Thursday 1 August 2013

UWT wamlilia Sarah Maemba


NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) umetuma salamu za rambi rambi kutokana na kifo cha Katibu wa UWT wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Sarah Maemba.
Akizungumzia kifo hicho jana, mjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa umoja huo Amina Makillagi, alisema UWT imempoteza kiongozi muhimu.
Amina alitoa salamu za pole kwa wanachama na viongozi wa umoja huo kwa kuondokewa na mpendwa wao na aliwataka wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
“UWT inaungana na ndugu, wana CCM na UWT wilayani Bunda, katika msiba huu mzito, kilichobakia sasa ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu, ili aipumzishe roho yake mahala pema peponi, Amin, ” alisema Amina.
Sarah alifariki Julai 30, mwaka huu katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza, ambako alilazwa kwa matibabu baada ya kuugua.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru