Thursday, 15 May 2014

Kinana kushusha mzigo kwa JK


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema kilio hicho cha wakulima wa tumbaku, atakifikisha kwa Rais Jakaya Kikwete, ili aweze kuchukua hatua zaidi za kisheria.

Alisema kuna uozo wa kutupwa kwenye sekta ya tumbaka na amevitaka vyama vya ushirika kuwa tayari kubeba lawama za wakulima.
Kinana alisema amepata taarifa za kutosha na amebaini kuna dhuluma na unyanyasaji mkubwa wanaofanyiwa wakulima wa Tumbaku.

”Taarifa ya uozo wa tumbaku inasikitisha, ni vyema taarifa hiyo wameieleza wenyewe wakulima, maana tukisema sisi, tunaambiwa tuna chuki, lakini hatuna chuki, tunawataka waliopewa madaraka warudi kwa wananchi kuwatatulia shida zao,” alisema.
Alisema waliopewa kusimamia matatizo ya wananchi, waache kukaa maofisini Dar es Salaam, badala yake waende mikoani kusikiliza matatizo ya wananchi.
Kinana alisema ni jambo la kushangaza wilaya moja kuwa na vyama vya ushirika zaidi ya 59, ambavyo vyote vimeanzishwa na watu wanaotaka uongozi.
Alisema wakati wa utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Ali Hassan Mwinyi, kila wilaya ilikuwa na chama kimoja cha ushirika.
Kinana alisema zao la tumbaku linahitaji kutazamwa kwa darubini ili kama kuna ulaji ushughulikiwe na kama vyama ni vingi viangaliwe upya.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru