NA WILLIAM SHECHAMBO
WANAWAKE 30 wamejitokeza kupima afya zao ikiwemo saratani za kizazi na matiti kwenye banda la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Mmoja wa madaktari wa taasisi hiyo, Dk. Rehema Ngomola, alisema kati ya kinamama hao, mmoja ndiye aliyekutwa na viashiria vya saratani ya kizazi.
Alisema kutokana na takwimu hizo, idadi ya kinamama wenye maradhi ya ya saratani ya matiti na kizazi, inapungua hivyo kuwataka kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutambua afya zao.
Alisema lengo lakutoa huduma hiyo katika maonyesho hayo imetokana na kugundulika kuwa wanawake wengi kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na matiti.
“Tumeamua kuleta huduma hii hapa, kutokana na kwamba wakina mama wengi wamekuwa na magonjwa hayam, lakini kutokana na idadi hii tuliyopima tunaweza kupata matumaini kuwa kidogo inapungua,” alisema Dk. Rehema.
Aidha alisema kinamama wanatakiwa kupima afya zao mapema kwa ajili ya kupatiwa matibabu haraka ili kuepusha wadudu kuwashambulia zaidi jambo linaloweza kuharibu kizazi.
Alisema mbali na kupima saratani, pia wamegundulika kuwa na maradhi ambayo ni ya kuambukiza.
Monday, 30 June 2014
Wanawake 30 wapima kansa Sabasaba
22:19
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru