Thursday, 15 May 2014

Mbunge Nkumba aibua mazito


Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba, alisema taarifa ya ukaguzi ya mkoa wa Tabora, imebainisha kuwa, viongozi wa vyama vya ushirika ni wezi na hawafanyi kazi kwa ubadhirifu.
Alisema ni vyema waliohusika na wizi wa mabilioni hayo ya fedha wapelekwe mahakamani mara moja ili haki itendeke.
Nkumba aliwataka wakulima kuwa macho na kwamba ushirika ni wa wanachama na sio wa viongozi wanaowakandamiza wakulima.
Alisema sheria ya ushirika iliyopitishwa na bunge inaeleza kuwa, yeyote atakayehusika na ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika, afilisiwe na mahakama.
Hata hivyo, Nkumba alisema pamoja na sheria hiyo kupitishwa, hadi sasa haijatungiwa kanuni na haijaanza kufanyakazi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru