Thursday 4 July 2013

Phil Neville, Giggs kumsaidia Moyes

KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes ameanza kazi kwa kupanga safu ya benchi la ufundi kwa kuwajumuisha wakongwe wa klabu hiyo.
Phil Neville, ambaye ameichezea Man Utd kwa muda mrefu kabla ya kujiunga na Everton, atakuwa katika benchi akimsaidia Moyes. Winga mahiri na mchezaji wa karne Ryan Giggs naye amepewa kazi ya ukocha japo atakuwa akicheza pale inapohitajika. Lengo la Moyes ni kusuka kikosi imara na ameanza kutafuta sapoti ya wakongwe ili kuleta ushawishi na utulivu katika vyumba vya kubadilishia nguo.

 
PHIL Neville (kushoto) akifanya mazoezi na kaka yake Garry. Wote wamekulia na kucheza soka Old Trafford.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru