Tuesday, 6 May 2014

Wakuu wa wilaya wapewa tahadhari


NA WILLIAM SHECHAMBO
WAKUU wa wilaya nchini wameaswa kutopuuzia tamko la serikali kuhusu ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari kabla ya kufikia Oktoba mwakani.
Tamko la ujenzi huo lilitolewa mapema mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete, ili kutoa muamko kwa wanafunzi kuchukua masomo ya sayansi na hatimaye kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini.  
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa, jumla ya shule 1,200 zimekamilisha ujenzi huo wa maabara na zinaendelea na hatua ya kuweka vifaa ili zianze kutumika.
Alisema shule ambazo hazijakamilisha au kuanza mchakato huo, wakuu wa wilaya na halmashauri husika zinapaswa kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi huo haraka iwezekanavyo.
Alisema serikali inatoa mchango wa hali na mali ili kufanikisha jukumu hilo kwa kuruhusu matumizi ya asilimia 50 ya fungu la ruzuku kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara. 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru