na mwandishi wetu
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa anatarajia kuhitisha mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili mustakabali wa Bunge Maalum la Katiba na kuhakikisha katiba Mpya na bora inapatikana.
Msemaji wa Ofisi hiyo Sisty Nyahoza amewaasa wajumbe wote wa Baraza la vyama vya Siasa nchini kuhudhuria mkutano wa Baraza hilo unaotarajiwa kufanyika Mei 9, mwaka huu.
Nyahoza alisema mkutano huo utajumuisha wanasiasa na watu mashuhuri kutoka Tanzania bara na visiwani,wakiwemo viongozi wa dini.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini hapa, alisema mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
“Huu ni mkutano muhimu katika tasnia ya Siasa nchini hasa mchakato wa Bunge maalum la katiba,na utaaangalia namna mchakato wa Bunge hilo ulivyokwenda na hatma yake,” alisema Nyahoza.
Alisema mkutano huo hauna lengo la kujadili kuhusu mfumo wa serikali ya idadi ya Serikali mbili ama tatu bali kupata mawazo ya kusaidia kunusuru Bunge maalum la katiba katiba mpya.
Alisema wajumbe wa Baraza hilo ni viongozi wakuu wa vyama vya Siasa nchini, lakini kwa umuhimu wa shughuli yenyewe kuna wageni waalikwa ambao pia watahudhuria mkutano huo.
Alisema jumla ya wajumbe 80 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ajenda Kuu ya mkutano huo ni mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba.
Aidha Nyahoza alisema, wajumbe wa Bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia waliosusia Bunge hawajasukuma kufanyika kwa mkutano huo.
Hata hivyo, alisema jambo hilo pamoja na yote ambayo wajumbe wataona yalikuwa ni changamoto ndani ya bunge maalum yatajadiliwa.
Thursday, 8 May 2014
Msajili ajitosa kunusuru Katiba
02:26
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru