Sunday 7 July 2013

Exim yaanzisha mfumo mpya


Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim imeanzisha mfumo mpya ili kupunguza foleni ndani ya matawi yake na kuboresha huduma za kibenki.
Mfumo huo ‘Queue Management System’ umeanza kutumika kwa mwezi mmoja sasa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro,  alisema jana kuwa, mfumo huo utasaidia kukuza utoaji huduma kwa wateja kwa wakati.
Alisema taarifa za mfumo huo zitakuwa zikitumwa kila wiki kwa wakuu wa matawi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Matoro alisema benki hiyo pia   imeanzisha huduma ya ‘kuchati’ mtandaoni, ikiwa ni nafasi ya wateja kutoa maoni na matatizo yao kwa wawakilishi wa benki.
Naye Meneja Mauzo wa Benki ya Exim, Heena Khakharia, alisema benki itaendelea kujikita katika kufanya utafiti ili kuvumbua bidhaa za kibenki za kipekeeν

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru