Friday 11 April 2014

Ndikilo aishangaa TFDA

NA PETER KATULANDA, MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo ameshangazwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), kutochangamkia kazi kwa wakati ili iende na kasi ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Alionyesha mshangao huo juzi wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha kuzalisha dawa za binaadamu cha Prince Pharmaceutical kilichojengwa Buhongwa wilayani Nyamagana.

Ndikilo alionyesha mshangao huo baada ya Meneja wa TFDA Kanda ya Mwanza kudai kuwa, Mamlaka yake itakagua kiwanda hicho mwishoni mwa mwezi huu.

Kiwanda hicho kitakachotoa fursa za ajira zaidi ya 100 kwa wananchi, kinatarajia kuanza uzalishaji mwishoni mwa mwezi huu baada ya ukaguzi huo, ingawa kingeweza kuanza hivi sasa iwapo kingekaguliwa.

“Hivi tukiwauliza TFDA, hapa katikati kutoka leo (juzi) Aprili 9 hadi Aprili 28, ni viwanda vingapi vya kukagua mtasema vipo vingi?” Alihoji Ndikilo kwa mshangao kabla ya kuwafanya wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo waangue kicheko.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru