Wednesday, 19 March 2014

Wajumbe wapigwa msasa wa kanuni


NA CHARLES MGANGA, DODOMA
WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba jana walipigwa msasa kuhusu Kanuni za Bunge kabla ya kuanza kuijadili Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni juzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, aliwasilisha rasimu bungeni, ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, aliwataka wajumbe waipitie kwa makini.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Profesa Costa Mahalu, aliwaongoza wajumbe wenzake wa kamati kuwasilisha kwa wajumbe kanuni hizo.
Wengine waliofanya kazi hiyo ni Tundu Lissu, Ismail Jussa Ladhu, Dk. Tulia Ackson, Evord Mmanda na Amon Mpanju.
Sitta alisema juzi kuwa, semina kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, itapangiwa muda baadaye.
Awali ilipangwa kuwa Watanzania sita, watatu kutoka Tanzania Bara na wengine kutoka Zanzibar wangetoa elimu kuhusu historia ya Muungano.
Mwenyekiti Sitta alisema Wakenya wawili wangetoa semina kuhusu masuala ya katiba kwa jumla.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru