Tuesday 6 May 2014

Vijana kuweni wazalendo- Angela


Na Mwandishi Wetu
VIJANA nchini wametakiwa  kuwa wazalendo na  nchi yao na kuacha kushawishika na vyama vyenye uchu wa madaraka.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa, wilaya ya Temeke, Angela Akilimali alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na vijana pamoja na chipukizi wa kata ya Tuangoma, Kigamboni, Dar es Salaam.
Alisema maisha bora kwa kila kijana hayaji kwa kukaa vijiweni, badala yake kila kijana anatakiwa kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupata fursa zinazotoka serikalini.
Angela alisema vijana ni chachu ya maendeleo ya Chama na taifa na kwamba kumuinua chipukizi mmoja ni sawa na kuiinua familia nzima,  hivyo jamii na viongozi wanapaswa kuwathamini vijana kwani ndio taifa la kesho.
 Aliwataka vijana kutumia fursa zinazotolewa na serikali kwa kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.
Angela alisema wakati umefika vijana wawe wazalendo na wasishawishike  na maneno ya upotoshaji yanayotolewa  na UKAWA bungeni  kwani lengo lao ni kuwapotosha wananchi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru