Friday 27 June 2014

Airo atoa vifaa kujengea shule



Na Samson  Chacha, Rorya 
MBUNGE wa Rorya, Lameck Airo (CCM)  ametoa msaada wa mabati 46 na ifuko 20 ya saruji kwa Shule ya msingi Nyanjogo iliyoko kata ya Goribe
Alitoa msaada huo katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza ulinzi shirikishi na kuendesha .
Airo aliwataka wananchi kushirikiana na kufanya msako makali wa wezi wa mifugo kwatika wilaya yao ambayo wizi huo umeshika kasi na kusababisha wananchi kukesha kwa ajili ya kulinda mifugo yao.

'Nawachangia mabati  46 na saruji  mifuko  20 kuwaunga mkono katika ujenzi wa madarasa katika shule hii ya Nyanjogo na pia kuhamazisha  kuhusu wananchi kushiriki katika ulinzi shirikishi,"alisema


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru