Thursday 3 April 2014

Meya Mwanza aamuru machinga watimuliwe


NA PETER KATULANDA, MWANZA

ALIYEKUWA Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Charles Chinchibela (CHADEMA), amesema wafanyabiashara ndogondogo (machinga) jijini hapa ni kero na kutaka waondolewe kwenye maeneo yasiyotakiwa.

Chinchibela, ambaye ni Diwani wa Kata ta Mahina, amedai licha ya wafanyabiashara hao kutoiingizia mapato halmashuri hiyo, wanasabaisha msongamano usiokuwa wa lazima katika baadhi ya maeneo mjini.

Mawazo hayo yanatofautiana na ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, ambao wamekuwa wakiwashawishi machinga wasihame kwenye maeneo hayo, hali ambayo imekuwa ikisabaisha uvunjifu wa amani kila wanapojaribu kuondolewa.

Alisema hayo hivi karibuni wakati wa Baraza la Madiwani huku akishangazwa na kutoondolewa kwa machinga hao wakati jiji lilitenga sh. milioni 24 kwa ajili ya kuboresha maeneo wanayotakiwa kuhamia.

Mawazo, ambaye aliwahi kuwa Naibu Meya, alipinga zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao kwa kuwashirikisha mgambo wa Jiji.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru