwingi kushughulikia migogoro ya uvunjifu wa amani katika nchi jirani.
Kwa mujibu wa Membe, licha ya baadhi ya watu kudharau utendendaji wa serikali katika kusimamia utawala wa kidemokrasia, mataifa mbalimbali duniani yanaiangalia kama taifa lililopiga hatua katika Nyanja ya utawala wa kidemokrasia.
Membe alisema katika nchi 54 barani Afrika, Tanzania imepiga hatua kubwa katika vigezo vya amani.
Alisema kidunia inashika nafasi ya 55 ns imeendelea kufuata falsafa za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo.
Alisema hata Rais wa China Xi Jinping aliahidi kuitembelea Tanzania kabla ya kuchaguliwa kuwa rais na alitekeleza ahadi hiyo.
Alisema ziara yake ilikuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ya nchi kwani  alisaini mikataba 18 ya maendeleo pamoja na kutangaza sera ya uchumi ya China na muelekeo wa uhusiano wake na nchi za Afrika.
Wakati huo huo; Waziri Membe amewashauri wananchi kutumia mkutano huo kama fursa ya kujiongezea kipato, hususani kwa wajasiriamali.
Amewataka watafute maeneo na kufanya biashara kama ya vyakula, kwakuwa wageni wanaokuja nchini ni wengi na tayari hoteli na migahawa imeshajaa.
“Na wengine watataka hata kula vyaula vyetu vya asili na kununua vitu mbalimbali, kwa hiyo wajasiriamali wajipange,” alisema Membe.

Mke aua mumewe kwa kumsukuma


NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA
MKAZI wa kijiji cha Iganduka, kilichopo wilayani Mbozi, amekufa baada ya kusukumwa na mke wake na kuangukia kisogo.
Inadaiwa alikuwa na ugomvi na mkewe huyo.
Ugomvi huo unadaiwa kuzuka baada ya mkazi huyo, aliyetajwa kwa jina la Rodrick Mwaipasi (55), kumtuhumu mkewe kuuza madebe mawili ya Karanga, bila ya idhini yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea Juni 24, mwaka huu saa 4:00 usiku, katika hospitali ya misheni Mbozi, ambapo marehemu alipelekwe kupatiwa matibabu.
Athuman alisema mzozo huo wa kifamilia ulizuka baada ya mke wa marehemu, aliyemtaja kuwa Makrina Mateo (42) maarufu kwa jina la Simbowe, kuuza debe hizo za Karanga huku mumewe akiwa hana taarifa.
“Hivyo kulitokea mzozo wa kifamilia baina ya wanandoa hao wawili, ambapo Makrina alimsukuma mumewe ambaye aliangukia kisogo,” alisema Kamanda Athuman.
 Alisema Polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mke huyo wa marehemu na utaratibu unafanywa ili aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma.
Kamanda Athuman, alitoa wito kwa jamii kutatua matatizo ama migogoro yao kwa njia ya mazungumzo, badala ya kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia hasira na nguvu.
Katika tukio lingine, dereva mmoja amekufa papo hapo na abiria wake kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu la mbele upande wa kushoto na kupinduka.
Athuman alisema ajali hiyo ilitokea Juni 25, mwaka huu saa 2:00 asubihi, katika kijiji cha Urunda wilayani Mbarali, ambapo ilihusisha gari lenye namba ya usajili T.545 AUL aina ya Toyota Escudo.
Alimtaja dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo kuwa ni Abinery Chaula (45), mkazi wa Mkombwe – Ubaruku, wilayani humo.
Alisema kufuatia ajali hiyo, dereva alikufa papo hapo na abiria aliyekuwemo ndani ya gari hilo, Johari Uguda (37), anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya misheni Rujewa.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo na uchunguzi zaidi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea.

Kampuni 34 zapigwe ‘stop’ kushiriki zabuni za umma


NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), imezifungia kampuni 34 kwa mwaka mmoja, kutoshiriki zabuni za manunuzi ya umma kwa tuhuma za kufanya udanganyifu.
Zinadaiwa kutotekeleza mikataba yao kwa wakati na kufanya malipo hewa.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA, Jaji Thomas Mihayo, aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, ya kuwajengea uwezo wa kusimamia sheria za ununuzi katika sekta ya umma ya mwaka 2011.
Jaji Mihayo, alisema kati ya hizo, kampuni 24 zilifungiwa kwa kushindwa kutekeleza mikataba na taasisi za umma na nane zilifungiwa kwa ajili ya kulipa malipo kwa kazi ambazo hazikufanyika.
Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Nyegezi J.J. Construction Limited, Muson Engineering Limited na Jossam and Company Ltd.
Alisema zingine tatu zinaendelea kufungiwa mapka hapo zitakaporejesha fedha walizolipwa.
Alizitaja kuwa ni pamoja na kampuni ya Man-Ncheye-Pa-Co, Ltd ya Bunda, Tengo Construction Limited ya Morogoro na Icon Engineers ya Mwanza.
Jaji Mihayo alitoa wito kwa wakurugenzi kutoa taarifa kwa kampuni zilizojiingiza katika udanganyifu au kushindwa kutekeleza mikataba ili nazo zifungiwe.
Alisema ni vyema kusimamia na kuiheshimu sheria ya manunuzi ya umma, ili kulinda fedha za serikali zinazotumika katika ununuzi wa vifaa mbalimbali.
Alisema kwa mujibu wa ripoti ya utendaji ya mwaka 2011/2012 ya PPRA imebaini zaidi ya sh. trillion 4.3 zilitumiwa na taasisi za umma 319 kufanya manunuzi ya kandarasi za ujenzi, vifaa na huduma, kwa mwaka wa fedha 2011/12.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Ramadhani Mlinga, alisema kiwango cha uzingatiaji wa sheria, kimekuwa kikikuwa
kutoka asilimia 39, 2006/2007 mpaka  asilimia 73, 2009/2010.
Hata hivyo, alisema mwaka 2010/2011, kiliporomoka kwa asilimia 68.
Dk. Mlinga, alisema pamoja na mafanikio hayo, PPRA inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kuendeleza utaratibu wa kuzipatia mafunzo taasisi za umma, hususan serikali za mitaa kuhusu sheria, kanuni na utaratibu wa manunuzi ya umma.
Nyingine aliitaja kuwa ni ya kujiimarisha  kimuundo kwa kuajiri watumishi wa
kutosha na wenye ujuzi.
Akizungumzia warsha hiyo, alisema imelenga kuwawezesha wajumbe wa Bodi kuelewa wajibu wao.

Tuesday 25 June 2013

Kampuni za simu zai-beep serikali


Na Hamis Shimye
MSIMAMO wa serikali kuzibana kampuni za simu kulipa kodi ya mapato, umechukua sura mpya, baada ya Umoja wa Wamiliki wa Simu za Mkononi Tanzania (Moat) kutunisha misuli.
Moat imesisitiza uamuzi wa kupandisha gharama za simu kwa watumiaji uko pale pale na kwamba, utaanza Jumatatu ijayo.
Kwa upande wake, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema itatekeleza kwa vitendo uamuzi wa serikali katika ukusanyaji kodi kwenye kampuni hizo, ambazo zinatajwa kupata faida kubwa huku zikilipa kodi kiduchu.
TRA imesema itaanza kazi ya kukusanya kodi kikamilifu Jumatatu, ikiwa ni miongoni mwa mambo yaliyopitishwa na Bunge katika bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/2014.
Akizungumza kwa simu jana, Mkurugenzi wa Huduma za Elimu wa TRA, Richard Kayombo, alisema wao ni watekelezaji wa sheria.
“Jukumu letu ni kukusanya kodi na si vinginevyo, hivyo iwapo serikali na Bunge zimeridhia na kupitisha, hakuna shida kwa upande wetu kwa kuwa ndiyo jukumu letu,’’ alisema.
Alisema TRA kwa sasa haiwezi kusema chochote kwa kuwa bado haijapewa au kutaarifiwa kuhusu kiwango cha kodi cha kukusanya, kwani bajeti ya serikali bado haijaanza kutumika.
“Mwaka wa fedha unaisha Juni 30, mwaka huu, hivyo natarajia Julai Mosi kila kitu kitajulikana,’’ alisema.
Serikali katiba bajeti iliyopitishwa na Bunge juzi, imependekeza kuzitoza kodi kampuni hizo kwa asilimia 14, badala ya asilimia 12 ya awali.
Kwa upande wake, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema haihusiki na kodi, bali utoaji leseni.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema msimamo wa kampuni hizo ni kuongeza gharama kwa watumiaji simu.
Kwa nyakati tofauti, wabunge na serikali wamesema kuongeza gharama za matumizi ya simu kunalenga kuendelea kuwanyonya wananchi.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema juzi kuwa, kampuni hizo zinatumia gharama ndogo kujiendesha, hivyo serikali inatarajia gharama zishuke zaidi na si kuongezeka.
Alisema gharama za uendeshaji za kampuni hizo zimepungua kutokana na kutumia mkongo wa mawasiliano wa taifa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/2014, alisema suala la kampuni za simu kutokulipa kodi stahili limekuwa kilio cha muda mrefu.
Alisema serikali itaanza kuzibana kampuni hizo ili zilipe kodi na mapato stahili, pia kuwashirikisha Watanzania katika umiliki wake.
Katika kufanya hivyo, alisema serikali itaweka mtambo maalumu wa kufuatilia miamala yote ya kampuni hizo na kuziingiza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Pikipiki zageuka chinjachinja


Na Epson Luhwago, Dodoma
AJALI za pikipiki zimeendelea kuwa chanzo cha vifo vya maelfu ya watu nchini, ambapo ndani ya miezi 17 iliyopita zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema bungeni jana kuwa, kuanzia Januari, mwaka jana hadi Mei mwaka huu, watu 1,282 walifariki dunia kutokana na ajali hizo.
Alisema vifo hivyo vilitokana na ajali 8,178 zilizotokea nchi nzima, ambapo Dar es Salaam ndiyo kinara wa matukio hayo kwa kuwa na ajali 3,650.
Kwa mwaka jana, alisema watu 930 walipoteza maisha kutokana na ajali za usafiri huo, na kwa mwaka huu, kuanzia Januari hadi Mei watu 352 walifariki dunia.
“Matukio haya yamesababisha idadi ya vifo na majeruhi kuwa kubwa kiasi cha kuzifanya hospitali nyingi kuanzisha wodi maalumu za majeruhi wa pikipiki,” alisema.
 Dk. Nchimbi alisema matukio hayo ni mengi na ya kutisha, hivyo hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza tatizo hilo.
Kushindwa kufanya hivyo, alisema kutasababisha vifo viendelee na kuongeza idadi ya walemavu, yatima na watu wasiojiweza, ambao wanakuwa tegemezi.
Kwa mujibu wa Dk. Nchimbi, ajali hizo zinasababishwa na waendeshaji kutokujua sheria, kanuni na matumizi ya alama za barabarani, mwendo kasi, kupita taa za kuongozea magari bila kuruhusiwa na kuwadharau askari wa usalama barabarani.
Alisema sababu nyingine ni baadhi ya madereva wa magari makubwa kutokuwaheshimu wenzao wa pikipiki, kutokana na kasumba iliyojengeka miongoni mwao kuwa waendesha vyombo hivyo maarufu bodaboda, hawana nidhamu.

Mitihani TEKU kutokufanyika


NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA

UMOJA wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKUASA), umesema hautatoa mitihani kwa wanafunzi inayotarajia kuanza Jumatatu ijayo, iwapo uongozi wa chuo hautayafanyia kazi madai yao.
Imeelezwa licha ya TEKUASA kuandika barua ya malalamiko kuhusu madai yanayotishia kuporomoka taaluma chuoni hapo, uongozi wa TEKU haujarudisha majibu kwa maandishi.
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Aman Simbeye, alisema hayo jana, alipozungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na wahadhiri wa chuo hicho.
Simbeye akizungumza chuoni hapo, alisema utaratibu wa uendeshaji wa elimu ya juu chuoni hapo unatia shaka.
Alisema licha ya TEKUASA  kuandika barua kwa menejimenti ya chuo ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali, hakuna majibu waliyopatiwa.
Kwa mujibu wa Simbeye, wanafunzi walioghushi vyeti na kufukuzwa wamerejeshwa chuoni kinyemela, kitendo ambacho hawakiafiki.
“Sisi ni jicho na mfano kwa jamii, kamwe hatuwezi kukubali kuona mambo yanaendeshwa kienyeji chuoni hapa, kwani mwisho wa siku chuo kitatoa wanafunzi wasio na sifa na lawama zitaturudia,” alisema.
Alisema wapo wahadhiri waliokwenda kuongeza elimu na wamewasilisha vyeti, lakini uongozi wa TEKU hautaki kuwapandisha madaraja, huku wengine wakishushwa na stahili walizokuwa wakipata zimeondolewa.
Mhadhiri huyo alisema wanashangazwa na uamuzi unaofanywa na menejimenti ya chuo, kwa kuwapandisha vyeo wahadhiri wengine, huku baadhi wakikataliwa.
Kwa mujibu wa Simbeye, kuna wahadhiri wasio na sifa, lakini wameajiriwa, jambo linaloshusha ari ya utendaji wa wahadhiri wengine.
Alisema chuo hicho kwa muda mrefu hakina kitengo cha kusimamia ubora wa elimu inayotolewa, hivyo iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa na serikali, wanaohitimu hawatakuwa na sifa zinazostahili kitaaluma.
Simbeye alisema kuna mwanafunzi ambaye alitakiwa kurudia kozi lakini hakufanya hivyo, na katika hali ya kushangaza amepewa daraja ambalo hakustahili.
Alisema chuo hicho hakina chombo cha kupitisha matokeo ya wanafunzi baada ya kupitiwa na wahadhiri. Kutokana na hilo, alisema matokeo yaliyotangazwa ni batili.
Simbeye alisema jengo la maabara limejengwa chini ya kiwango, hivyo kuwa na nyufa nyingi na halifai kwa matumizi.
“Utawala umekuwa unatumia lugha za vitisho na matusi, kila tunapotaka kupata ufafanuzi wa jambo lolote, hali ambayo inavunja ari ya utendaji,” alisema.
Makamu Mkuu wa chuo, Profesa Tully Kasimoto hakupatikana kuzungumzia madai hayo ya wahadhiri. Ilielezwa kuwa yuko Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa TEKU, Dk. Daniel Mosses, alisema si msemaji wa chuo.

Kapombe huyooo Uholanzi


Kapombe huyooo Uholanzi

NA SOPHIA ASHERY
BEKI wa Simba Shomari Kapombe, anatarajia kwenda Uholanzi kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya FC Twente.
Klabu hiyo yenye maskani katika mji wa Enschede nchini humo, inashiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Eredivisie na ilianzishwa mwaka 1926.
Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala, alisema kwamba, FC Twente iliandika barua kumtaka Kapombe kwenda kufanya majaribio, akifuzu watampa mkataba.
Mtawala alisema, uongozi wa Simba umekubali na beki huyo atakwenda Uholanzi baada ya taratibu za safari kukamilika.
Alisema, Simba ingependa kuona Kapombe anafanikiwa na kusajiliwa kucheza soka Uholanzi.
Alisema, hilo likifanikiwa, itakuwa faraja kwa Simba kupeleka mchezaji kucheza soka ya kulipwa nje ya nchi.
Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992, aliibukia timu ya Polisi Morogoro kabla ya kujiunga na Simba miaka mitatu iliyopita ambako anatarajiwa kumalizia mkataba wake Desemba mwaka huu.
Tovuti ya FC Twente imeripoti kuwa, Kapombe atatua Uholanzi wakati wowote kuanza majaribio hayo.
 Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, klabu hiyo imefurahishwa na Simba kumruhusu beki huyo kufanya majaribio.
Kapombe akifuzu, atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika mashariki ndani ya kikosi hicho cha FC Twente.

Rooney atakiwa Barcelona


MADRID, Hispania
BARCELONA nayo imeingia vitani kuwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Mbali ya Barcelona, Chelsea na Real Madrid zimeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya England.
Barcelona iko tayari kutoa pauni milioni 25 (sawa na sh. Bilioni 62.5) kuwezesha Rooney kutua Nou Camp.
Rooney (27), wiki hii alitarajiwa kufanya mazungumzo na kocha wake David Moyes kuhusu mustakabali wake ndani ya Old Trafford.
Kabla ya kustaafu, Sir Alex Ferguson alisema, Rooney hatauzwa baada ya mshambuliaji huyo kuomba kuondoka Man United.
Vyanzo vya uhakika ndani ya Barcelona vinaeleza kuwa, klabu hiyo inafuatilia mchakato mzima kuhusu nafasi ya Rooney na kama Man United itaamua kumpiga bei, itakuwa tayari kumnyakua.
Mtoa habari mmojawapo alisema: “Rooney ni mshambuliaji ambaye atamudu mfumo unaotumiwa na Barcelona.
“Kwa Barcelona, ulinzi unaanza kuanzia mbele na Rooney anafanya kazi ukilinganisha na wengine.
"Ni mchezaji mzuri ana vigezo vyote. Klabu yake ikimuweka sokoni, Barcelona iko tayari kuwania saini yake.”

Brandts akuna kichwa


NA MWANDISHI WETU
KOCHA mkuu wa Yanga Eenest Brandts, amesema anatarajia kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Brandts alisema mapambano kwa ajili ya msimu huo yatafanyika ili Yanga itetee ubingwa wa Tanzania bara iliyoutwaa msimu uliopita.
Brandts alisema, ratiba ya maandalizi kwa timu yake, itaanza rasmi mwanzoni mwa wiki ijayo kwa mazoezi mepesi kabla ya kuanza kambi.
Alisema, wachezaji wake walipewa mapumziko ya wiki mbili, anaamini wamepumzika vya kutosha hivyo kazi iliyopo mbele yao ni kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.
Alisema wakati kikosi chake kikifanya mazoezi hayo, maandalizi kwa ajili ya kambi ya kudumu kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, yanaendelea na anataka kuona timu inakuwa kambini muda mrefu.
Brandts alisema, anataka wachezaji wake wazoeane ndiyo maana anataka wawe kambini kwa muda mrefu.

JK atua Dodoma leo

RAIS Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda muda mfupi baada ya kuwasili mjini Dodoma leo. JK amewasili mjini hapa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

Wahadhiri TEKU kugoma, mitihani hatihati

NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA
UMOJA wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKUASA), umesema hautatoa mitihani kwa wanafunzi inayotarajia kuanza Jumatatu ijayo, iwapo uongozi wa chuo hautayafanyia kazi madai yao.
Imeelezwa licha ya TEKUASA kuandika barua ya malalamiko kuhusu madai yanayotishia kuporomoka taaluma chuoni hapo, uongozi wa TEKU haujarudisha majibu kwa maandishi.
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Aman Simbeye, alisema hayo jana, alipozungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na wahadhiri wa chuo hicho.
Simbeye akizungumza chuoni hapo, alisema utaratibu wa uendeshaji wa elimu ya juu chuoni hapo unatia shaka.
Alisema licha ya TEKUASA  kuandika barua kwa menejimenti ya chuo ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali, hakuna majibu waliyopatiwa.
Kwa mujibu wa Simbeye, wanafunzi walioghushi vyeti na kufukuzwa wamerejeshwa chuoni kinyemela, kitendo ambacho hawakiafiki.
“Sisi ni jicho na mfano kwa jamii, kamwe hatuwezi kukubali kuona mambo yanaendeshwa kienyeji chuoni hapa, kwani mwisho wa siku chuo kitatoa wanafunzi wasio na sifa na lawama zitaturudia,” alisema.
Alisema wapo wahadhiri waliokwenda kuongeza elimu na wamewasilisha vyeti, lakini uongozi wa TEKU hautaki kuwapandisha madaraja, huku wengine wakishushwa na stahili walizokuwa wakipata zimeondolewa.
Mhadhiri huyo alisema wanashangazwa na uamuzi unaofanywa na menejimenti ya chuo, kwa kuwapandisha vyeo wahadhiri wengine, huku baadhi wakikataliwa.
Kwa mujibu wa Simbeye, kuna wahadhiri wasio na sifa, lakini wameajiriwa, jambo linaloshusha ari ya utendaji wa wahadhiri wengine.
Alisema chuo hicho kwa muda mrefu hakina kitengo cha kusimamia ubora wa elimu inayotolewa, hivyo iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa na serikali, wanaohitimu hawatakuwa na sifa zinazostahili kitaaluma.
Simbeye alisema kuna mwanafunzi ambaye alitakiwa kurudia kozi lakini hakufanya hivyo, na katika hali ya kushangaza amepewa daraja ambalo hakustahili.
Alisema chuo hicho hakina chombo cha kupitisha matokeo ya wanafunzi baada ya kupitiwa na wahadhiri. Kutokana na hilo, alisema matokeo yaliyotangazwa ni batili.
Simbeye alisema jengo la maabara limejengwa chini ya kiwango, hivyo kuwa na nyufa nyingi na halifai kwa matumizi.
“Utawala umekuwa unatumia lugha za vitisho na matusi, kila tunapotaka kupata ufafanuzi wa jambo lolote, hali ambayo inavunja ari ya utendaji,” alisema.
Makamu Mkuu wa chuo, Profesa Tully Kasimoto hakupatikana kuzungumzia madai hayo ya wahadhiri. Ilielezwa kuwa yuko Dar es Salaam. Kaimu Makamu Mkuu wa TEKU, Dk. Daniel Mosses, alisema si msemaji wa chuo.

Sugu mbaroni kwa kumtukana Pinda


Na Theodos Mgomba, Dodoma
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kumtusi Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika mtandao wa kijamii.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana kuwa, mbunge huyo wa CHADEMA alikamatwa saa nane mchana akitoka bungeni na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi, ambako alihojiwa kwa saa mbili na nusu.
Alisema Sugu alikamatwa baada ya kunaswa akimtukana waziri mkuu kuhusu utendaji wake wa kazi.
Mbunge huyo anatuhumiwa kumtusi waziri mkuu kutokana na kauli aliyoitoa hivi karibuni bungeni wakati wa maswali ya papo kwa hapo.
Pinda alivitaka vyombo vya dola, likiwemo Jeshi la Polisi kutowavumilia watu wanaotishia amani na utulivu nchini.
Kamanda alisema Sugu alidhaminiwa saa 10.30 jioni na mbunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu na mwalimu wa Shule ya Sekondari Viwandani.
Alisema mbunge huyo ametakiwa kufika tena polisi kesho saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa.
Misime alisema polisi itaendelea kuchukua hatua kwa kadri itakavyoona inafaa, ikiwemo kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema polisi haitasita kumkamata mtu yeyote anayepandikiza mbegu za chuki, zinazoweza kusababisha kuvunjika amani na utulivu nchini.
Kamanda amewataka wanaotumia mitandao hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Hivi sasa kumezuka tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia mitandao ya kijamii kuwachafua viongozi wa serikali, hivyo kujenga chuki kati ya wananchi, serikali na viongozi.

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO


SIMU ZISIZOSAJILIWA MWISHO JULAI 10
SERIKALI inatarajia kuzima simu zote za mkononi ambazo hazijasajiliwa Julai 10, mwaka huu.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema hayo jana, alipojibu swali la Dk. Getrude Rwakatare (Viti Maalumu -CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu baadhi ya watu ambao wanatumia simu za mkononi kusambaza ujumbe wa uzushi kwa wengine.
January alisema hatua hiyo ni moja ya mikakati ya serikali katika kudhibiti matumizi mabaya ya simu za mkononi.
Alisema serikali imeondoa muda wa siku 30 zilizowekwa kwa ajili ya mnunuzi kutumia simu kabla ya kusajiliwa.
Naibu waziri alisema namba za simu 24,4036,999 zimesajiliwa na serikali.
Kwa mujibu wa January, usajili wa simu unalenga kupunguza matumizi mabaya yaliyoanza kujitokeza.
Alisema licha ya kuzisajili, serikali imekumbana na changamoto mbalimbali za matumizi mabaya ya simu.
Baadhi ya changamoto hizo alisema ni mawakala kusajili simu bila kutumia vitambulisho au majina halisi ya watumiaji.

HALMASHAURI ZAONYWA MADENI YA WALIMU
OFISI ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, imetoa maelekezo kwa wakurugenzi wa halmashauri kutosababisha madeni ya walimu.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Kassim Majaliwa, alitoa maelekezo hayo alipojibu swali la Meshack Opolukwa (Meatu -CHADEMA).
Opolukwa alitaka kujua ni lini serikali itaondoa tatizo la walimu Meatu la kuchelewesha kupandishwa madaraja na kutolipwa stahili zao.
Majaliwa alisema serikali imedhamiria kuondoa tatizo la walimu kuchelewa kupandishwa madaraja na kulipwa stahili zao, ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha mfumo wa taarifa za watumishi.
Alisema ili kuepuka madeni, halmashauri zimetakiwa kutenga fedha za kuwapandisha madaraja watumishi, wakiwemo walimu na kuhakikisha marekebisho ya mishahara yanalipwa kwa wakati.
Naibu waziri alisema katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 serikali imetenga nafasi za kuwapandisha vyeo walimu 39,602 walio katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kwamba, sh. milioni 64 zimetengwa.
Majaliwa alisema fedha hizo zimetengwa kupandisha madaraja walimu 330 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Katika mfumo huo, alisema serikali inaweka utaratibu wa kiutumishi wa kushughulikia malimbikizo ya mishahara, uhamisho, ukomo wa watumishi na marekebisho ya taarifa za mtumishi.
Alisema serikali imeunda kamati ya kuchambua na kutoa mwongozo kwa ajili ya kushughulikia changamoto ya upandishwaji madaraja walimu.
Kamati hiyo alisema itawasilisha  mapendekezo katika Baraza la Majadiliano ya Pamoja katika sekta ya elimu.

Taasisi za Tanzania zabeba tuzo tatu Ghana


NA MWANDISHI WETU
TANZANIA imeshinda tuzo tatu za juu za ubunifu katika Utumishi wa Umma, barani Afrika, kufuatia taasisi zake tatu kushinda nafasi ya kwanza na kunyakua vikombe vya ushindi.
Vikombe hivyo vimekabidhiwa na Rais wa Ghana, John Mahama wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Afrika, yaliyofanyika mjini Accra.
Taasisi za Tanzania zilizoshinda ni Ofisi ya  Ukaguzi ya Taifa, (NAO), Wakala wa Vipimo, (WMA) na Wakala wa Vitambulisho vya Taifa, (NIDA), ambapo zilifanya vizuri kwenye maonyesho ya  siku 7 ya shughuli za utumishi wa umma yaliyofikia kilele mwishoni mwa wiki.
Akizungumzia ushindi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, alisema Tanzania ilistahili ushindi kutokana na taasisi zilizoshiriki kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Pia, alisema amefarijika kwa taasisi hizo kupata ushindi mkubwa katika maonyesho hayo, ambapo taasisi 42 kutoka Tanzania zilishiri.
Katika hotuba yake Celina, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi Afrika, aliwataka watumishi wa umma kuwatumikia wananchi kwa bidii, unyenyekevu, uadilifu na kueleza utumishi wa umma ni kuwatumikia watu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi, amekiri kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri katika maonyesho hayo Afrika

KAMPUNI ZA SIMU ZAITUNISHIA MISULI SERIKALI


KAMPUNI za simu za mkononi nchini zimeitunishia misuli serikali kwa kusema kuwa, msimamo wao wa kuongeza gharama za huduma za kupiga simu kwa wateja upo pale pale na utaanza Julai Mosi, mwaka huu, kama walivyoapanga.
Habari zilizoifikia blog hii hivi punde zinasema kuwa uamuzi uliotolewa na serikali kutaka kampuni hizo kutoongeza gharama za huduma za simu kwa wateja wao kutokana na kushuka kwa gharama za uendeshaji, umekataliwa na kampuni hizo. HABARI ZAIDI SOMO UHURU KESHO

MKURABITA yaonyesha njia ya maisha bora

na mwandishi wetu
MPANGO wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge nchini (MKURABITA), umeendelea kuwa mkombozi wa watanzania katika kufikia Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.
Hatua hiyo imetokana na kuendelea kugawa hati miliki za kimila kwa wananchi mbalimbali nchini ikiwa ni kuwawezesha kupata fursa za mikopo kwa kutumia rasilimali walizonazo.
Mratibu wa MKURABITA Seraphia Mgembe, alisema hayo juzi wakati akitoa tathimini ya kazi ya kutoa hatimiliki hizo kwa wakulima wa chai katika wilaya za Mbinga, Mufindi na Njombe.
Kazi ya kutoa hatimiliki hizo ni mwendelezo katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wiki mbili zilizopita wananchi wa wilaya ya Rungwe walikabidhiwa hati miliki za kimila.
Alisema maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezi kupatikana kwa wananchi kukaa vijiweni ama kubweteka bila kufanya kazi na kusubiri serikali kufanya kila kitu.
Seraphia alisema jukumu la serikali ni kujenga mazingira bora kwa wananchi kuzalisha mali ikiwa ni pamoja na kutumia vizuri rasilimali walizonazo kama dhamana ya kupata mitaji.
“Tunaendelea kutoa hati miliki za kimila ili kuwezesha wananchi kupata mitaji kwa kutumia rasilimali walizonazo. Kazi inayoafuata ni kuendelea kuwajengea uwezo na jinsi ya kuzitumia kama dhamana,” alisema.
Alisema maendeleo ya kweli na ya haraka ni yale yanayotokana na matumizi ya rasilimali zinazowaunganisha wananchi na MKURABITA imekuwa kiunganishi muhimu baina yao na taasisi za fedha nchini.
Katika hatua nyingine, wakuu wa wilaya za Njombe, Sarah Dumba na Mufindi, Evarista Kalalu, waliipongeza MKURABITA kutokana na jitihada za kuhakikisha wakulima wa chai wanayamiliki rasmi mashamba ili kuwakomboa na umasikini.
Walisema kuwa awali wakulima hao walikuwa na utajiri, ambao haukuwafainisha zaidi ya kulima na kuuza mazao yao, lakini kwa sasa watakuwa wamiliki na pia watatumia hati miliki zao kukopa fedha kwenye taasisi za fedha. Jumla ya hatimiliki za kimila zimetolewa kwa wakulima wa chai.
MKUU wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya kimila, mkazi wa kijiji cha Iwafi, Everina Jonas, wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe. Katikati ni Mratibu wa MKURABITA, Seraphia Mgembe. (Picha kwa hisani ya PPRA).

WANANCHI wakifurahi kukagawiwa hati miliki za kimila kutoka kwa mmoja wa maofisa wa MKURABITA

Carlo Ancelotti abeba mikoba ya Special One

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa PSG, Mtaliano Carlo Ancelotti ametangazwa rasmi kuwa kocha wa Real Madrid kuchukua mikoba ya Jose Mourihno aliyejirudisha Chelsea. Ancelotti aliyewahi kutamba na AC Milan kabla ya kutimuliwa Chelsea, ametangazwa rasmi jana. Nafasi yake PSG imechukuliwa na mlinzi wa zamani wa Man Utd, Laurent Blanc.
                                          Carlo Ancelotti

Kampuni za simu zashushiwa rungu


Na waandishi wetu, Dar na Dodoma
SERIKALI imesema itaanza kuzibana kampuni za simu ili zilipe kodi na mapato stahili, pia kuwashirikisha Watanzania katika umiliki wake.
Katika kufanya hivyo, imesema itaweka mtambo maalumu wa kufuatilia miamala yote ya kampuni hizo na kuziingiza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Serikali imesema kamwe gharama za huduma za simu hazitaongezwa, kwa kuwa kuziongeza ni kuwanyonya Watanzania, kwani gharama za uendeshaji zimeshuka kwa kiwango kikubwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/2014, alisema suala la kampuni za simu kutokulipa kodi stahili limekuwa kilio cha muda mrefu.
Alisema ili kuhakikisha serikali inapata mapato hayo, kampuni hizo kuanzia mwaka ujao wa fedha zitawekewa mtambo maalumu utakaofuatilia miamala na viwango vyote vinavyotozwa na kampuni hizo.
Kwa mujibu wa Janet, mtambo huo maalumu utakuwa ukisimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Mtambo huu utasaidia kudhibiti wizi wa aina yoyote na kubaini miamala ya fedha ndani ya kampuni hizo, pia kutambua kama kuna udanganyifu wowote unaofanywa,” alisema.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema serikali imeanzisha vikosi kazi kwa ajili ya kuzifuatilia kampuni hizo ili kuhakikisha zinaingizwa kwenye orodha ya kampuni zilizoko DSE.
Saada alisema vikosi kazi hivyo vinatokana na sheria mpya inayolenga kuzidhibiti kampuni hizo na vitakuwa chini ya TCRA na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kudhibiti kampuni za madini nazo kuingia katika soko la hisa.
Alisema Kampuni ya Airtel imeorodheshwa kwenye soko hilo pamoja na zingine za sukari za Kilombero na Mtibwa, Saruji Mbeya, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Kampuni ya Mabati ya ALAF Limited na kampuni ya vyombo vya umeme ya TANELEC.
Kampuni hizo zinaungana na Benki ya NMB, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TOL Gases Limited, Swissport, Saruji Tanga na CRDB.
“Kuingia kwa kampuni hizo katika soko la hisa, kutawawezesha Watanzania kupata fursa katika umiliki na kuendesha uchumi wa nchi.
Wabunge waliochangia bajeti walisema serikali imekuwa ikikosa mabilioni ya shilingi kwa mwaka kutokana na kampuni za simu kutokulipa fedha kupitia huduma mbalimbali zinazotoa kwa wateja.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema kampuni hizo zinatumia gharama ndogo kujiendesha hivyo, gharama kwa watumiaji zinapaswa kupungua zaidi na si kuongezeka.
Alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuangalia gharama za uwekezaji katika kampuni hizo ili iweze kukusanya kodi inayostahili, kwa kuwa kuna udanganyifu mkubwa.
"Tusingependa wananchi waathirike wala kubebeshwa mzigo wa gharama, kampuni hizi zinatumia gharama ndogo kujiendesha kwa kutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano," alisema.
Alisema kampuni hizo zimevunja  sheria ya soko huria kwa kukutana na kupanga kupandisha gharama kinyume cha sheria.
"Hairuhusiwi kisheria kampuni zinazofanya biashara moja kukaa na kukubaliana kupandisha gharama, huo si ushindani na suala hili halikubaliki,” alisema.
Kampuni hizo kupitia Chama cha Wamiliki wa Simu za Mkononi Tanzania (MOAT), zimetangaza gharama za matumizi ya simu zitapanda kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
Hatua hiyo imeelezwa huenda  inatokana na serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 kueleza itazitoza kodi kwa asilimia 14.

Wafanyakazi 15 TRA wachunguzwa

Na Epson Luhwago, Dodoma
BUNGE limepitisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/2014, ambayo itatumia sh. trilioni 18.2 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. 
Bajeti hiyo ilipitishwa jana kwa wabunge kupiga kura kukubali au kuikataa. Jumla ya wabunge 270 walikuwepo wakati wa kupiga kura, ambapo kura za NDIYO zilikuwa 235 na za HAPANA 35.
Wabunge wote wa CCM waliokuwepo waliikubali, huku wapinzani wakiikataa. CHADEMA hawakupiga kura kwa madai hawakushiriki kuijadili.
Hata hivyo, mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), kama ilivyo ada, aliikubali. Alisema anaiunga mkono tangu alipokuwa akiijadili. Kila mwaka amekuwa akiunga mkono bajeti ya serikali.
Licha ya upigaji kura ambao ni hatua ya mwisho, wabunge walijadili kwa siku nne mfululizo na kutoa hoja mbalimbali. Wabunge 119 walichangia kwa kusema na wengine 36 kwa maandishi.
Awali, akijibu hoja za wabunge waliochangia, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema bajeti iliyopitishwa imekidhi vigezo na kujibu maswali muhimu ambayo wataalamu wa bajeti wanataka yazingatiwe.  Vigezo hivyo, kwa mujibu wa Waziri Mgimwa ni kuleta unafuu kwa wananchi, kiwango cha upunguzaji umasikini, kutambua umuhimu wa makundi yaliyosetwa kama wanawake na vijana, na kutambua vipaumbele muhimu.
“Bajeti hii imekidhi mambo hayo muhimu kwa sababu imetoa majibu kwa kuweka kipaumbele kwenye uwekezaji wa mambo muhimu ya kiuchumi. Mfano ni kutengwa kwa sh. trilioni 1.2 kwa ajili ya miundombinu ya barabara, umeme na usafirishaji ili kuchochea uzalishaji nchini,” alisema.
Katika kudhihirisha bajeti inajali maisha ya wananchi, Dk. Mgimwa alisema serikali imejikita katika kutatua kero za maji, umeme, pembejeo za kilimo na umeme vijijini.
Alisema umeme vijijini pekee umetengewa sh. bilioni 186 ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo yapate nishati hiyo na maji yametengewa sh. bilioni 184.5.
Maeneo mengine yaliyopewa kipaumbele kwa kuongezewa bajeti na kiasi katika mabano ni uwekezaji maeneo maalumu -EPZ (sh. bilioni 30), usafirishaji (sh. bilioni 30), mifugo (sh. bilioni 20) na mfuko wa mbolea (sh. bilioni 21.5).
Kuhusu hoja ya kukusanya kodi kutoka kampuni za madini, alisema zimekuwa zikikusanywa na juhudi zinafanywa ili kuzibana ziweze kulipa kodi zaidi kutokana na fedha zinazopata.
Alisema kampuni hizo zimekuwa zikilipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kampuni, maendeleo ya elimu, ushuru wa stempu na kodi za mapato.
Dk. Mgimwa alitoa takwimu za kodi zinazolipwa kwa miaka mitano katika mabano kuwa, 2007/08 (sh. bilioni 69.5), mwaka 2009/10 (sh. bilioni 66.6), 2010/11 (sh. bilioni 85.5), 2011/11 (sh. bilioni 119), 2011/2012 (sh. bilioni 274.8) na kwa mwaka 2012/13 hadi kufikia Machi mwaka huu zilikusanywa sh. bilioni 251.8.
“Kwa miaka yote hiyo mitano, serikali imekusanya sh. bilioni 867.38 kutoka kwa kampuni za Bulyanhulu, North Mara, Pangea, Resolute, Tanzanite One na Williamson Diamond,” alisema. 
Kwa kampuni zinazofanya utafiti na utafutaji wa mafuta na gesi, alisema haziwezi kutozwa kodi kwa kuwa hazijaingizwa katika utaratibu huo, kwani hazijaanza kuzalisha.
Hata  hivyo, Dk. Mgimwa aliwaondoa hofu juu ya kasi ya kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 19.8 hadi asilimia 8.4 kwa kusema ni takwimu ni za kweli.
Alisema hatua hiyo imetokana na kudhibiti uhaba wa chakula na mafuta, ambavyo ndivyo chanzo kikuu cha kupanda kwa mfumuko wa bei. Pia alisema hatua hiyo ilitokana na kupunguzwa kwa ushuru wa bidhaa za mafuta na kuwabana waliokuwa wakichakachua.
Waziri alisema kodi ya mapato kwa wafanyakazi iliyopendekezwa kupunguzwa hadi asilimia 10 kutoka asilimia 13 iliyopendekezwa na serikali itabaki kama ilivyo. Aliahidi kuwa kodi hiyo itapunguzwa mwaka hadi mwaka.
Katika harakati za kupunguza matumizi makubwa yasiyo na tija,  alisema serikali imekubali hoja za wabunge na kwamba kuanzia mwaka ujao wa fedha magari yatanunuliwa kwa mfumo wa jumla. Pia alisema serikali itapunguza misamaha ya kodi kwa maeneo yasiyo na tija.
Alisema serikali inakusudia kubadilisha sheria ya ununuzi wa umma ili kuwabana wanaonufaika na mfumo wa sasa na kuigharimu serikali fedha nyingi katika eneo hilo.

WAFUTWA KAZI TRA
Katika hatua nyingine, wafanyakazi 15 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamefukuzwa kazi katika miaka mitatu iliyopita kwa kujihusisha na njama za kuikosesha serikali mapato.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, alisema hayo bungeni jana, alipojibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2013/2014.
Alisema wafanyakazi hao walifukuzwa kazi kutokana na  kushirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi, hivyo kuifanya serikali kukosa mapato yanayostahili.
Kwa mujibu wa Janet, wafanyakazi hao wamefukuzwa kazi kati ya mwaka 2010 na Mei, mwaka huu, katika sehemu mbalimbali ikiwemo, Dar es Salaam.
Kuhusu kuhamishwa kwa maofisa waliotuhumiwa kuhusika na wizi wa makontena bandarini, alisema hatua hiyo imefanyika ili kutoa nafasi kwa uchunguzi unaoendelea.
“Huo ni utaratibu wa kawaida wa TRA kwa kuwa huwezi kumwacha mtuhumiwa katika kituo chake cha kazi wakati uchunguzi unafanyika. Baada ya kukamilika uchunguzi hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria zitachukuliwa,” alisema.
Naibu waziri alisema utoroshaji wa makontena bandarini, ulifanywa na maofisa wa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na mawakala wa forodha wasio waaminifu. Alisema mawakala hao watachukuliwa hatua kulingana na ripoti ya uchunguzi itakayotolewa.
Alikiri rushwa imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa serikali kukosa mapato ndani ya TRA na kutokana na hilo, mamlaka imeanzisha mkakati wa kupambana na rushwa, ambao umesaidia kubaini wahusika na kuwachukulia hatua.
Ili kuhakikisha wafanyakazi wanaoajiriwa wanakuwa waadilifu, alisema hivi sasa TRA imekuwa ikiwafanyia uchunguzi kupitia vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya mamlaka. 
MADUKA YAFUTIWA LESENI
Wakati huo huo, maduka 17 ya kubadilishia fedha yamefutiwa leseni kutokana na kukiuka sheria na masharti ya uendeshaji wa shughuli, imefahamika.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema bungeni jana kuwa, maduka hayo yamechukuliwa hatua baada ya kubainika yalikuwa yakiendesha shughuli kinyume cha utaratibu.
Alisema maduka mengine matano yamefungiwa kwa muda, 33 yametozwa faini na mengine 103 yamepewa onyo kali kutokana na makosa yaliyofanywa kutokuwa makubwa.
Saada alisema hatua hiyo iliyochukuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambayo ndiyo msimamizi wa maduka hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Kubadilisha Fedha.
Alisema moja ya makosa yaliyofanywa na maduka hayo ni kutokufanya biashara inayozidi dola 10,000 (zaidi ya sh. milioni 160) kwa siku kwa duka moja.
“Hiki ndicho kiwango cha juu kwa bureau de change (duka la kubadilisha fedha). Kiasi kinachozidi hapo ni lazima kiombewe kibali, vinginevyo hatua zinaweza kuchukuliwa,” alisema.
Alisema kwa sasa, ili maduka hayo yaweze kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, masharti makali yamewekwa, ikiwemo ya kusajiliwa kama kampuni.
Sharti la pili kwa mujibu wa Saada ni wamiliki lazima wawe Watanzania na la tatu ni kutofanya biashara nyingine nje ya kubalisha fedha.

Gharama huduma za simu



Na waandishi wetu, Dar na Dodoma

SERIKALI imesema itaanza kuzibana kampuni za simu ili zilipe kodi na mapato stahili, pia kuwashirikisha Watanzania katika umiliki wake.

Katika kufanya hivyo, imesema itaweka mtambo maalumu wa kufuatilia miamala yote ya kampuni hizo na kuziingiza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
    
Serikali imesema kamwe gharama za huduma za simu hazitaongezwa, kwa kuwa kuziongeza ni kuwanyonya Watanzania, kwani gharama za uendeshaji zimeshuka kwa kiwango kikubwa.

Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2013/2014, alisema suala la kampuni za simu kutokulipa kodi stahili limekuwa kilio cha muda mrefu.

Alisema ili kuhakikisha serikali inapata mapato hayo, kampuni hizo kuanzia mwaka ujao wa fedha zitawekewa mtambo maalumu utakaofuatilia miamala na viwango vyote vinavyotozwa na kampuni hizo. 

Kwa mujibu wa Janet, mtambo huo maalumu utakuwa ukisimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Mtambo huu utasaidia kudhibiti wizi wa aina yoyote na kubaini miamala ya fedha ndani ya kampuni hizo, pia kutambua kama kuna udanganyifu wowote unaofanywa,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema serikali imeanzisha vikosi kazi kwa ajili ya kuzifuatilia kampuni hizo ili kuhakikisha zinaingizwa kwenye orodha ya kampuni zilizoko DSE.

Saada alisema vikosi kazi hivyo vinatokana na sheria mpya inayolenga kuzidhibiti kampuni hizo na vitakuwa chini ya TCRA na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kudhibiti kampuni za madini nazo kuingia katika soko la hisa. 

Alisema Kampuni ya Airtel imeorodheshwa kwenye soko hilo pamoja na zingine za sukari za Kilombero na Mtibwa, Saruji Mbeya, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Kampuni ya Mabati ya ALAF Limited na kampuni ya vyombo vya umeme ya TANELEC.

Kampuni hizo zinaungana na Benki ya NMB, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TOL Gases Limited, Swissport, Saruji Tanga na CRDB.

“Kuingia kwa kampuni hizo katika soko la hisa, kutawawezesha Watanzania kupata fursa katika umiliki na kuendesha uchumi wa nchi.

Wabunge waliochangia bajeti walisema serikali imekuwa ikikosa mabilioni ya shilingi kwa mwaka kutokana na kampuni za simu kutokulipa fedha kupitia huduma mbalimbali zinazotoa kwa wateja.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema kampuni hizo zinatumia gharama ndogo kujiendesha hivyo, gharama kwa watumiaji zinapaswa kupungua zaidi na si kuongezeka.

Alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuangalia gharama za uwekezaji katika kampuni hizo ili iweze kukusanya kodi inayostahili, kwa kuwa kuna udanganyifu mkubwa.

“Tusingependa wananchi waathirike wala kubebeshwa mzigo wa gharama, kampuni hizi zinatumia gharama ndogo kujiendesha kwa kutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano,” alisema.

Alisema kampuni hizo zimevunja  sheria ya soko huria kwa kukutana na kupanga kupandisha gharama kinyume cha sheria.

“Hairuhusiwi kisheria kampuni zinazofanya biashara moja kukaa na kukubaliana kupandisha gharama, huo si ushindani na suala hili halikubaliki,” alisema.

Kampuni hizo kupitia Chama cha Wamiliki wa Simu za Mkononi Tanzania (MOAT), zimetangaza gharama za matumizi ya simu zitapanda kuanzia Julai Mosi, mwaka huu. 

Hatua hiyo imeelezwa huenda  inatokana na serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 kueleza itazitoza kodi kwa asilimia 14.