NA RACHEL KYALA
SERIKALI kwa mara ya kwanza imetoa fursa kwa wananchi ya kuwekeza kwa kununua hisa katika sekta ya mafuta na gesi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia serikali kutoa kibali kwa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala, kuwa ya kwanza kuuza hisa Afrika Mashariki na kumilikiwa na wazawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swala, David Ridge, akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa uuzaji wa hisa, aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili kuinua uchumi wao na wa taifa kwa jumla.
“Utafiti wa awali unaonyesha kuna dalili nzuri ya kuwepo kwa mafuta na gesi katika maeneo ya Kilosa, Kilombero na Pangani kwani yapo katika ukanda mmoja wa bonde la ufa na eneo la Lake Turkana nchini Uganda, ambako tulifanikiwa kupata mafuta kwa wingi,” alisema.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Swala Tanzania, Abdullah Mwinyi, alisema hisa zilianza kuuzwa rasmi jana, ikiwa ni wiki moja tu baada ya kupata idhini kutoka Mamlaka ya Masoko na Mitaji Tanzania (CMSA) ambapo ni ofa ya kwanza katika sekta hiyo.
Tuesday, 10 June 2014
‘Ruksa kununua hisa mafuta na gesi’
09:02
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru