NA MUSSA YUSUPH
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, ameshangazwa na vitendo vya wajumbe wa bunge maalum la katiba vya kutoleana lugha za kashfa zisizoendana na maadili ya Kitanzania.
Alisema vitendo hivyo vinaashilia kuwa wajumbe hao hawathamini uwakilishi wao kwa Wananchi na kudharau mamlaka ya Rais aliyowateua.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Askofu Mwamalanga alisema kutofautiana kwa mawazo miongoni mwa wajumbe kusiwe sababu ya baadhi yao kuanza kutupiana maneno ya kejeri, kashfa na dharau, vitendo ambavyo havina tija kwa Taifa.
“Wajumbe hao wanapaswa kuzingatia maadili ya taifa na heshima yao kama Wawakilishi tunaowategemea katika kutuletea katiba bora, sasa kama wao wanaendelea kukashifiana ni kutudharau sisi kama Wananchi tunaowategemea,” alisema.
Thursday, 13 March 2014
Askofu awashangaa wajumbe Bunge la Katiba
00:51
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru