Thursday 3 April 2014

DPP aiwakia TPA

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Jinai nchini, Dk. Elieza Feleshi ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuhakikisha inakuwa na wanasheria wa kutosha na wenye uwezo ili kuweza kupunguza tatizo la kesi mbalimbali za jinai.
Alitoa agizo hilo jana wakati akifungua mafunzo ya wanasheria na maofisa ulinzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa  TPA yenye lengo la kuwajengea  uwezo wa kupeleleza, kufungua na kuendesha mashtaka.
Mafunzo hayo ni  moja ya mkakati wa TPA wa kukabiliana na uhalifu Bandarini.
Dk. Feleshi alisema ulinzi wa bandari lazima uimarishwe kwa kuweka mitambo maalumu itakayosaidia kutambua mizigo inayoingia na kutoka kwa lengo la kubaini na kutokomeza uhalifu mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari,   Kokutulage Kazaura alisema  mafunzo hayo yana manufaa makubwa kwa wanasheria na maofisa wa Ulinzi wa TPA kwa kuwa yatawajengea uwezo wa kuendesha kesi za jinai pasipo kufuata mfumo wa zamani.

"Mafunzo hayo yataiwezesha TPA kuendesha kesi za jinai na yatabadilisha mfumo uliotumiwa zamani wa kupeleka kesi Polisi na Taasisi za Mwanasheria Mkuu, badala yake zitaandaliwa na kuendeshwa na wanasheria wa mamlaka na hivyo kwa kiasi kikubwa zitaboresha huduma za kisheria katika Mamlaka,” alisema Kazaura.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru