NA mwandishi wetu, dodoma
SERIKALI inalifanyia kazi tatizo la madai ya malipo ya mishahara ya wafanyakzi wa Mamalaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kurejesha huduma ya usafiri.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo.
Pinda, alisema suala hilo la madai ya wafanyakazi limechukuliwa kwa uzito na serikali na sasa inaendelea kulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi.
“Serikali kwa sasa inaendelea kushughulikia suala hilo na kwa imani yangu, litaisha haraka iwezekanvyo,’’ alisema.
Pinda, alisema ingawa ni ukweli usiopingika kuwa reli hiyo inatumika na wananchi wengi kutokana na mafuriko katika maeneo mbalimbali inakopita, pia Serikali inafuatilia kwa karibu hali hiyo ya mafuriko.
Waziri Mkuu Pinda, alisema mvua iliyonyesha Mkoani Morogoro, ilikuwa ni nyingi na imeathiri kivuko cha Kilombero.
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Suzan Kiwanga (Viti Maalumu-CHADEMA).
Katika swali lake, Susan alisema, mafuriko yaliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha yamesababisha kata 14 kati ya 23 za Wilaya ya Kilombelo kukosa mawasilano.
Kwa mujibu wa Susan, wakazi wa kata hizo wanategemea mawasiliano ya reli ya TAZARA ambayo nayo kwa sasa wafanyakazi wake wamegoma na hivyo kufanya hali ya usafiri kuwa ngumu.
Thursday, 15 May 2014
Serikali kutatua kero ya mishahara TAZARA
07:45
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru