NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
MIRADI saba yenye thamani ya sh. milioni 510 inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Gairo mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Khanifa Karamagi alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema Mwenge wa Uhuru utapokewa leo katika mpaka wa Mkoa wa Morogoro na Dodoma ukitokea wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Khanifa alisem kati ya miradi itakayozinduliwa katika wilaya hiyo ni nyumba mbili za kuishi watumishi wa mamlaka ya mji mdogo wa Gairo na nyumba ya kulala wageni iliyopo katika eneo la Ukwamani Gairo, zahanati ya Kijiji cha Madege na mradi wa shamba darasa la ufugaji nyuki na hifadhi ya mazingira Kata ya Msingisi.
Kwa upande wa miradi itakayowekewa mawe ya msingi ni zahanati katika Kijiji cha Kwipipa na mradi wa uchimbaji kisima cha maji Kata ya Kibedya na ujenzi wa nyumba ya mwalimu Chakwale.
Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru wananchi kwa kuchangia nguvu na mali zao katika maandalizi hayo na kuwataka kujitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo.
Monday, 16 June 2014
Mwenge kuzindua miradi ya mamilioni wilayani Gairo
08:53
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru