Tuesday, 6 May 2014

Tanroads kujenga barabara ya Namtumbo-Tunduru


Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS), umetia saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Namtumbo-Tunduru, kuanzia Kilimasera mpaka Matemanga.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 68.2, ni sehemu ya barabara ya Namtumbo-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193, ambayo imegawanywa katika sehemu tatu kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Ujenzi kwa vyombo vya habari  ilisema serikali itagharamia ujenzi wa barabara hiyo kupitia mkopo kutoka Benki ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).
Ilisema mkopo huo ni kwa ajili ya mradi wa Road Sector Support Project 1 (RSSP 1), unaohusisha ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara za Iringa – Dodoma (km 260 ), Namtumbo –Tunduru ( km 193).
Taarifa hiyo ilisema mkopo wa mradi huo ulitiwa saini Machi mwaka 2010 na kwamba una thamani ya sh. bilioni 472.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkataba wa ujenzi wa barabara za Namtumbo-Kilimasera na Matemanga-Tunduru,  ulitiwa saini Februari 17, mwaka huu.
Ilisema mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kilimasera-Matemanga yenye urefu wa kilometa 68.2 ulitiwa saini Aprili 30, mwaka huu.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru