NA RABIA BAKARI
BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imejidhatiti kuendelea kutoa huduma za kisasa kwa mfumo wa teknolojia.
Pia, imesema imepata mafanikio kwa kuongezeka mapato kutoka bilioni 31 hadi kufikia bilioni 38 kwa mwaka jana.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPB, Sabasaba Moshingi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam kuhusu mafanikio na changamoto za uendeshaji wa benki hiyo.
Alisema mpaka sasa kuna huduma mbalimbali za kielektroniki, ikiwemo ya huduma za fedha kwa mtandao, pamoja na huduma ya TPB Popote, na mwaka huu kunamipango madhubuti ya kuiboresha.
Alisema benki hiyo ina wateja zaidi ya 670,000, ikiwa ni ongezeko la wateja 70,000 kutoka mwaka jana mpaka mwaka huu.
Kwa upande wa faida, Moshingi alisema TPB imepata sh. bilioni 6.99 ambazo ni kodi kutoka bilioni 5.6, mwaka juzi.
Aliongeza kuwa, mapato kwa ujumla yameongezeka na kufikia sh. bilioni 38.8 mwaka huu kutoka sh. bilioni 31 mwaka jana, sawa na ukuaji wa asilimia 24.
Alisema amana za wateja ziliongezeka na kufikia bilioni 170 kutoka bilioni 138 kwa mwaka 2012 sawa na asilimia 22.
Pia alisema faida iliyotokana na mikopo imeongezeka hadi kufikia bilioni 119.7 kutoka bilioni 100.8 sawa na ongezeko la asilimia 18.7
Wednesday, 16 April 2014
TPB yajidhatiti kutoa huduma bora
02:21
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru