KUNDI la tembo wapatao 46 kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wamevamia makazi ya watu na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao na vyakula vilivyokuwa vimehifadhiwa katika kijiji cha Mwachumu kata ya Girya, wilayani Bariadi.
Diwani wa kata hiyo, Safari Lewa, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10:00 jioni.
Alisema tembo hao wameharibu mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na pamba katika mashamba ya wananchi.
Lewa, alisema zaidi ya hekari 60 za mazao ya mahindi na pamba zimeharibiwa vibaya na wakazi wa kijiji hicho wanahofia kushambuliwa na tembo hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Abdallah, alikiri wanyama hao kuvamia maeneo hayo.
Alitoa rai kwa wakazi na viongozi wa maeneo hayo kutoa taarifa mapema pindi wawaona tena ili hatua za kuwarudisha hifadhini zichukuliwe haraka
Wednesday, 16 April 2014
Tembo wazusha balaaNa Chibura Makorongo, Bariadi
02:27
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru