NA EMMANUEL MOHAMED
CHUO Kikuu Kishiriki cha Elimu,(DUCE), kimeanza mkakati wa kupunguza uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi nchini kwa kuongeza udahili wa wanafunzi
wa masomo hayo.
Mkakati huo umeongeza wadahiliwa 1700 wa masomo hayo kwa mwaka huu,
katika chuo hicho, huku kukiwa na jumla ya walimu 20,000 wa masomo hayo nchi
nzima.
Hayo yalielezwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (UDSM),
Profesa Rwekaza Mukandala, jana , wakati akiwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa
kwanza DUCE.
Profesa Mukandala alisema mkakati huo umeanza vizuri, kwani serikali
imeanza kuboresha miundombinu ya Mfumo wa Habari na Mawasiliano, (TEHAMA) kwa
lengo la kuongeza maarifa ya ziada kwa masomo hayo kwa wanafunzi.
Alisema juhudi za serikali na DUCE
imefanikiwa kujenga maabara kubwa tatu za sayansi, ili kuongeza uwezo wa
mkakati huo wa kupokea wanafunzi wengi zaidi wa masomo hayo ya sayansi.
“Tuliomba kuongezewa idadi ya wadahiliwa wa masomo ya sayansi kwa Taasisi ya Usajili wa Vyuo Vikuu, (TCU), kwa mwaka huu na walituunga mkono katika juhudi za mkakati huo,” alisema.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Godliving Mtui, alisema awali chuo
kilikuwa na uwezo wa kupokea
wanafunzi wachache wa masomo ya
sayansi, hivyo mkakati huo utapunguza uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru