Monday 1 July 2013

Ilipojificha siri ya kujiamini Rais Obama


NA MWANDISHI WETU
HAKUNA anayebisha kuwa Rais Barack Huusein Obama ndiye kiongozi wa taifa lenye nguvu kubwa kuliko yote duniani.
Pia, hakuna anayebisha kuwa ushindi wa Rzais Obama katika uchaguzi mkuu wa Marekani umeweka historia ya kutukuka kwa bara la Afrika kutokana na kuwa kiongozi wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuchaguliwa kuongoza taifa hilo.
Na hakuna ubishi kuwa kiongozi huyo amekuwa na mvuto mkubwa miongoni mwa jamii ya Wamarekani kiasi kwamba alifanikiwa kuibuka na ushindi kwenye uchaguzu wa awamu ya pili ambao ulikuwa na ushindani mkali kuliko ule wa kwanza.
Wengi wanajiuliza ujasiri na kujiamini kwa Rais Obama kunatoka wapi, kwani kuna viongozi wengi wamepita, lakini yeye amekuwa na mvuto mkubwa hasa kwa vyombo vya habari.
Jibu la swali hilo ni kuwa nyuma yake yupo Michelle Obama ambaye amepata umaarufu mkubwa kwa Wamarekani kuliko hata mumewe.
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais Obama alikiri kuwa Michelle ni maarufu kuliko yeye.
Akihutubia moja ya mikutano hiyo mbele ya mwanamuziki Shawn Knowles-Carter, (Jay Z ) ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa, Rais Obama alikaririwa kisema kuwa kuna sifa moja ambaya anafanan na mwanamuziki huyo nayo ni kuwa wake zao ni maarufu  kuliko wao. Mke wa Jay Z ni mwanamuziki Beyonce.
Rais Obama na mkewe Michelle Robinson walioana mwaka 1992, ikiwa ni baadayta miaka mitatu ya uhusiano wa kirafiki ambao ulianza wakati Obama akifanyakazi kwenye Kampuni ya uwakili ya Sidley Austin LLP ya Chicago.
Michelle alizaliwa  Januari 17, 1964 huko Chicago na kufanikiwa kupata Digrii ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Havard mwaka 1988. Baada ya hapo alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni ya uwakili na ambako alikutana na Rais Obama.
Baada ya Rais Obama kuingia madarakani, Michelle amekuwa akijihusisha na masuala ya kijamii ikiwemo kuhimiza umuhimu wa kufanya mazoezi na kula kwa mpangilio mzuri, mambo ambayo yamemfanya kupata umaarufu mkubwa kwa yeye binafsi na sio kama mke wa rais.
Michelle ambaye na Rais Obama wamefanikiwa kupata watoto wawili Malia aliyezaliwa 1998 na Natasha maarufu Shasa aliyezaliwa mwaka 2000, alianza kuvuta hisia za vyombo vya habari mwaka 2004, alipoonekana akiwa pembeni ya mumewe wakati akitoa hutiba baada ya kuchaguliwa kuwa Seneta wa Illinois.
Aliendelea kuvuta hisia hizo mwaka 2007, aliposhiriki kikamilifu kampeni za Rais Obama kutaka ateuliwa kuwania urais kupitia chama cha Democratic.
Baada ya hapo majarida mbalimbali yalianza kuchapisha habari zake yakimtaja kama mmoja wa wanawake wanaovaa ngu kwa mitindo mizuri na wanawake wenye mvuto.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru