Na Happiness Mtweve,Dodoma
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage, amesema haridhishwi na utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini.
Mwijage, ambaye alikaa ofisini kwa siku tatu baada ya kuteuliwa, alisema hayo jana wakati akijibu maswali ya nyongeza ya mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby.
Alisema mpaka sasa utekelezaji wa usambazaji umeme katika mkoa wa Manyara ni asilimia sita, Pwani asilimia 22 na Kagera asilimia 52, kasi ambayo bado ni ndogo.
Mwijage alisema atawasilisha taarifa hizo kwa aliyemteua iwapo REA hawatatambua majukumu yao na kuyatekeleza kwa wakati.
Katika maswali yake, Shabiby alitaka kujua kama waziri yuko tayari kuambatana naye jimboni kwake akiwa na watendaji wa REA na TANESCO ili kuona kazi inavyoendelea.
Mbunge huyo pia alitaka kujua hatua zitakazochukuliwa kwa wataalamu wa wizara, ambao wamekuwa na tabia ya kuwapa mawaziri taarifa za uongo na hivyo kutoa majibu ya uongo endapo watadhibitika.
Thursday, 29 January 2015
Mwijage: Siridhishwi na mradi wa usambazaji umeme vijijini
06:36
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru