NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP Limited, Dk. Reginald Mengi, amesema kuwa tuhuma mbalimbali zilizosambazwa kupitia ujumbe mfupi wa simu na mitandao ya kijamii juu yake ni za uongo, chuki na uzushi.
Dk. Mengi aliyasema hayo jana kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma, kwa maelezo kwamba hivi karibuni ameshuhudia kusambazwa kwa taarifa kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms) na mitandao ya kijamii zikimhusisha na tuhuma mbalimbali.
"Napenda kuufahamisha umma kwamba taarifa zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za uongo, chuki na uzushi.
ìKilichonisikitisha sana ni kuona kuwa uzushi huo unachochea kuifarakanisha jamii yetu kwa misingi ya ukabila, ambalo ni hatari kwa umoja na mshikamano, ambao Tanzania tumejitahidi sana kuujenga na mtu yeyote anayediriki kuleta uchochezi wa kikabila, hastahili kuwa kiongozi wa ngazi yoyote katika taifa letu,î alisema.
Dk. Mengi aliongeza kuwa, amekuwa ni miongoni mwa Watanzania walio mstari wa mbele wanaomuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kusisitiza kuwa rasilimali za asili zilizopo nchini ni mali ya Watanzania, na ni lazima wawe wamiliki wakuu wa rasilimali hizo na gesi asilia.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni, dhana ya Watanzania kuwezeshwa na kumiliki uchumi wa nchi yao, imetambuliwa na serikali na Chama tawala.
Mwenyekiti Mtendaji huyo wa IPP, alisema amekuwa akiishawishi serikali kutekeleza sera na sheria ya uwekezaji ili kuwashirikisha Watanzania kikamilifu katika uchumi wa taifa na kwa sasa katika uchumi wa gesi asilia ili kudumisha amani na utulivu nchini.
Thursday, 29 May 2014
Mengi akana tuhuma alizozushiwa
01:17
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru