NA EPSON LUHWAGO, Dodoma
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Profesa Esther Mwaikambo, ameshauri wakati wa kujadili muundo wa serikali, wajumbe watafakari kwanza ustawi wa taifa.
Amesema mjadala wa Rasimu ya Katiba utakapoanza, wajiulize kama uwepo wa serikali tatu ndiyo matakwa ya wananchi au la.
Profesa Esther alisema wananchi wanataka maendeleo na si serikali tatu au moja, hivyo wajumbe wanapaswa kutambua vipaumbele vyao.
“Tunapaswa kujiuliza ni nini mahitaji halisi na muhimu ya wananchi. Sidhani mwananchi wa kawaida anataka muundo gani wa Muungano, anachohitaji ni huduma muhimu kama vile afya, elimu, barabara na usalama wake.
“Sioni mantiki ya kuanzisha tena serikali ya Tanganyika iliyokufa miaka mingi, wakati ule nikiwa nimeshajiunga chuo kikuu. Nashauri hilo lisitupotezee muda tukaacha mambo ya msingi,” alisema.
Profesa Esther alisema awali pamoja na wenzake waliingiwa wasiwasi kama azma ya kupata katiba ingetimia lakini baada ya kanuni za bunge kupatikana ana imani mambo yatakwenda vyema.
Thursday, 13 March 2014
Mjadala Rasimu ya Katiba uzingatie ustawi wa taifa
07:23
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru