Thursday, 13 March 2014

Mkosamali: Si kosa kutofautiana


NA CHARLES MGANGA, DODOMA
FELIX Mkosamali, amesema si kosa kutofautiana na mwenyekiti wake wa taifa wa chama, kwa sababu kila mmoja ana uhuru wa kuamua.
Mkosamali, ambaye ni mbunge wa Muhambwe (NCCR -Mageuzi), alisema licha ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, kuunga mkono Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, mawazo yake yalikuwa tofauti.
“Hakuna mnadhimu mkuu hapa, kila mmoja ana mawazo yake. Msimamo wangu siungi mkono rasimu ya kanuni, hayo ni mawazo yangu na si kosa kutofautiana na mwenyekiti wangu. Sina sababu ya kukubali kama wengine walivyofanya,” alisema.
Alilalama kuwa, Mwenyekiti wa Muda wa bunge, Pandu Ameir Kificho, hakuwapa fursa baadhi ya wajumbe kuchangia mijadala.
Wakati wa kupitisha rasimu ya kanuni Mbatia alisema bunge limeingia katika historia baada ya kutumia muda mfupi kuzifanyia kazi.
Alisema kuna nchi zilichukua muda mrefu kuandaa kanuni tofauti na wiki tatu zilizotumika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru