Thursday 3 April 2014

TFDA yakamata bidhaa feki

NA RACHEL KYALA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imekamata bidhaa mbalimbali zisizokidhi viwango vya ubora zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria.
TFDA imebaini kuingizwa, kusambazwa na kuuzwa kwa bidhaa  za vyakula, dawa na vipodozi kutokana na ukaguzi iliyoufanya kwenye maduka 107  jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 10 hadi 21, mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, akizungumza Dar es Salaam jana, alisema jumla ya maduka 39 hayakuwa na kibali, hivyo yamefungwa hadi hapo yatakapotimiza masharti na sheria.

"Bidhaa tulizozikamata ni pamoja na maziwa ya watoto makopo 591, makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu, chumvi za kopo na paketi 6,090, vyote vikiwa na thamani ya takribani sh. milioni 30," alisema.

Aliongeza kuwa bidhaa zingine za vinywaji vyenye ladha ya matunda, ambavyo havikidhi kanuni ya vielelezo, vimezuiliwa kutumika kwa lengo la kuchukua hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuviharibu.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru