Tuesday 1 April 2014

Jeshi la Polisi lakamata pikipiki 1031

NA WILLIAM SHECHAMBO

Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inazishikilia pikipiki 1,031 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya kuzuia vyombo hivyo kuingia eneo la kati ya Jiji.
Operesheni hiyo imeingia wiki ya pili sasa, ambapo zaidi ya sh. milioni 26. 2 zimekusanywa kutokana na faini mbalimbali wanazotozwa madereva wake.
Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema jana kuwa utekelezaji wa operesheni hiyo imefanyika kwa mujibu wa sheria za halmashauri zinazozuia vyombo vya usafiri vya aina hiyo kuingia eneo la katikati ya mji.
Alisema walibaini kuwa mafunzo kadhaa waliyotoa siku zilizopita bado yamekuwa hayazingatiwi na wamiliki na madereva wa vyombo hivyo na kwamba, wameendelea kuvunja sheria za usalama barabarani.

Hivyo kuwataka kuzingatia utii wa sheria bila shuruti ili waweze kuwa salama na mkono wa dola.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru