NA MUSSA YUSUPH,
SERIKALI imepiga marufuku Wakala wa Huduma za Ajira kuajiri na kukodisha wafanyakazi kwa niaba ya kampuni zingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Pia, imewataka wakala wa kampuni hizo zilizokuwa katika utaratibu huo, ziwahamishie wafanyakazi husika kwa kampuni zilizowakodisha na kuwasilisha maombi ya usajiri wa uwakala kwa kamishna wa kazi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Kamishana wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela alisema kutokana na agizo hilo, wameanza kufuatilia utekelezaji wake.
"Serikali itaanza ufuatiliaji, ukaguzi na kutoa uamuzi sahihi kuhusiana na utoaji vibali vya uendeshaji wa huduma za ajira nchini. Baadhi ya wakala wameanza kusitisha kukodisha wafanyakazi,''alisema.
Alisema hilo linafanywa na wakala hao, ikiwa ni pamoja na kuhamishia ajira za wafanyakazi hao kwa kampuni husika kwa kuzingatia Sheria ya Kukuza Huduma za Ajira namba tisa ya mwaka 1999.
Hata hivyo, Kinemela alisema tayari serikali imeanza kupokea maombi mapya 56 kwa ajili ya kutaka kutoa huduma za maombi ya ajira, lakini bado hayajajibiwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru