NA CECILIA JEREMIAH
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama kwa kuanza kuwanadi wagombea kinyume cha kanuni zilizopo.
Viongozi walionywa na UVCCM ni Wenyeviti, Makatibu, Madiwani na wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakitumika kuwanadi wagombea hao kinyume cha taratibu na kanuni za Chama.
Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, Paul Makonda, alisema viongozi hao wamekuwa wakifanya kampeni kabla ya muda haujafika, hivyo wanatakiwa kuacha vitendo hivyo na badala yake wanapaswa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo.
“Kamati ya maadili ya CCM ina wajibu wa kutafsiri hasira ya wana-CCM na viongozi wao kwa vitendo ikiwemo kufuatilia suala hilo na kuwachukulia hatua endapo wakibainika kuhusika na vitendo hivyo,’’alisema.Aliseam UVCCM inawataka wale wote walioanza kampeni za urais, ubunge na udiwani, waachane na vitendo kwa kuwa muda haujafika.
Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, alioa taarifa ya kulaani vitendo vya baadhi ya viongozi ndani ya Chama kuanza kampeni za urais kabla ya wakati.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru