NA MWANDISHI WETU-MUSOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, kimesema kazi iliyopo kwa sasa ni kuendelea kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia kimesema wataendelea kuunganisha nguvu za wanachama na wapenzi katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Kauli hiyo ilitolewa na viongozi wa CCM katika uwanja wa shule ya msingi Nyamatare, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufungua ofisi ya kisasa na kupokea wanachama wapya 47 kutoka CHADEMA.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Vedastus Mathayo, alisema watahakikisha kila kata kwenye Manispaa ya Musoma inakuwa na ofisi ya kisasa ili kuongeza ufanisi kwa watendaji wake.
Alisema kata zote 13 zitakuwa na ofisi za kisasa pamoja na kuwekwa thamani za ofisi na kwamba zitakamilika kabla ya uchaguzi mkuu ujao kwa kushirikiana na makada wengine wa CCM.
Matayo alisema kila mwanachama kwa nafasi yake, anayo dhamana ya kuhakikisha Chama kinazidi kuwa imara na kuwatumikia wananchi kwa bidii.
“Wana CCM Musoma wasijione wanyonge kupoteza jimbo pamoja na halmashauri bali watumie muda huu kujiimarisha zaidi na kufanya kazi za chama na kutafuta wanachama wapya,” alisema.
Akipokea wanachama 47 kutoka CHADEMA, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Christopher Sanya, alisema ameendelea kupokea wanachama kutoka upinzani baada ya kuona wanadanganywa.
Tuesday, 6 May 2014
CCM yaipa maumivu CHADEMA
07:46
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru