Monday 10 February 2014

EFD ni lazima zitumiwe na Wafanyabiashara nchini - KAYOMBO

NA mwandishi wetu

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema wafanyabiashara wanapaswa kufuata sheria na matumizi ya mashine za kielectronics (EFD) hayatasitishwa.

Richard Kayombo Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alitoa msimamo huo jana alipozungumza na Uhuru kuhusu mgomo wa wafanyabiashara.
Baadhi ya wafanyabiashara jijiji Dar es Salaam na mikoa ya Iringa na Mara jana waligoma kufungua maduka kupinga matumizi ya mashine hizo.

"Msimamo wa serikali upo pale pale hakuna mabadiliko, wafanyabiashara wanatakiwa kutumia mashine hizo na kama elimu ilishatolewa na kwa ambaye bado aje tupo tutamuelekeza," alisema.
Aliongeza kuwa mfanyabiashara ambaye hataki kutumia mashine hizo aendelee kutofungua duka na asijaribu kushawishi wengine kwa kuwa ni kinyume cha sheria na atachukuliwa hatua.
Alisema wafanyabiashara walipewa muda wa kutosha kujiandaa na matumizi ya mashine hizo hivyo, kinachotakiwa kwa sasa ni utekelezaji tu.

Mgomo huo unatokea kwa mara ya tatu kwa wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo kufunga maduka yao wakigomea kutumia mashine hizo.

1 comments:

  1. Wafaanyi biasharabhawa wanalalamika kwamba mashine hizo zitawletea hasara kisisa bila ya kuthibitisha kauli yao. Hata hivyo yaelekea kuwa ni mbumbu au ukorofi tuu ambao unaendeshwa kwa makusudi ili kuona serikali itafanya nini.

    ReplyDelete